Hadi saivi unapiga tu maneno matupu badala ya kuweka hivyo vipengele vinavyoonesha tumepoteza our sovereignty. Sasa kati ya mimi na wewe nani anapaswa kutolewa lugha mbovu?
Mimi sio kilaza kama wewe eti niamini tu maneno matupu wanayosema watu bila uthibitisho na maelezo ya uhakika
Kwani wewe ni kiziwi? Mkataba ulisomwa pale bungeni pia. Hata kama pengine una shida na uwezo wa kusoma, ulishindwa hata kusikia?
Machache tu yaliyopo kwenye mkataba:
1. Serikali italazimika kuwapa DP eneo lolote la ardhi watakalolihitaji kwa shughuli za bandari.
2. Ukomo wa mkataba ni wakati shughuli zilizoridheshwa kwenye mkataba zitakapokoma. Maana yake hakuna ukomo.
3. Kuuvunja mkataba ni mpaka pande zote zikubaliane, na hakuna mahali imeelezwa mambo gani yakifanyika au yasipofanyika, mkataba utalazimika kuvunjwa.
4. Serikali itahakikisha mkataba hauathiriki hata kama sheria za nchi au serikali vitabadilika.
5. Serikali italazimika kutoa unafuu wa kodi kwa shughuli zinazofanywa na DP. Hii maana yake tubadilishe sheria zetu za kodi kwa sababu ya DP.
6. Hukumu ya disputes itafanyika na mahakama ya South Afrika kwa kutumia sheria za UK, wakati sheria zetu za nchi zinasema disputes zote zinazohusiana na rasilimali zetu zitaamliwa na mahakama za ndani kwa kutumia sheria za nchini mwetu. Kwa hiyo tutalazimika kubadilisha sheria hiyo kama wanavyotaka hawa waarabu. Hii ina maana sasa ni DP ndio wenye maamuzi juu ya sheria zetu ziwe namna gani ili zifuate matakwa yao DP. Huko ni kupoteza mamlaka ya nchi kama Taifa huru kwenye maamuzi yake.
7. Hakuna sehemu ambayo mkataba unatamka uwekezaji wa DP ni kiasi gani mpaka kufikia ku-dilute uwekezaji uliofanywa na Tanzania kuwa zero percent. Inawezekana vipi, bandari ambayo nchi imewekeza mabilioni ya pesa, halafu nchi iwe na umiliki wa zero percent? Huu si upumbavu wa hali ya juu na wa pekee?
Kanuni ya umiliki wa miradi, ili wewe uwe na 90% ni lazima uwekezaji wako uwe mara tisa zaidi ya uwekezaji wangu. Huwezi kutoka ulikotoka na upumbavu wako, mahali mimi nimewekeza trillioni 10, wewe unakuja na vibilioni 700, halafu unasema kwamba wewe utakuwa na umiliki wa 100%. Halafu mimi niseme ni sawa. Ndiyo maana tunasema bunge hilo lililoridhia limejaa mijitu mijinga, punguani wa akili na maarifa, iliyojaa uwendawazimu ambao haujawahi kuonekana mahali popote Duniani.