Born-town wanamcheka mwenzao anayeulizia Barabara Bunge hili. Kwa kumkumbusha biashara ya kujali wananchi ilishaisha kitambo! Aisee nawahurumia watakaoenda kupanga folen tena.
- Tunachokijua
- Katika ulingo wa siasa, mara nyingi wakati wa uchaguzi ikijumuisha kabla na baada, kunakuwa na ongezeko la taarifa zisizo sahihi zinazolenga kupotosha wananchi kuhusu wagombea wa kisiasa, sera zao, na hata utendaji wa serikali.
Wapotoshaji hutumia mbinu mbalimbali kugeuza uhalisia wa taarifa zikiwahusisha viongozi ama wanasiasa ambazo huenezwa kupitia mitandao ya kijamii, vyombo vya habari visivyoaminika, na hata midahalo ya hadhara, jambo ambalo linawafanya wananchi kushindwa kutofautisha ukweli upotoshaji.
Madai ya video kuwa ni ya 2025
Ipo video ambayo imechapishwa mtandaoni ikionesha mbunge akitaka kujua kutoka kwa serikali kwamba ni lini barabara ya Nyashimo, Ngasamo, Dutwa itaanza kujengwa kwa lami, wakati huo akifuatiwa na mbunge mwingine akionekana kujibu akisema kwa muda uliobaki si wa kuomba barabara bali kuaga kwani karibuni Rais atavunja bunge.
Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search ulibaini kuwa video hiyo si ya mwaka 2025.
Vilevile video imepotoshwa kwa kuunganisha vipande viwili ambavyo havihusiani kabisa kwani wabunge hao walizungumza katika nyakati tofauti.
Kipande cha kwanza kilichapishwa kwa mara ya kwanza mtandaoni na Global TV mnamo tarehe 23 Aprili, 2018 ambapo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Busegwa, Dkt Raphael Chegeni alikuwa akichangia hoja bungeni kuhusu wizara ya uchukuzi na mawasiliano inayosimamiwa na Profesa Makame Mbarawa.
Alimtaka Waziri Mbarawa kufafanua kwanini barabara ya Nyashimo, Ngasamo na Duto ambayo Rais Magufuli aliahidi kuwa itajengwa kwa kiwango cha Lami, mpaka wakati huo bado haikujengwa kwa kiwango cha lami? "Rais Aliahidi Lakini Mpaka Leo Sijaona" alisema Mbunge Chegeni
Aidha kipande cha pili cha video hiyo kilichapishwa mtandaoni kwa mara ya kwanza na Millard Ayo mnamo tarehe 4 Aprili 2020 ambapo aliyekuwa mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde sasa akiwa mbunge wa Mvumi ambapo aliwashauri wabunge walioona maji yakizidi unga kuaga bungeni akiwataja wabunge wa upinzani, kwani alidai ulibaki muda mfupi kuelekea kuvunjwa kwa bunge.
"Spika jambo zuri wangelifanya baadhi ya wabunge wa upinzani kama alivyofanya profesa. Ukiona maji mazito aga, jamani tumieni bunge hili kuaga kuweni wastaarabu, ivi saivi unaomba lami kweli, bunge hili unaomba lami? game imeisha hiyo hapa tunajadili uchaguzi kesho kutwa Rais anakuja anasema bunge limevunjwa wewe unaomba lami kilomita 70 taabani hapa. Nataka niwashauri tutumie haki ya kidemokrasia wakati mwingine kuaga ukiona maji yamezidi kama alivyosema mama mimi naomba niwashukuruni safari ijayo sitakuwepo" (Profesa Anna Tibaijuka anasimama kumpa taarifa mbunge Lusinde kwamba hakuaga kwa kuwa maji ni marefu bali ni kwa sababu alikuwa anang'atuka)
Rejea hapa video ya awali
View: https://youtu.be/ASM7jgM9v1I?si=X0lbHMAHeMLI3j_q&t=122
Video ya pili
View: https://youtu.be/6UIM6be00fA?si=9zenSf_kP6D54KQD&t=225