Niliacha kila kitu.. nilikuwa naidai kampuni milioni kadhaa nilizisamehe. Nilianza kupanga chumba cha 25000/= kwa mwezi. Katika maisha yangu ule ndo uamuzi wa kishujaa zaidi niliowahi fanya kwa sababu baada ya huo uamuzi nilikaa miaka miwili ya kupigika haswa. Ilinijengea heshima mimi binafsi hadi familia yangu. SIMAMA KWENYE HAKI hutaonewa wala kumsujudia mtu.