Mbunge: Kwanini mwananchi akileta TV Bara kutoka Zanzibar analipia kodi wakati nchi ni moja?

Mbunge: Kwanini mwananchi akileta TV Bara kutoka Zanzibar analipia kodi wakati nchi ni moja?

Zanzibar VAT ni 15% wakati bara VAT ni 18% .... ukileta kitu bara hiyo 3% ndo inakatwa ili kuweka uwiano sawaaa uwe umelipa 18% kama bidhaa nyingine
Kwa nini usilipie 18% huko huko Zenji ili ukifika bara unakuwa ushamaliza kila kitu vinginevyo bara Wana tamaa na hakuna muungano wa kulipa kodi mara 2 kwenye nchi moja.
 
Unanunua bidhaa kutoka nchi nyingine kwanini usilipe Kodi? Wala hawakosei kukutwanga Kodi, Zanzibar Kuna raisi pale, hivyo Ile ni nchi.. ukileta bidhaa huku bara, tayari unakuwa umeingiza kwenye nchi nyingine ambayo ni Tanzania, maana huku nako Kuna raisi....
Basi huo ni muungano bandia,
Sijui bwana Teacher na Maalim walikusudia nini kuungana kama hakuna uafadhali wa mambo kama haya kwa raia wa pande zote mbili,maana kuna malalamiko wabara hawaruhusiwi kumiliki ardhi visiwani....sasa iko wapi faida ya Muungano ama lengo kuu la huo muungano ni nini?
 
kama nchi ni moja, kwanini kule kuna rais (sio Rais), pia watu wa bara hawaruhusiwi kununua/kumiliki ardhi kule wakati wao wanamiliki ardhi kwetu, kwanini wana chuki sana na wabara wakati wao ndio wanafaidika zaidi kuliko sisi wabara? au wanadeka?
Muungano uvunje sasa,kila mtu abaki na chake......lakini mbona kama bara ndio wanautaka sana Huu muungano kuliko watu wa Visiwani.
 
A

Acha kupotosha watu wewe,hata kama unaenda zanzibar kama una kitu ambacho kinaonekana labda umekinunua lazima ukilipie tu,itategemea na ukubwa wake,au wingi wake.HlMimi siku moja nimebeba cramping tool moja,na ninaenda kufanyia kazi huko,na nina vifaa vingine,ambavyo nilikuwa na barua ya TRA,havikuwa na shida,hii moja nilikuwa nimeibeba mkononi tu,nimefika unguja ZRA wakanikomalia ikawa inshu kubwa,wakati kwenye delivery note imo ila TRA,walisahau kuiandika!!Hadi boss wao ndio alikuja kuli solve!!,nimetoka unguja kwenda pemba nako wakakomaa!!lakini badaye wakaelewa!!!Inshu ikaja tena kwenye vifaa vilivyobakia baada ya kumaliza kazi kuvirudisha tena Dar,ikawa inshu,ila vilifika.Tuwe wakweli usumbufu ni mkubwa sana.Huo muungano unafaida kisiasa tu,lakini kiuchumi hapana.
Cramping tool, ni kama plaiz?
Ndio hadi ulipie?
Kumbe ni shida.
 
Kuna haja ya kutokuwa na Muungano kwa hali hii.
Ni maridhiano tu, tena waweke tangazo kabisa HAKUNA KULIPA
Watu wanaibiwa tu ila sio kisheria
Utalipiaje TV moja

Yaani kila leo ni chokochoko zisizoisha
Bora wagawane fito tu
 
Hao ndio wanasiasa wetu, Muungano ume devolve maswala ya kodi.

Ukishafanya maamuzi hayo bidhaa kutoka Zanzibar hasa zile ambazo awatengenezi wazanzibari ukileta bara ni importation.

Na kwa mujibu wa sheria za bara imported goods zina kodi zake itoke Zanzibar au Ulaya.

Angepitia kwanza hiyo sheria ya tax devolution au regulations zilizopo na kukosoa vipengele tata; common sense unataka kuona some goods imported for personal use vyenye thamani ndogo havina kodi. Lakini uwezi kubeba TV yako uilete bara au gari kiholela tu lipa kodi kama wengine.

Unabaki unajiuliza hata hizo degree za siasa au vitabu vya siasa vina cover topic gani, kama wabunge hawajui tu implications za devolution matters; sasa hao wananchi wakawaida si ndio balaa.
 
Kwa nini usilipie 18% huko huko Zenji ili ukifika bara unakuwa ushamaliza kila kitu vinginevyo bara Wana tamaa na hakuna muungano wa kulipa kodi mara 2 kwenye nchi moja.
Kodi haipo miongoni mwa mambo ys muungano
 
Wakisema waache kutoza Kodi Italeta mianya ya ukwepaji Kodi , kwamba hata wamalawi watapitisha mizigo Zanzibar wakisingizia umetoka Zanzibar kumbe la
Kwani uraia wa hao watu wanaopitisha mizigo haufahamiki?
 
Kero ni Mzanzibari, kisiwa chenye idadi ya watu milioni 1, kuongoza Bara kwenye watu millioni 60. Tuanzie hapo kwanza.
Zanzibar, kama tutatumia akili timamu ni mkoa sawa na mikoa mingine kama kweli tumeungana na siyo longolongo na siasia za wanasiasa
 
MiMI SIUPENDI HUU MUUNGANO

KILA SIKU NAOMBEA AJITOKEZE MTU AUVUNJE NA NAAMINI SOON MAOMBI YANGU YATAJIBIWA
 
Wewe hujui muungano unawanufaisha wanasiasa na wazanzibar,huku Tanganyika tuendelee kutawaliwa tu.
 
Wakisema waache kutoza Kodi Italeta mianya ya ukwepaji Kodi , kwamba hata wamalawi watapitisha mizigo Zanzibar wakisingizia umetoka Zanzibar kumbe la
Nadhani Kuna vitu hujaelewa, mtu anakwepaje Kodi ili hali huo mzigo umeingia Zanzibar na ZRB wametoza Kodi? Mtu anapaswa kulipia ushuru wa matumizi ya bandari na si Kodi. Kwani huyo mmalawi hawezi kununua kitu Morogoro,Dar au Mbeya?
Kama umewahi kununua kitu Zanzibar kwenda bara unaweza kumwelewa pindi unapofika bandarini, ila kama unaenda na upepo tu huwezi kumwelewa huyo mbunge
 
Muungano uvunje sasa,kila mtu abaki na chake......lakini mbona kama bara ndio wanautaka sana Huu muungano kuliko watu wa Visiwani.
viongozi ndio wanautaka ndugu. ila ukweli wakiweka referendum leo hii, utashangaa wazanzibar ndio wanataka kwasababu hakuna mbara anayeukubali ambaye hafaidiki nao.
 
Back
Top Bottom