Akiwa club house amesema kwamba mara nyingi anaambiwa na vijana wake waingie barabarani kudai katiba mpya na yeye huwajibu hivi mnajuwa maana ya barabarani? Vijana hukaa kimya na kushupaza shingo zao wapo ambao tayari wameanza kusema kwa sasa anamegewa kiduchu keki ya taifa ndiyo maaana ameamua kukaa kimya wengine wanasema jela amejifunza mambo mengi sana hasa kutii mamlaka za nchi.
Hata hivyo yeye mwenyewe ameshawambia vijana wake waache kutukana vyama hasimu kwani kufanya hivo hawatopata ushawishi wowote ndani ya jamii.
Mbowe ameamua kutokuwa karai kila siku kubebeshwa zigo la katiba huku wengine wakitoa matamko kupitia vyombo vya habari na media kwa ujumla kaamua kukaa kimya maisha yaendelee.