Mbunge Condester Michael atimuliwa Bungeni kwa kuvaa ovyo. Spika awaagiza askari wa bunge kuwazuia getini wavaa ovyo

Mbunge Condester Michael atimuliwa Bungeni kwa kuvaa ovyo. Spika awaagiza askari wa bunge kuwazuia getini wavaa ovyo

Yes huko SA wanazo haki za LGBT na kwingi duniani but nani aliyepewa haki ya kuhukumu wengine?kama wewe upo straight sio tatizo but why kuwe na tatizo la mtu ambaye sio straight?

Ni culture ndiyo inayotoa hukumu. Ndiyo maana kama umewahi kuishi western Europe ni mwiko kuwa na wake zaidi ya mmoja.
Tafakari, chukua hatua.
 
Kama hujapata kifungua kinywa hebu anza nacho kwanza maana km dishi limecheza!
Kila nchi ina utamaduni na mila zake amabzo inaamua kuufuata, usitake kukurupukia kila ukionacho kwenye luninga kutoka ughaibuni ukadhani kinatufaa.

Hilo vazi alilovaa lina shida gani? mbona ndio vazi linalovaliwa na wadada asilimia Zaidi ya 80% hapa mjini
 
Amri 10 za Mzee Panchi.

7. Ni marufuku kwa wanachuo wa kike kuvaa ‘vibanachoo’ au kujipulizia pafyumu .................

Bunge la Mzee Panchi!
 
Hii nchi ni ya kipuuzi sana, Tatizo la huyu dada ni nini? na bado kuna watu wanasapoti huu upuuzi uliofanywa.

Nguo aliyovaa sio ya heshima, na isitoshe bunge sio la wanawake tu bali wanaume pia. Itapendeza wastiri miili yao.

Kosa alilofanya spika ni kumtoa, angetulia kwanza mpaka mwisho wa meeting n the wamuonye na asirudie huo ujinga wa kuvalia watu minguo ya ajabu.
 
Hilo vazi mbona ni vazi la kawaida tu tatizo liko wapi? spika n mbunge wake wamefanya kituko cha aibu kwa kweli
 
Mbunge wa Momba Condester Michael Sichalwe ametolewa ndani ya ukumbi wa Bunge ili akabadilishe mavazi yake baada ya Mbunge wa Nyangw'ale Hussein Nassor Amar kuomba muongozo wa Spika kuwa kuna baadhi ya Wabunge wamevaa mavazi yasiyo na maadili...
Sijaona tatizo la mavazi haya.

Labda kama kuvaa suruali ni tatizo humo bungeni, basi ni hilo laweza kuwa sawa...
 
Hilo vazi mbona ni vazi la kawaida tu tatizo liko wapi? spika n mbunge wake wamefanya kituko cha aibu kwa kweli

Mkuu dos. Suruali imembana, na kiblauzi kifupi. Tatizo wanajisahau sana.

Kama ni mimi nisingemtoa wala nisingemruhusu kusimama/kuongea na minguo yake ya ajabu kadamnasi, ila onyo angelipata
 
Tukio la leo asubuhi , lalamiko la Mbunge wa Nyangw'ale Hussein Nassor Amar akilalamika ati Mbungwe mwenziwe Condester Minael Sichalwe kavaa visivyo, limeelezea zaidi mtoa hoja anafikiri nini huko Bungeni kuliko kile “waliomchagua” kuwawakilisha wanachokitaka toka kwake.

Tunaifahamu Dodoma, na jinsi watu wanakaa bila wake zao kwa muda mrefu, na tunafahamu imagination ile Mbunge kama huyu wa Nyang’wale anavyoweza kufadhaika kiakili pasipo na sababu.

BINTI YULE ALIVAA VIZURI KABISA.
1622574504644.png

Tena kwa heshima kabisa, sasa sijui huyu Hussein Nassor Amar alitaka avae baibui au?

Hata picha zinaonesha binti yuko sawa kabisa.

Mbunge wa Nyang’wale alipita ubunge kwa vigezo vipi haswa vya kutetea chama na maslahi ya nchi?
 
Mkuu dos. Suruali imembana, na kiblauzi kifupi. Tatizo wanajisahau sana.

Kama ni mimi nisingemtoa wala nisingemruhusu kusimama/kuongea na minguo yake ya ajabu kadamnasi, ila onyo angelipata

Mkuu acha element za udikteta, Maisha mnayafanya magumu sana
 
Tukio la leo asubuhi , lalamiko la Mbunge wa Nyangw'ale Hussein Nassor Amar akilalamika ati Mbungwe mwenziwe Condester Minael Sichalwe kavaa visivyo, limeelezea zaidi mtoa hoja anafikiri nini huko Bungeni kuliko kile “waliomchagua” kuwawakilisha wanachokitaka toka kwake.

Huo mkia wa njano alioutanguliza hapo mbele ukiwa umeshuka kwa "chini" ndio shida.🤣
 
Back
Top Bottom