Duh! Ndugu kwa huu mtazamo wako basi tutazidi kupigwa sana na wanasiasa. Na vijana wakifuata huu mtazamo wataishia tu kuolewa na wanaume wenzao wenye hela. Binafsi kama miaka 11 iliyopita niliacha kazi ndani ya masaa 24 baada ya boss wangu kunipa kauli mbaya sana iliyomhusisha mzazi wangu. Hiyo kazi nilikuwa nalipwa Tsh 1.2m kwa mwezi, nyumba bure self contained yenye maji na umeme. Nikaenda kuanza upya kabisa nikawa mjasiriamali... baada ya miaka kadhaa nikawa napata pesa nyingi kuliko ule mshahara. Yule boss tunaheshimiana sana kwa sasa na nilisamehe baada ya yeye kukiri alikosea miaka ile. PLEASE JIAMINI.