Tetesi: Mbunge Shangazi ana ubia na Kampuni ya DP World

Tetesi: Mbunge Shangazi ana ubia na Kampuni ya DP World

Mie siandamani bali nitapiga goti kumuomba Jehova ashughurike na hao wezi, imani yangu inao uwezo wa kuhamisha milima.
Kila la heri mtumishi. Utaomba maombi ya aina gani? Ya visasi na kupatilishwa ili mafisadi wote wafe? Mungu Aingilie ugomvi?

Uzuri/"Ubaya" wa Mungu ni kwamba Yeye huwa hapangiwi ratiba ya kujibu maombi yako. Anaweza akajibu leo, kesho au baada ya miaka elfu moja...au anaweza asijibu kabisa!

Hitimisho: Njia yako ya kuikomboa nchi yako ni ya kinjozi zaidi. Nakushauri uingie kwenye maandamano yatakayoitishwa na Mbowe!
 
Hitimisho: Njia yako ya kuikomboa nchi yako ni ya kinjozi zaidi. Nakushauri uingie kwenye maandamano yatakayoitishwa na Mbowe!
Maandamano sio solution, kumbuka vita hii sio ya kimwili, na hao wapiga dili walianzia kwa waganga wa kienyeji so hii ni vita ya kiroho.

Mafisadi na majini yao ya kuwaletea hela za dhurma, makahaba wao na rasrimali zao zote lazima vitoweke kwa njia ya maombi.

Tunapambana na nguvu za giza mkuu, huyo Mbowe ni tapeli hana jipya ktk mapambano huu aandamane peke yake na matapeli wenzie.
 
Maandamano sio solution, kumbuka vita hii sio ya kimwili, na hao wapiga dili walianzia kwa waganga wa kienyeji so hii ni vita ya kiroho.

Mafisadi na majini yao ya kuwaletea hela za dhurma, makahaba wao na rasrimali zao zote lazima vitoweke kwa njia ya maombi.

Tunapambana na nguvu za giza mkuu, huyo Mbowe ni tapeli hana jipya ktk mapambano huu aandamane peke yake na matapeli wenzie.
Sasa nimekuelewa Mtumishi.

Sina hata swali la kuuliza.

Vita ni vita mura!
 

Attachments

  • 85C3CC1B-3220-4478-9C1E-169BA77BEB3C.jpeg
    85C3CC1B-3220-4478-9C1E-169BA77BEB3C.jpeg
    45.3 KB · Views: 1
Simtetei lakini mkataba ulisainiwa Oktoba mwamba Kauliza novemba ila je mbona wengine tulichelewa kusanuka shangazi asulubiweeeeeeee
 
Kwani TAKURURU wao siyo zao la mfumo huu huu wa kifisadi? Kwani wao wameshushwa kutoka Sweden, Finland au Denmark? Si ajabu ndo walitoa assurance kwa watia sahihi kuwa hakuna kitakachoharibika!
Utakuta hata hiyo kazi ya TAKUKURU alipata kwa Rushwa.
 
MBUNGE, Rashid Shangazi anatajwa kuwa ndiye Dalali wa Kampuni ya DP World inayotaka kuuziwa bandari zote Tanzania isipokuwa za Zanzibar tu, Shangazi alianza kuipigia debe na baadaye kuwaleta nchini na kukamilisha hiyo dili ambalo limezua mgogoro mkubwa Tanzania.

Ushahidi wa ni SWALI NA 58 LA TAREHE 4 NOVEMBA, 2022 ambapo kwa mujibu wa Tovuti ya Bunge, Mbunge huyo aliuliza

"58. MHESHIMIWA RASHID ABDALLAH SHANGAZI (MLALO) :Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi: Je, ni lini utekelezaji wa Mkataba wa Kibiashara kati ya Serikali na Kampuni ya Dubai World utaanza"
Serikali kupitia Naibu Waziri wa Ujenzi( ATUPELE MWAKIBETE ALIJIBU NAKUU)

United Republic of Tanzania


Primary Questions
MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: -

Je, ni lini utekelezaji wa Mkataba wa kibiashara kati ya Serikali na Kampuni ya Dubai World utaanza?

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Mlalo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2022 Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ilisaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Kampuni ya Dubai Port World (DP-World) ya Umoja wa Falme za Kiarabu, kuhusu uwekezaji katika maeneo ya bandari nchini. Aidha, tarehe 25 Oktoba, 2022 Serikali ilisaini makubaliano na Serikali ya Dubai (Inter-Governmental Agreement - IGA).

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mkataba wa kibiashara unakwenda katika hatua mbalimbali. Hatua ya kwanza ni mkataba kati ya nchi na nchi (Intergovernmental Agreement - IGA) ambao tayari umesainiwa. Mkataba huo unaweka msingi wa Serikali za pande mbili kuanza majadiliano kuhusu maeneo ya uwekezaji.

Baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, majadiliano yataendelea kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kuhakikisha kwamba uwekezaji huo unakuwa na tija kwa nchi. Matarajio ya Serikali ni kuwa majadiliano hayo yatafikia tamati mwishoni mwa mwezi Desemba, 2022.

Mwisho wa Kunukuu.

Hivyo basi Watanzania tusimtafute mchawi wa suala hili kwani aliyeileta kampuni hii na kuipenyeza serikalini ni Mhe. Shangazi ambaye ni Katibu wa Wabunge wa CCM ambaye ametumia ushawishi wake alionao ndani ya Chama na Serikali kuileta kampuni hii na kumchafua Rais wetu Samia Suluhu Hassan.

Mbunge Shangazi ni Mbunge wa Mkoa wa Tanga amepigia debe ili bandari zote ziuzwe kwa kampuni hiyo ambayo inasemekana yeye wadau wake wamepewa donge nono kuhakikisha kampuni hiyo inanunua bandari zote na kuendesha kwa miaka isiyojulikana.

View attachment 2649962
Rashid Shangazi- Mbunge wa Mlalo
Shangazi kaja na begi la Shangazi
 
Wakati huo huo Gwajima naye anaomba waendelee kulamba asili vzr bila bughuza

Hii itakuwa kama lile tukio la Nabii Eliya na manabii wa baal. Gwajima na genge lake kama atakuwa na msimamo huu wa kutetea kulamba asali atalambwa yeye na Moto Ulao wa Mungu wa Mbinguni.
 
Mwisho wa siku yakimshinda mwenzio atakimbilia kwao Oman wewe utarudi kwenu Maneromango hohe hae... kuwa na akili hata kidogo basi we ajuza.
 
Back
Top Bottom