Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Mbunge unakosa hoja ya kulisemea taifa lako unaongelea upuuzi?!
Kwamba changamoto lukuki zinazowakabili wana-Rukwa huyo mpuuzi kaiona ya viuno vya wanaume kuumia viuno ndiyo agenda kuu?!
Nimetukana!
===========================
MBUNGE BUPE: MATUTA YANAHARIBU VIUNO VYA WANAUME
Mbunge wa Viti Maalum (Rukwa), Bupe Mwakang’ata ameyasema haya Bungeni leo Jumatatu Aprili 11, 2022:
“Wanaume wa Mko wa Rukwa wanapata shida, nyumba nyingi zinavunjika chanzo ni matuta makubwa sana.
"Hayati Magufuli alipokuja aliona na akamwambia Waziri wa Uchukuzi wa wakati ule kuwa anampa mwezi mmoja yatoke, hayakutolewa, Katibu wa CCM alipokuja katika ziara Mkoani Rukwa alipata tabu sana hakulala siku hiyo, akaiambia Serikali iyatoe lakini mpaka leo kimya.
“Tunaomba Serikali ifanyie kazi suala hili matuta yaweze kuondolewa."