Mbunge Shabiby: Hata wewe Spika ukileta siasa zako tunaweza kukuazimia

Mbunge Shabiby: Hata wewe Spika ukileta siasa zako tunaweza kukuazimia

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mbunge wa Gairo amesema Viongozi wa Serikal Wana mtindo wa kuajiri walimu na kuwapangia vijijini kisha wanatuma vimemo wahamishiwe Mjini

Shabiby amesema Utaratibu Huu siyo mzuri na ikibidi watatoa Azimio Waziri na Watendaji wake waindolewe na kama Spika ataleta Siasa zake naye Atakaa pembeni

Spika sisi ndio tumemchagua hivyo ni lazima twende Sawa, amesema Shabiby

Chanzo: East Africa tv

Walewale. CCM ni wamoja.

Zamani vimemo vilihusu kupangiwa Dar, Arusha, Tanga , Mwanza na Mbeya mjini, ila sasa hivi vimemo vinahusu kuomba fulani asiachwe kwenye hizo nafasi.

Huna mbuyu hata huko kijijini hupangiwi utaendelea kupiga tempo za laki na kumi mpaka ufe
 
Nepotism ni tatizo kubwa sana hapa nchini.

Kijana kama Huna connection elimu Yako inaweza kuwa mzigo wa majuto.
Bora watanzania wengi au hata wote walifahamu hili,itawasaidia sanaa
 
Nepotism ni tatizo kubwa sana hapa nchini.

Kijana kama Huna connection elimu Yako inaweza kuwa mzigo wa majuto.
Connection ni nyenzo muhimu sanaaa 😔

Hustle na mateso niliyo pitia kitaa hapo hapo Nika andika sikati tamaa by Darasa CMB

Huo wimbo hapo juu na uwe faraja Kwa vijana wote TZ ambao wana pambana kuzitengeneza kesho zao zilizo Bora 🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Wasalaam
Kwa Sasa
+267
 
Nepotism ni tatizo kubwa sana hapa nchini.

Kijana kama Huna connection elimu Yako inaweza kuwa mzigo wa majuto.
Tume ya Ajira wakitangaza nafasi za kazi mwanzoni wanaendesha usaili wa mchujo na matokeo wanatangaza kila aliyefanya matihani aaona maksi zake. Kimbembe kinakuja wale wanaoendelea na usaili wa mahojiano matokeo yake maksi haziwekwi hadharani ili kila mmoja ajue maksi alizopata ili alinganishe na namna alivyojibu maswali. Hapa ndipo watu wanapitishwa kwa kujuana.

Hi limefanywa makusudi kwa sababu mtu anapojibu maswali anaelewa kabisa atapata maksi kati ya range fulani, hivyo maksi zikiwekwa hadharani Tume itaumbuka.

Wabunge wadai maksi za kila mmoja za matokeo ya usaili wa mchujo yawekwe hadhatani sio kutoa majina tu ya waliofaulu pekee. Tuna uhakika gani hao ndio waliofaulu.

Tume ya Ajira iache kutapeli waombaji kazi.
 
Ingaawa yeye mwenyewe alipita bila kupingwa lakini Hoja zake zina aksi uwezo wake wa economic liberation. Kwamba hamwogopi mtu kwa kuwa hamlishi.

Mbunge wa Gairo Mohamed Shabiby akitoa hooja zake na malalamiko juu ya Tamisemi kutoa ajira kwa kujuana, upendeleo kwa mawaziri amesema wao Kama bunge wana wajibu wa kuisimamia serikali.

Amedai ikiwa kuna mtumishi anaenda kinyume na utaratibu basi wanaweza kupeleka hoja Bungeni na kuazimia kumkataa.

Hata Spika akileta siasa zake wanaweza kumwazimia.

Je ni siasa zipi anazohisi zinaweza kuazimiwa?

Sikiliza mwenyewe kweny Clip hii.

Ukiwa na pesa huwa huogopi mtu.
Hizi ni fikra za kizamani sana. Nani kakwambia huwezi kuwa na msimamo bila ya kuwa na fedha?? Watanzania wengi wamekuwa dhaifu kimisimamo kwa kuwa na fikra kama hizi kwamba ili uwe huru ni lazima uwe na fedha.

Huyo Shabiby inawezekana katoa maneno hayo kutokana na mtizamo wake binafsi na wala si kwa hela alizonazo.
 
Unataka kupigana na kisiki.

Hakuna mbunge wa magumashi anaweza hoja hizo.

Ndio maana woote ni watu wa NDIYOooo!!!
 
Back
Top Bottom