MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Inasikitisha sana kuona mbunge wa bunge la JMT akiibeza elimu kwa kudhani kuwa na pesa ni mbadala wa elimu. Hizi kauli za mtu kama Kasheku zinafifisha kabisa malengo ya watanzania kujikomboa kupitia elimu. Kasheku na baadhi ya watu hudhani kuwa na hela nyingi ndo tayari unakuwa umepata mbadala wa elimu kitu ambacho sio kabisa. Kasheku hajui kwamba serikali inaweza kununua vifaa tiba vya kila aina ila bila wataalamu wa kuvitumia vikaishia kukaa stoo?
Taifa haliwezi kuendelea kwa kudhani hawa matajiri uchwara wa biashara za uchuuzi wa bidhaa za China ndo wataleta maendeleo. Maendeleo ya kweli yataletwa kwa kuzalisha na kuuza zaidi nje bidhaa na huduma. Hilo haliwezi kufanikiwa kama hatutakuwa na wataalamu wetu wa kufanikisha hayo.
Mbunge Kasheku anapaswa kupuuzwa na kushauriwa kurudi shule. Kuwabeza wasomi ni laana kwa taifa.