Mbunge Mstaafu na Mtu Maarufu anahitaji Mchango wa matibabu, wewe unadhani uta survive vipi?

Kumbuka mwenye nacho ataongezewa na asiye kuwa nacho hata kile kidogo atanyanga'anywa, akifariki mtu maarufu kila mtu atajua hadi wengine wanaitwa hayati, mvimba macho akifa ni ndugu zako tu na utaitwa marehemu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Laiti wengi munge jua maisha ya hao watu mnao fikili kwamba ni matajiri wengi musinge jibeza.......imagine mtu ana nyumba tatu lakini zote hati zimeshikiliwa na benki, na kuna arrears za madeni kibao, hamna mtu anae mpa chochote kwa sabb wote wanajua anazo....mimi sitamani hayo maisha kabisa, ni kweli hana, sio masihara
 
Hizi bima zimekaa kiwiziwizi tu, mimi nadhani kila mtu angekuwa na akaunti yake ya bima ambako fedha anayokatwa iingizwe huko na the only way anaweza kuitumia ni kwenye matibabu tu, kwa maana ya kwamba mtu anaweza ku accumulate fedha ikamfaa siku akiwa na uhitaji wa matibabu ya gharama ya juu kabisa kuliko hii ya kupimiwa kiwango cha tiba wakati fedha ni yako mwenyewe
 
Kutoa ni moyo sio utajiri.. kama tu mwana jf mmoja akiomba msaada hunyimwa na kuambiwa tapeli mfano mzuri yule tulie mpoteza Mpauko mnataka masikini gani sasa wasaidiwe ? Kama tu masikini wenyewe hawasaidiwi hata wale ambao tupo nao,Tuache unafiki saidien bila kuangalia,, mwingine ni unafiki na upumbavu na ww ulie leta mada bila shaka unakaujinga fulani hivi kakipuuz
 
kabisa, wengi wanapoteza maisha kwakua tu hana 20k ya matibabu, hao ndiyo wakusaidiwa kwa hali na mali na wapo wengi kweli, nenda MOI Muhimbili pale au vitengo vingine
Mlienda kuwasaidia hao wanyonge mkanyimwa na badala yake mkaambiwa mchangieni Pro J kwanza? Na hao waliokosa hiyo 20k walikatazwa kuomba msaada? Kuomba msaada na kutoa msaada ni maamuzi ya mtu. Kama prof J ugonjwa wake unahitaji matibabu ya gharama kubwa ana haki ya kuomba. Na hao wanyonge walioko Moi nao wana haki ya kuomba.
 
Mawazo yako ni mfu, nani aliyekuambia tajiri achangiwi panapo matatizo?, ingekuwa hivyo matajiri wangejizika wao na familia yao.

Hayo ni mawazo ya kimasikini, kama unacho na imekugusa changia, kama huna pita pembeni !
 
Mkuu unayakumbuka yale matibabu ya mstaafu ndugai
Wewe umesema. Huyu analalamikia mbunge aliyestaafu anasahau speaker aliyetumia mamilioni wakati yupo kazini na marupurupu kibao.
Inategemea na aina ya ugonjwa nagharama zake.
Komeo la chuma kama una hela mchangie na kama huna usiwakatishe tamaa wenye moyo wa kutoa
 
Mkuu dunia hailingani.

Usipotumia AKILI dunia hi, utajikuta unatumika mpaka mwisho wa Maisha yako.

Hivi hujawahi kusikia msemo kuwa, wewe ukiwa huna gari unaombewa upate ila Kiongozi wako wa kidini akitaka gari ANACHANGIWA😀

Imagine,

Mwanasiasa anahitaji Support yako:

Utatunga nyimbo utamwimbia sana, na kumsindikiza akachukue fomu ya kugombea.

Utaondoka nyumbani kwako, utaenda kwenye mikutano yake ya kampeni kumpa support.

Siku ya KURA utasimama JUANI siku nzima kumpigia kura.

Ukishampigia kura inabidi usubirie kituoni kulinda kura ili asiibiwe.

Akiibiwa inabidi uandamane upigwe mpaka atangazwe kuwa yet ndio mshindi.

Pamoja na kulipwa mabilioni, akiugua Ni lazima achangiwe.

Watanzania Ni WAKARIMU sana, na Kuna watu weshajua hili na wananufauka nalo kill siku.

Hasa Wanasiasa na Wasanii.
 
Komeo la chumaa ni aina ya mtu mpumbavu, asiyejua nini anachotakiwa kuwajibika kwa jamii yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…