Mbowe: Waliokimbia CHADEMA watarudi, tutawasamehe dhambi zao

Mbowe: Waliokimbia CHADEMA watarudi, tutawasamehe dhambi zao

Kusameheana ni Mhimu.

Kuna watu humu wanatampiga mbowe kana kwamba chama ni chao peke yao wakati chama ni cha watanzania wote. Hata SAMIA anaweza kujiunga na chadema. COVID 19 bado wanaumuhimu kwenye chama.
 
Walifukuzwa na Kamati Kuu, ila wakakata rufaa kwa Baraza Kuu kama katiba ya Chadema inavyotaka, na Baraza kuu ndio chombo chenye maamuzi ya mwisho.

Muhimu mtu akishaadhibiwa anaanza kuitumikia adhabu yake hapo hapo mpaka pale rufaa yao itakaposikilizwa, kama wakishinda ndio warudishiwe uanachama wao.

Kwa sasa wale sio wanachama tena wa Chadema na hawastahili kuwepo bungeni kwani wanavunja sheria za nchi, mbunge lazima awe member wa chama cha siasa.
sasa kwanini hamuwapeleki mahakamani ili mahakama itowe order ya kuwatoa bungeni? mmepewa mashart na spika mpeleke vielelezo ya vikao halali mpaka leo mnahangaika tu inamaana ni mtu tu kaamka na stress zake anataka watu watoke chamani?
 
Anatuandaa kuhusu walio kimbilia ccm na NCCR wakijua watapewa ubunge na watateuliwa na mwendazake sasa wamepewa kadi nyekundu. wamemuomba warudi kawaambia wasubiri kwanza ili atupe jiwe gizani asikie maoni ya wananchi kwenye mitandao kama hivi alivyoongea.
 
Kuna jamaa alipopata madaraka tu akaanza kutekeleza ilani ya CDM na kuiweka pembeni ya chama chake, kwa kuwa hakuilewa undani kwake basi akakwama vibaya na akaishia njiani..

CDM hutangulia na wengine wanafuata na ndiyo maana kauli ya sentesi moja tu toka Mwenyekiti wa CDM ya KUWASAMEHE wale wato waliokiasi chama basi itajadiliwa wiki nzima na wadau wote nchini.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe amesema Chama hicho kikisema kinajenga uadui wa kudumu na watu waliohama, watakuwa haitakii mema Nchi.

Amesema, "Tunatakiwa tuwapokee wote, waliokimbia watarudi tutawasamehe dhambi zao. Tutajenga CHADEMA kuwa Chama Kiongozi. Tusivae utakatifu, sisi sote ni binadamu, tuna mapungufu yetu."

Amefafanua, Chama hicho kinapigania Haki za Watanzania wa Vyama vyote hata CCM akisisitiza lengo ni kuwa na Taifa lenye mshikamano.
Mbowe anafaa kuwa kiongozi wa dunia
Ana hekima, busara nyingi sana.
Hakujawahi kuwa na kiongozi kama huyu
 
Anatuandaa kuhusu walio kimbilia ccm na NCCR wakijua watapewa ubunge na watateuliwa na mwendazake sasa wamepewa kadi nyekundu. wamemuomba warudi kawaambia wasubiri kwanza ili atupe jiwe gizani asikie maoni ya wananchi kwenye mitandao kama hivi alivyoongea.
wengi wameshaomba msamaha ki-chini chini warudi, maana CCM ya sasa haieleweki tena baada ya Mwendazake kuwaacha chaka....

..na kwa kuwa Mh. Mbowe ni mtu makini na mstaarabu si lazima aanze kuwaanika hadharani kwa mbwembwe kama ile style mwendazake !! Kuna jamaa alipigishwa magoti huku anarecordiwa - laaah
 
Mbowe bado anatakiwa kuulizwa kwanini zile rufaa walizokata wale 19 bado hazisikilizwi mpaka leo, shida iko wapi? akiendelea kukaa kimya wanaanza kuonekana matapeli.
Mnyika amefafanua mara nyingi. Katiba ya CHADEMA inaeleza ni wakati gani Baraza kuu hukutana. Halikurani kwaajili ya ajenda moja.
 
Sometime mbowe huwa simuelewagi ni mpinzani wa aina Gani?
Ndugu yangu,
Pamoja na unyanyasaji na ukatili wote ambao alifanyiwa na awamu ya tano, SIDHANI kama ulitamani kumwona Mbowe AKIELEKEA kuwa kama wale ambao walikubali na kulegea mpaka wakawa CCM B.
Hata hivyo kumsamehe mtu aliyetubu na kujirudi ni jambo jema kwa binadamu wote na mpaka kwa Mungu. Huo utakuwa ndio ukomavu wa kweli tunaotakiwa kuuishi. Kamwe haitakuwa busara kujenga na kulea chuki na visasi kama alivyokuwa Mwendazake.
Pamoja na maujinga na majungu yote waliofanya, sisi tunatakiwa kuwa mfano HAI na msingi wa kujenga jamii yenye upendo na sio ya kujivunia kukomoana, maadamu Mungu kesha tusaidia kwa kututoa kwenye njia chafu ya kishetani, tuliyokuwa tunapelekwa kwa kasi kubwa.
Ila la msingi ni kuwa hao wanaorudi, hawatatakiwa kuaminika kama ilivyokuwa mwanzo.
AMEN
 
Dr Slaa karibuuu....huyo mwamba hawatamwacha kamwe....
 
Back
Top Bottom