Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. DR. RITTA KABATI AWAPA SOMO WANAFUNZI CHUO KIKUU, AELEZA NAMNA RAIS SAMIA ANAVYOWAJALI
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, (CCM) Mhe. Dkt. Ritta E. Kabati @dr.rittakabati amewataka wanafunzi wa Vyuo Vikuu kujikita katika masomo yao wawapo vyuoni na kuacha mambo ambayo yatapelekea kusitishwa masomo yao.
Mhe. Kabati ameaema hayo wakati wa ibada maalum ya kuwaombea wanafunzi wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa wanaojiandaa na mitihani yao ya kufunga muhula iliyofanyika katika kanisa la KKKT Mkwawa, dayosisi ya Iringa.
Amewataka wanafunzi hao kuwa na hofu ya Mungu ili kupata wasomi wenye maadili katika kazi zao na pia kulisaidia Taifa kupata maendeleo .
Aidha, Mhe. Kabati ameeleza kuguswa na jitihada za Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Elimu nchini na zaidi kwa uamuzi wake wa kuongeza pesa za kujikimu kwa wanafunzi wa Chuo kikuu nchini.
Amesema kuongezwa kwa fedha hiyo ya kujikimu kutawasaidia wanafunzi hao kuzingatia masomo na kupunguza utegemezi kwa wazazi.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wengine, Atupasye Lazaro amesema anamshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza fedha hiyo ya kujikimu kwa kuwa itapunguza ugumu wa maisha kwa wanafunzi wengi.
Ameongeza kuwa fedha hiyo itasaidia wanafunzi kusoma kwa bidii na hata wengi kumaliza masomo yao tofauti na awali ambapo wapo walioweza kukatisha masomo kutokana na ukosefu wa fedha.
Atupasye amempongeza Rais Samia kwa jitihada zake anazofanya kuboresha sekta ya elimu nchini.