Mbowe: Utawala wa Magufuli uliwatesa sana watu wa Kilimanjaro na Arusha!

Mbowe: Utawala wa Magufuli uliwatesa sana watu wa Kilimanjaro na Arusha!

Wale ni matapeli walitapeliana wakataka Magufuli awalipe tena! Waende mahakamani kama wanayo haki mama Samia si yupo! Ila kwa vile hawana haki hutona mtu anapeleka miguu yake ya supoku mahakamani!
Sasa ndugu yangu Ile barabara ingepanuliwaje? You guys are so selfish, kwamba watanzania ni Bora tuwe na barabara ya sentimita mbili ili kuwanufaisha nyie?
 
Machadema na wachaga walifikiri wataendelea kutawala kila sekta kama ilivyokuwa zaman>!

Zama zimebadirika sasa yenyewe bado yanafikira za miaka ya 70 huko

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Yaani hadi wabunge viti maalumu wakienda mikoani cha kwanza ni kuangalia pana wa kilimanjaro mkoa huu? Akiwepo wanasema mpeni ubunge viti maalumu huyo ni mwenzetu
 
Hii kauli ya Kiongozi huyu amekuwa akiirudia rudia sana naona kama haina afya kwa taifa!
Inabidi asamehe asonge mbele maisha ndo yalivyo! Yeye anaona utawala wa Magufuli uliwatesa lakini kuna watu hawaoni hivo!
Inabidi aondokane na hizi chembechembe za ubaguzi yeye kwanza!
Hivi wewe Babako akivunjiwa Kitega uchumi chake kwa hila, akapigwa na kuvunjwa yeye mwenyewe kwa hila, wakaharibu shamba lenu na kung'oa mazao kwa hila, wakakamata na kuua watoto wenu kwa hila we utasemaje ? wewe utaongea kauli gani ?

Wakati huo wafanyaji hayo kwa amri ya utawala wa Magu akiwemo huyo SSH ndio hao kina Makonda leo hii wanalilia nankugombania mali za dhuluma mtaani, ndio hao kinasabaya wapo wanatumikia vifungo virefu gerezani, ndio hao kina Ally Hapi, wapo wanashangilia jengo la Dubai kuwaka taa za rangi ya bendera ya TZ huko Duniani

Niliwahi kusikia wakisema Mama kaupiga mwingi, ila sasa naona mama wamtereza and this time wamtereza kweli kweli kama Yesu alivyowaokoa walimwengu kwa damu yake iliyomwagika akafa kisha akafufuka Leo hii vitabu vinatuambia ndie Mungu wa Dunia na walimwengu

Kumbukeni damu ya Lissu iliyomwagika kwa kujaribu kuwaokoa watanzania akauawa kwa risasi 36 alizopigwa akapelekwa hospitali kisha akafufuka basi kesho vitabu vya historia ya TZ vitatuambia kuwa Lissu ndie Raisi wa Nchi na wananchi wote wa Tanzania

Mama anazidi kupwaya sio mtu wa haki kama anavyojinadi Mungu atamdhalilisha kama alivyo wadhalilisha watangulizi wake Amen!!!

Maisha yanenda kasi sana, leo hii Dictator Magu a.k.a Chuma. Kufumba na kufumbua Chuma kinaongelewa kama kumbukumbu iliyopita tu kama kumbukumbu zingine tu aliyo yalazimsha hayapo tena wala walio mtukuza hawana nguvu tena.

Duniani tunapita tu.
 
Makengeza kahamia kwenye ukanda na ukabila, Peter Zakaria aliyepigwa risasi Tarime alikuwa wa kilimanjaro au Arusha? Hili chama Cha wachaga shida sana
Unalalamika huku ukifanya yale yale unayoyalalamikia! Ungeweza kuwasilisha hoja yako bila 'kumnyanyapaa' Mbowe. Hakuna mtu (labda anayejitoa akili) asiyejua kuwa Magufuli alikuwa na roho mbaya sana dhidi ya watu wa Kilimanjaro na Arusha. Hilo lilitokana na sababu mbili kubwa miongoni mwa nyingine. Kwanza, ni asili ya watu wengi wa maeneo hayo kuunga mkono upinzani wakati yeye dhamira yake ilikuwa ni kufuta kabisa upinzani kama alivyojiapiza hadharani; na pili, aliwachukia watu wa maeneo hayo kutokana na uchakarikaji wao wa kutafuta fedha. Magufuli aliamini wachakarikaji ni wezi tu, na ukumbuke yeye alikuwa aina ya watu wanaopenda wapate wao tu!

Vitendo alivyofanyiwa Mbowe mwenyewe kwa amri za Magufuli au kwa watu kujipendekeza kwa Magufuli, ni watu wachache mno ambao wangeweza kukaa kimya wasiseme neno lolote. Mbowe alivunjiwavunjiwa shamba lake la maua, biashara zake zingine zilipigwa nati wazi wazi kibabe, na bado OCD wa Hai akishirikiana na Sabaya walitekeleza wazi wazi mkakati haramu wa kuhakikisha hatangazwi kuwa mbunge wa Hai, licha ya ukweli kwamba wana Hai walikuwa bado na imani naye zaidi kuliko yule pandikizi ambaye leo inaendelea kudhihirika kuwa hakuwa chaguo la wana Hai!

Umeleta hoja ya Zakaria wa Tarime kupigwa risasi. Niishie kusema tukio hilo haliwezi kumzuia Mbowe au mtu wa Kilimanjaro au Arusha kukumbuka madhila waliyokutana nayo awamu ya Tano. Na ninakualika ufafanue tukio la Zakaria ili tupime uelewa wako katika hilo, usije ukawa umejiandikia tu!
 
Ujinga uliopitiliza, Hayupo, ukatili wake unakusumbuaje? Nenda kalipie Tozo, baada ya hapo kumbuka cement imepanda 25k toka 17k
Mbona Nyerere anasemwa japo hayupo?...kuweka kumbukumbu za marais wetu si ujinga ila ni kujifunza kupitia mazuri na makosa yao.

Hayo ya tozo na mfumuko wa bei hayahalalishi kuzuia kujadili uongozi uliopita maana hili taifa bado lina miaka mingi ya kuwepo huo mfumuko wa bei na tozo hazitaishia awamu hii bado zitakuwepo tu.
 
Makengeza kahamia kwenye ukanda na ukabila, Peter Zakaria aliyepigwa risasi Tarime alikuwa wa kilimanjaro au Arusha? Hili chama Cha wachaga shida sana
Nakuongezea hapo, John Heche alivyosumbuliwa alikuwa wa Kilimanjaro ? Au Zitto ? Au Mathayo ? Aache ufala
 
Hapo umeoneshwa tu jinsi wachaga walivyosambaa ulimwenguni, hajasema yupi ana nafasi nzuri zaidi ya mwingine, mmetawaliwa na wivu na chuki ya kishamba sana.
Hivi kuwa kwenye jeshi la Marekani ndo kusambaa. Unadhani huyo mchaga pekee ndo yuko jeshini huko Marekani? Fikra hizi ni finyu. Kwa taarifa yako kuna watanzania wengi tu kutoka makabila tofauti wapo katika vyombo vya usalama vya Marekani na nchi tofauti, ila hawapendi shobo.
Pia fahamu nchi za nje kujiunga na jeshi ni rahisi sana. Wanatafuta watu kuingia jeshini, na huko nje unafanya kwa mkataba. Watu kutoka Mexico wengi wao ujiunga na jeshi la Marekani. Hizi ni kazi rahisi kupata.

Kuna mtoto wa Jaji mmoja hapa Tanzania kutoka katika kabila kubwa tu anafanya kazi na Nasa, lakini uwezi jua. Si yeye tu wapo kibao. Hivyo swala la kusambaa makabila mengi Tanzania yamesambaa ila hawana time ya kujisifia ujinga, na kujiona. Wao wanaona ni kawaida tu.
Tuache sifa za kijinga.
 
Yani wakija MWANZA lazima watafute ukumbi wa mchaga mwenzao wapumbavu sana!
Hata wahindi wana hii tabia. Na sisi makabila mengine tufanye sio kulalamika. Mtu katoka uchagani, kaja usukumani kafungua ukumbi, wageni toka uchagani wamekuja wanataka ukumbi unategemea wasimkumbuke mtoto wao wa uchagani?
 
..Na Magufuli chuki aliitoa wapi?

..Magufuli hakuwa kufungwa kwa dhuluma.

..Magufuli hakuharibiwa biashara na mali zake.

..Magufuli hakuwahi kuvunjwa mguu.

..Kwanini alikuwa na chuki na mbaguzi kiasi kile?

Maduka ya kubadilisha fedha ya Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro yalivamiwa na JWTZ,Police & BOT na kuporwa fedha.
 
Wamesama mtapata katiba mpya na kutakuwa na utawala wa majimbo wananchi mjipangie vipaumbele vyenu na kujiletea maendeleo wenyewe kwa haraka.
Tunataka Mbowe na CHADEMA watuambie watanzania watalifanyia nini taifa hili endapo watapata madaraka ya kuongoza nchi. Haya mengine ni utumbo kama utumbo!
 
Mbowe tumia mdomo vizuri kama una mpango wa kuwa kiongozi
Namna hii ni wazi ni jinsi gani utakavyokuwa mbaguzi kama kawaida yenu
 
Utawala uliwatesaje?

Kwamba Magufuli alikua anaua, anafunga na kuwapoteza watu wa Arusha na Kilimanjaro?

Kitu mbowe hana hua ni reasoning. Mbowe hutanguliza hisia kuliko uhalisia. Mbowe kuropoka lolote linalokuja kichwani mwake ni kawaida.

Magufuli aliwatesaje watu wa Kilimanjaro na Arusha?

Hii ni mara ya pili Mbowe anaendelea kusambaza chuki ya ukabila kwa wachaga wenzake.

Hata kama kweli(ingawa sio kweli) Magufuli alifanya hivyo, Magufuli alishakufa mwaka mmoja uliopita, yeye sasa ajikite kwenye kujenga chama, Magufuli hayupo tena.

Sasa yeye kila akisimama tu kwa wachaga wenzake anamzungumzia Magufuli, Magufuli, Magufuli.

Magufuli angekua anawatesa na kuwachukia watu wa Kilimanjaro na Arusha angempa mkuu wa Usalama wake kutoka Kilimanjaro?

Vyama vingine ni vya kitapeli tu.
Mwacheni aseme aliyoyapitia, iwe funzo kwa wengine pia, kwanini munampangia ya kusimulia?

Kama Magufuli alitenda haki kwenu elezeni namna alivyowatendea haki, na aliyeumizwa mwacheni asimulie namna alivyoumizwa, sio unahitimisha kwamba "hakutendewa vibaya" wakati yeye ndiye anajua kilichomtokea!

Kuna watu mpaka sasa utawasikia "LISSU HAKUPIGWA RISASI NA MAGUFULI" stupid kabisa, angekuwa amecharazwa risasi mama yake JPM ungeona kitu ingetokea, Magufuli alikuwa na roho mbaya sana kwa wapinzani wake wa kisiasa, aliwatendea yasiyo ya kibinadamu, aliwaua na kuwafilisi ili tu ubovu wake usisemwe, na asifiwe wakati wote!

Mnaomfurahia kwa sababu zenu ni sawa, na wanaosimulia maovu waliyofanyiwa na JPM pia ni sawa kabisa,kwani kwa yote kuna mafunzo muhimu sana ndani yake, SABAYA anaweza kuwa shuhuda mzuri sana wa yaliyotokea, akiamua kusema kweli!
 
Anamuinea wivu Hayati. Aiseee mkabila ulingoni
 
Nilijua tu wewe ni mtu wa sampuli gani kwa thinking capacity uliyonayo, na hii comment yako imenithibitishia hauna kitu kichwani ni kelele tu.
Wewe ulitaka ujibiwe nini kwenye upumbavu wako.
 
Back
Top Bottom