Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Mbowe ameshazungumza kuonesha msimamo wake, ajabu nyie bado mnaamini hisia zenu, hebu acheni kuishi kama mnatembea barabarani huku mnaota ndoto mchana wa jua kali, amkeni!.
Muda wote alikuwa wapi mpaka anaongea sasa hivi au kaona kule kwenye bank kumemgusa mimi ndio maana siwaamini Wanasiasa wote wapo kimaslahi tofauti yao ni Moja mmoja yupo madarakani mwingine anasaka madaraka kwa kutumia matatizo ya wananchi
 
Kama ni hivyo angeweza pia kuamua kukaa kimya tu badala ya kuhadaa watu ambao tayari wana shida na wanaumia, siyo vizuri kumkejeli mtu ambaye anataabika tayari!
Wewe unayewaza ujinga ndiye unayewaza hivyo ila wenye busara wanajua kaongea mambo ya msingi.
 
Hii kauli ya Mbowe kwamba "nakwazika sana kuona wanakuwa waoga" inaonesha bado ana dhamira ya dhati kuleta mabadiliko nchi hii.

Kinachomkwamisha ni kukosekana kwa ushirikiano anaohitaji toka kwetu, tupo kama misukule ndio maana naye anajua hilo, japo ameshindwa kutumia hilo neno kwa heshima yake aliyonayo kwetu.

Naamini wale wajuaji wanaosema kila siku Mbowe amelamba asali ndio maana yupo kimya, sasa ni wakati wao kum-prove wrong Mbowe, simameni mhesabiwe kulinda haki zenu ili Mbowe awe pamoja nanyi.
Iitaridhisha kuona upinzani wa Mbowe upo imara ikiwa atailazimisha serikali kuruhusu mikutano ya kisiasa ambayo si ya kujificha mahala.

Pili, itaridhisha serikali ikikiruhusu chama cha Umoja kuendelea na shughuli zake za kisiasa na wanachama wake kuendelea kusambaza ujumbe ulobeba malengo na dhamira ya chama hicho.

Tatu, serikali kupitia TCRA iwaruhusu wale wanojitoa kuwaelimisha watanzania juu ya haki zao na mfano mmoja ni Humphrey Poleople arudishiwe tovuti na mtandao wake wa Shule ya Uongozi.

Nne, Tundu Lissu, Zitto Kabwe na wapinzani wengine wote wajiunge pamoja wakitoa kauli za kweli za upinzani na sio kukaa kimya baada ya Lissu kupoozwa au Zitto Kabwe kujipooza mwenyewe kwa kauli yake ya kijinga kwamba "watu wanomuenzi hayati JPM wakazikwe nae kule Chato".

Tano, serikali iruhusu mchakato wa katiba mpya uendelee kwa kuwapa nafasi wananchi wapige kura ya maoni. Wananchi wakiamua tubadili katiba inakuwa kheri la wakikataa hiyo pia yawa ni uamuzi wa wengi na itasemwa kuwa tumejaribu.

Serikali ionekane yakubali kupingwa au kukosolewa kwa staha bila kuchukua hatua kali za kuwaadhibu raia wake kwani wanatumia haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni.

Hiyo iendane na kumuachia yule kijana wa TRA aendelee na maisha yake bila kubugudhiwa kwani ametumia haki yake ya msingi ya kutoa maoni ambayo kiukweli haiwezi kuiangusha serikali au kuikebehi bali inaipa mwamko wa kufikiri zaidi juu ya hizi tozo za zaida.

Nchi ikiwa na watu wenye mawazo tofauti ndo huwa chachu ya kuleta maendeleo kwani kiujanja serikali inakuwa yatumia mawazo ya wapinzani kutekeleza mipango yake.

Ni dhahiri serikali imeshindwa kukusanya kodi na fedha zinokusanywa kama ushuru katika mikoa yote ya Tanzania zinaibwa. Kwa mfano Waziri mkuu Kassim Majaliwa alipokwenda kwenye moja ya halmashauri nchini alikuta kuna mchezo wa kuonyesha mapato ya milioni 2 hadi 3 lakini kumbe kuna zaidi ya fedha milioni hadi 4 na nusu hio kuonyesha kwamba badoi upogaji upo na wafumbiwa macho.

Serikali iketi tena na washauri wake wa uchumi kutathmini hizi tozo zisizo na maana ambazo zinaumiza wananchi.

Kisha serikali ikazanie kukusanya kodi kwa kila afanyae biashara halali nchini na iwe ni sheria kwamba ukikutwa unakwepa kodi basi kuna adhabu ya malipo zaidi.

Hata TRA wakikuta mtu hajalipa kodi ni wajibu wao kuketi na mtu huyo ili wapange namna ya kulipa "arrears" hizo kwa awamu hadi amalize lakini lengo likiwa lilelile kuhakikisha kila mtanzania mwenye shughuli za kuingiza fedha alipa kodi.

Mbona masuala haya ni rahisi sana kuonekana kwenye macho ya watanzania?, miaka mitano ilopita Tanzania iliweza kufikia uchumi wa kati ya kusifiwa hata na hao IMF na Benki tya Dunia, leo hii imekuwaje tena serikali imebadili gia angani na kuharibu kila chema kilichobuniwa na kiongozi aliepita?

Hakika sasa Mbowe kaibuka na ametoa neno na aungwe mkono na hii iwe twasema kwa kiingereza "Moment of truth" au wakati wa kufanya kweli.
 
Siku hizi kuweka fedha bank imekuwa si kimbilio tena. Pesa ikikaa muda bila kufanyiwa transaction yoyote unakuta imekatwa bila sababu ya msingi na maelezo yasiyojitosheleza, imekuwa sawa na kuweka salio kwenye simu(voda) na uliache bila kujiunga! Wanakukata kwa lazima! Ili utafute ya kujazia
 
Maneno MAZITO....Kiongozi anaongea TAIFA zima LINAMSIKILIZA....
 
Kuonyesha Chadema tunapinga matumizi ya ma V8 serikalini, tulimbembeleza Mbowe asikubali kupokea gari hili kwani lingefifisha kelele zetu hakutusikia. Leo kalirudisha ndio akumbuka kumbe alikuwa anatembelea gari litokanalo na kodi za wananchi.
images (1).jpeg
 
Hoja nzuri.

Bt tuseme Kweli, Mnyika anaweza akasimama jukwaani na kumwambia mwananchi haya?

Ndugu wananchi, mmetozwa tozo, mmeminywa Kodi Kila Mahali, nichagueni niwawakilishe,

Nitapofika bungeni nitalipwa zaidi ya ml 12 Kwa mwezi, Nitakopeshwa gari ya ml 800 na ntailipa polepole ingawa najua wananchi wengi hapa wanamiliki BAISKELI. Pia wanakosa pesa za matibabu wakiugua.

Nikimaliza ubunge mtanilipa zaidi ya ml 200 kama Asante ya kuwatumikia.


Jambo hili ni la kimfumo. Tuwabane kwenye KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ameeen.

..hoja yako inafikirisha.

..naunga mkono katiba mpya.

..lakini pia lazima tuchague Raisi na wabunge kwa namna ambayo itawezesha mfumo na katiba kufanya kazi.

..tuige mfano wa Wamarekani. Wao wakichagua Raisi toka Democrat, basi bungeni huchagua Republican wengi zaidi.

..Ni lazima tujenge utamaduni wa kuwawajibisha na kuwabadilisha viongozi wanaopigiwa kura.
 
Anaongea nini huyo nae, atulie hakuna wa kumsikiliza.
Angekuwa ni mtumishi wa umma ndiyo kasema hivi! mngemfukuza kazi, mngemkamata na kumfungulia mashtaka ya utovu wa nidhamu, na bla bla nyingine!

Ila kwa huyu jamaa; mtafyata tu mikia yenu. Maana mkijiroga tu kumkamata, mnajua fika shughuli ya akina Kibatala na wenzake.
 
Siamini tena CHADEMA kuanzia pale mulipomuuzia lowassa chama chenu, hadi kuwapoteza zitto na slaa, siasa za tz ni za ovyo sana. usimwamini mwanasiasa. amini nakuambia
 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kinachoendelea katika ajira ya Watumishi ni kukatwa kodi mara mbili.

Hizi hapa nukuu za Mbowe...

“Tunapowapa Watawala nafasi ya kuongoza maisha yetu na wanaamua bila kujali kinachotupata, hatupaswi kuwa waoga.

Kuna wakati nakwazika sana kwa kazi ninayofanya mnapokuwa waoga na hofu, halafu mnalalamika.

Hao wanaowatoza kodi hiyo wanakwenda kununua V8 ya Shilingi Milioni 450 au 500, mtu ambaye angekuwa nyumbani kwa mumewe au mkewe asingeweza kununua V8.

Lakini kwa kuwa kuna pesa ya Wajinga Watanzania wanaweza kununua gari la kumpa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Jaji kila mmoja.

Jiulizeni ni Wafanyabiashara wangapi ambao wana uwezo wa kuendesha magari mapya?

Magari mapya Nchi hii ni mali ya viongozi wa Serikali, na mnavyokaa kimya mambo haya ndiyo yanaendelea, mnatakiwa kuamka.

Kama mnataka kuibadilisa Nchi hii lazima tuache woga, lazima viongozi wa dini muongee.

Nilimwambia Rais Samia hii simulizi ya ‘amani’ ‘amani’ ‘amani’ ni kupoteza muda, simulizi sahihi ni haki haki haki.

Kuwepo na haki kwa watu wote litakuwa tafa bora la kuishi. Watanzania wameangalia uchaguzi wa Kenya kila mmoja ametamani, ulikuwa wa wazi hakuna mizengwe
Uchaguzi wa Kenya hauna mizengwe
 
Back
Top Bottom