Mbunge Jesca Msambatavangu: Wanafunzi wanatumia Boom Kubeti badala ya Kusoma. Serikali itafute utaratibu mpya wa kuwakopesha

Mbunge Jesca Msambatavangu: Wanafunzi wanatumia Boom Kubeti badala ya Kusoma. Serikali itafute utaratibu mpya wa kuwakopesha

Mtu mzima unataka umpangie matumizi ya hela ambayo at the end of the day atailipia yeye mwenyewe..?
What happened to common sense..?

Nilikuwa nakuheshimu kumbe mtu wa hovyo hivi
Mkuu - Hawapangiwi matumizi, lengo la kupewa Mkopo ni kwa ajili ya kusoma. Sio Biashara wala kubeti - kama wanataka pesa ya ku-beti - wakakope Benki (NMB, CRDB etc)....
 
Nahisi kuna agenda anatengenezewa mazingira, unless otherwise ilalamikiwe serikali kwa kuruhusu kubeti kiholela
 
Yaani mkopo wala sio grant..., alafu alaumiwe yule ambaye ni addicted na sio yule ambaye anafaidika kila huyu teja anaposhinda kwa kula 15% (Kwa taarifa yako huyo ni Serikali); Anatumia kodi zetu kukopesha wachache (na sio kutafuta vyanzo vya grants) na bado ananufaika na hii Kamari (kwa kuchukua kile kidogo iwapo huyu Zumbukuku atashinda)
 
Mkuu - Hawapangiwi matumizi, lengo la kupewa Mkopo ni kwa ajili ya kusoma. Sio Biashara wala kubeti - kama wanataka pesa ya ku-beti - wakakope Benki (NMB, CRDB etc)....
Mbona hao wabunge mikopo yao hawapangiwi wailipe waitumiaje
 
Unaandika ujinga gani, matumizi ya pesa za mtu tena mkopo uyo mbunge anawashwa washwa na nini
Hakuna Mkopo unaotopewa ukatumike hovyo bila kuleta Tija tarajiwa, Serikali inafanya investment na inatoa previlege sio Haki na elewa hilo.Hizo ni hela za walipa.kodi sio kwamba zimekosa Kwa kutumika
 
Hakuna Mkopo unaotopewa ukatumike hovyo bila kuleta Tija tarajiwa, Serikali inafanya investment na inatoa previlege sio Haki na elewa hilo.Hizo ni hela za walipa.kodi sio kwamba zimekosa Kwa kutumika
Kwa iyo mtu umkopeshe pesa na bado upo pale kumonitor matumizi yake ? Huu ni ukoloni, je wabunge izo posho wanalipwa sio pesa au kodi za wananchi? Na je wanazitendea haki , badala mbunge jikita kwenye mambo ya maana anaongelea wanafunzi kubet bom zao , si wafunge ayo makampuni ya kupeti, mbona serikali inachukua kodi kule kama sio biashara halali? Na kama ni halali unampagiaje mtu cha kufanya
 
Hapana watu wazima pale ,90% ni Vijana wadogo wako 19-23 age still they are young and foolish.

Mwisho hata watu wazima Huwa wanapangiwa ,sio Kila mtu mzima ana akili ya mtu mzima
Kwani wakisha kula au wakimaliza kubeti wanarudi kuomba tena?kama hawarudi kuomba tena achana nao watajua wenyewe .
 
M nashauri Serikali iongeze Riba ya mkopo mpaka 20% na makato yawe 20% ili huku mtaani tuheshimiane 😂
 
Mbona hao wabunge mikopo yao hawapangiwi wailipe waitumiaje
Si unaona; Kama Mbunge - akipewa Mkopo wa gari - huwa anakwenda kununua gari. Na wanafunzi wafanye hivyo pia - ama sivyo atawekwa Mzabuni wa kupika, Hostel zipo tayari - kisha mwanafunzi hatopewa pesa ya chakula - na hostel - zote zitalipwa chuoni moja kwa moja. Itabidi mka-beti kwa pesa ya Stationery na nauli tu.
 
Lakini si kuna watu wapo mtaani mshahara wao ni laki nne na wanabet, wanakunywa pombe na bata sana?
Mi naona mi naona serikali itimize wajibu wa kuwakopesha matumizi iwaachie wao maana mwisho wa siku ile ni pesa ambayo watatakiwa kuilipa!
Tanzania sio nchi pekee inayotoa mkopo kwa wanafunzi, alafu wabunge vipo vitu vya kuzungumzia bunge vipi wapoteze mda wao talking about trivial things like this?
Mwambie ukweli huyu pimbi hajielewi kabisa! Mbunge hovyo sana huyu!
 
Hapa shida ni elimu ya matumizi sahihi ya fedha. Watoto wafundishwe personal finance toka wakiwa wadogo, jinsi ya kusimamia hela zake binafsi wawe na uelewa.

Sasa mtu anatoka huko bush hajawahi kushika hata laki ya kwawe mwenyewe, anafika chuo mnamrundikia laki 6 ama 7 ghafla kwenye akaunti lazima achanganyikiwe.

Tuwafundishe matumizi sahihi ya fedha, hawatatumia kubeti watafanyia shughuli nyingine za manufaa zaidi.
Mtu mkataba anasaini mwenyewe, anakatwa about 9% kwenye mshahara akipata kazi, anatozwa faini ya 10% kila mwaka akichelewa kurudisha, alafu bado unataka umpangie matumizi utafkiri hela umempa tu akatumie?? Hivi mnakuwaga na matatizo gani aseeee 😂😂?
 
Mtu mzima unataka umpangie matumizi ya hela ambayo at the end of the day atailipia yeye mwenyewe..?
What happened to common sense..?

Nilikuwa nakuheshimu kumbe mtu wa hovyo hivi
Hii nchi inaujinga ujinga mwingi sana, yani mtu anakukopa hela halafu unampangia matumizi😂
 
Waacheni nao watumbue - huyo mbuge analipwa ma.million ya shilling kwa wiki kwa kazi gani hasa anayoifanya humo.
 
Back
Top Bottom