Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Hana lolote huyo! Hata yeye anamgao wa hizo tozo ndio maana anaongea kwa kuvizia.
 
kwa mantiki yake ni kapinga izo tozo ila raia wa kawaida kama yule meneja wa TRC kapinga kidogo adi maabusu kaenda
why??
 
Makanisa yatuondolee pepo la tozo kwenye mabenki.
 
TISS wapo kazini kupitia mbowe
Ya Mbowe ni mmoja wa hao jamaa, siku Mungu akimchukua ndio tutakuja kuona wasifu wa cheo chake ktk hicho kitengo kama tulivyoona kwa Mrema. Kwa sasa anajifanya kuchokonoa mzinga wa nyuki afu wale watakaongia mkenge kuhusu kauli yake waingie ndan ya mikono ya dola.
Kalagha baho kwa wale wote wanaofikiri kuwa Mbowe alimaanisha.
 
Wewe unafanya nini? AU ni Usalama?
Usalama ni yeye na wenzake. Kama hauamini ingia barabarani uone kama haujachezea kichapo na ikulu hautaitwa kama alivyoitwa yeye. Kama unafikiri jamaa ni mtu wa kawaid kama ulivyo wewe basi kalagha baho.
 
Katika magari mengi yanayonunukiwa na Serikali hizo V8 ni kwa viongozi wachache wa ngazi za Juu kuanzia makatibu wakuu, Mawaziri,majaji na wakuu wa Taasisi wengine wote ni magari ya kawaida..

Gharama ya manunuzi na uendeshaji ni zaidi ya bil.554 kwa mwaka na ndio Serikali Ili propose ku cut hii to only 50 bln bado mkawa mnapinga..

..Ccm ndio wenye bunge na serikali hakuna anayeweza kuwapinga.

..billion 500++ kutumiwa kwa anasa na watu wachache ni ubinafsi na ufisadi uliopitiliza.
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu,pole sana.
Hivi ushahidi wa kuwa alikopeshwa hilo gari unao au unaropoka tu???
Mimi nina shida sana na watu wajinga kama huyu unayemjibu mkuu. Badala ya kuangalia hoja anachambua mtoa hoja. Ameambiwa kuwa tozo ni nyingi matumzi yake ni hayo ya mav8 lakini aisee tuna safari!!
 
Baadae atampigia mama simu amwambie asimuelewe vibaya, ameamua kujitokeza ili kuwazubaisha na kuwahadaa wadanganyika, baada ya malalamiko mengi juu ya ukimya wake.

Kalagha baho kwa wale wote wanaofikiri kuwa Mbowe alimaanisha. Siku Mungu akimchukua wengi mtashangaa mtaposikia wasifu wa cheo chake kweny kile kitengo cha "gizani".

Hata Mrema wengi walipinga juu ya utumishi wake pale kitengoni, tuliaminishwa kuwa ni kiongozi wa upinzani alienyima mzee Mwinyi usingizi mwaka 1994 to 1995.
Lkn juzi kila kitu kiliwekwa wazi baada ya kifo chake, alikuwa mtumishi alietukuka pale kitengoni. RIP Mrema umetuachia somo la kujitafakari upya kuhusu huu upinzani butu wa Tanzania.
Ona hili zezeta hapa! Kuna uwongo ameongea! ?? Jamani watanzania waachwe wateseke hadi "walimie meno" JPM quote.
Mwigulu ongeza tozo hadi asilimia 80 ya pato la kila mmoja! Nenda na kwenye meza sokoni somba mahela! Nunua mav8 ya ST piga nunua ndege binafsi.
Mbowe nenda kwenye ile ghorofa yako masaki, au pumzika kwenye hekalu la machame, au nenda kwenye 5star yako pale aishi au kule Dubai kwenye hotel na biashara zako! Kula maisha bro unajizeesha bure! Ndezi kama hizi hazitaruhusu wenzao wafaidi uhuru wa kiuchumi.
Na sisi watz hakuna kusaidiana wala chumvi au kibaba cha unga! Kila mtu afe lwake!! Rubbish!!
 
Jamaa wanaitafuna nchi vizuri sn

..hebu fikiria waziri wa fedha siku ya kusoma bajeti anasindikizwa na msafara wa ma-V8 na mapikipiki.

..wakati huohuo kuna vijiji havina zahanati, kuna shule hazina matundu ya choo.

..Na baadhi ya hivyo vijiji haviko mbali na hapo Mh Waziri anapofanyia mbwembwe zake.

..Ni bahati mbaya kwamba kuna baadhi yetu wenye uelewa kutokana na ushabiki wa Ccm, wanatetea mambo hayo.
 
Press nzima ya leo hakuna mahali ameongelea serikali kupunguza matumizi ya anasa
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kinachoendelea katika ajira ya Watumishi ni kukatwa kodi mara mbili.

Hizi hapa nukuu za Mbowe...

“Tunapowapa Watawala nafasi ya kuongoza maisha yetu na wanaamua bila kujali kinachotupata, hatupaswi kuwa waoga.

Kuna wakati nakwazika sana kwa kazi ninayofanya mnapokuwa waoga na hofu, halafu mnalalamika.

Hao wanaowatoza kodi hiyo wanakwenda kununua V8 ya Shilingi Milioni 450 au 500, mtu ambaye angekuwa nyumbani kwa mumewe au mkewe asingeweza kununua V8.

Lakini kwa kuwa kuna pesa ya Wajinga Watanzania wanaweza kununua gari la kumpa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Jaji kila mmoja.

Jiulizeni ni Wafanyabiashara wangapi ambao wana uwezo wa kuendesha magari mapya?

Magari mapya Nchi hii ni mali ya viongozi wa Serikali, na mnavyokaa kimya mambo haya ndiyo yanaendelea, mnatakiwa kuamka.

Kama mnataka kuibadilisa Nchi hii lazima tuache woga, lazima viongozi wa dini muongee.

Nilimwambia Rais Samia hii simulizi ya ‘amani’ ‘amani’ ‘amani’ ni kupoteza muda, simulizi sahihi ni haki haki haki.

Kuwepo na haki kwa watu wote litakuwa tafa bora la kuishi. Watanzania wameangalia uchaguzi wa Kenya kila mmoja ametamani, ulikuwa wa wazi hakuna mizengwe
Mbowe ni cheap leader, aliuza utu wake na chama chake ili awe huru, ni kiongozi mwoga sana hawezi kuongoza nchi kama kamanda mkuu, alienda Ikulu mara kadhaa bila ya ushauri wa chama chake lakini na alipotoka jela tu., namfananizia mbowe na kama Mrema au mzee Mtikila kwenye siasa hizi za Tanzania.
 
Ona hili zezeta hapa! Kuna uwongo ameongea! ?? Jamani watanzania waachwe wateseke hadi "walimie meno" JPM quote.
Mwigulu ongeza tozo hadi asilimia 80 ya pato la kila mmoja! Nenda na kwenye meza sokoni somba mahela! Nunua mav8 ya ST piga nunua ndege binafsi.
Mbowe nenda kwenye ile ghorofa yako masaki, au pumzika kwenye hekalu la machame, au nenda kwenye 5star yako pale aishi au kule Dubai kwenye hotel na biashara zako! Kula maisha bro unajizeesha bure! Ndezi kama hizi hazitaruhusu wenzao wafaidi uhuru wa kiuchumi.
Na sisi watz hakuna kusaidiana wala chumvi au kibaba cha unga! Kila mtu afe lwake!! Rubbish!!
Bila shaka wewe ni mkewe ndio maana umeguswa na kile kilichoandikwa hapa. Ngoja nikwambie mama, hapa ni JF na mumeo kazi yake ni siasa kwahiyo hutakiwi kuchukia pale anapoambiwa ukweli.
Kama kweli mumeo ana nia ya kutuongoza watanzania kwenye mapambano ya kudai haki, basi atangulie kwanza yeye, watoto pamoja na wewe mke wake katika maandamano hayo afu baadae na sisi tutafuata. Mumeo hawezi kutuambia kuwa sisi tuingie barabarani kupambana na jeshi la polisi wakati huo yeye akiwa ikulu kwa raisi kunywa juisi na familia yake, kisha akishatoka ikulu arudi nyumban akaangalie kwenye taarifa ya habari jinsi wadanganyika walivyovunjwa vunjwa miguu kutokana na maandamano hayo. Mwambie mumeo sio kila mtu ni kilaza kama anavyodhania.
Wengi walidanganyika miaka hiyo ya 2010 hadi 2015. Sio sasa.
 
Baadae atampigia mama simu amwambie asimuelewe vibaya, ameamua kujitokeza ili kuwazubaisha na kuwahadaa wadanganyika, baada ya malalamiko mengi juu ya ukimya wake.

Kalagha baho kwa wale wote wanaofikiri kuwa Mbowe alimaanisha. Siku Mungu akimchukua wengi mtashangaa mtaposikia wasifu wa cheo chake kweny kile kitengo cha "gizani".

Hata Mrema wengi walipinga juu ya utumishi wake pale kitengoni, tuliaminishwa kuwa ni kiongozi wa upinzani alienyima mzee Mwinyi usingizi mwaka 1994 to 1995.
Lkn juzi kila kitu kiliwekwa wazi baada ya kifo chake, alikuwa mtumishi alietukuka pale kitengoni. RIP Mrema umetuachia somo la kujitafakari upya kuhusu huu upinzani butu wa Tanzania.
Wanasiasa kuwaamini inataka moyo.
 
Back
Top Bottom