Mbunge Tarimba apendekeza TANESCO kufumuliwa na kuwepo kampuni 3 kwa ajili ya Uzalishaji, Usafirishaji na Ugawaji umeme

Wakikaa kimya; HAKUNA WANAFOFANYA ZAIDI YA KUPIGA MAKOFI!!

wakiongea na kutoa michango; MAFISADI HAO, WEZI, WAMETUMWA!!

wakati mwingine nachukia kweli kuwa raia wa nchi moja na hii mijitu isiyojuelewa iliyojaa fitna, wivu, uzushi na majungu!
 
Mimi niulize swali, ni nani anahusika na kufanya tafiti kwa ajili ya vyanzo vipya vya umeme hapa Tanzania?
 
Mimi niulize swali, ni nani anahusika na kufanya tafiti kwa ajili ya vyanzo vipya vya umeme hapa Tanzania?
Anayetafuta vyanzo vipya vya umeme ni wizara ya nishati. Lakini pia mashirika yake kama TPDC katika masuala ya gesi na mafuta na tanesco katika masuala ya teknolojia.
 
Hoja hii iliwahi ,kutolewa na watu wengi tu akiwemo Zitto.Kabwe...nafikiri.kuna hoja!
 
Kosa inaanzia hapo kwa maoni yangu, kungekwepo na taasisi ambayo inahusika na tafiti kuhusu vyanzo mbalimbali za umeme.
Pia kungekwepo na taasisi unayojitegemea kwa ajili ya uzalishaji pekee, TANESCO iachiwe kazi ya kusafirisha na kusambaza kwani unapotegemea kitu kutoka kwa taasisi nyingine lazima umakini ufanyike ili kuepuka hasara kwa kila pande
Anayetafuta vyanzo vipya vya umeme ni wizara ya nishati. Lakini pia mashirika yake kama TPDC katika masuala ya gesi na mafuta na tanesco katika masuala ya teknolojia.
 
Financing ya hayo mashirika matatu itakuwaje?
Ni lipi litapokea malipo ya luku? Mzalishaji, msafirishaji ama msambazaji?
 
Kimsingi sina shida na kuimarisha kampuni katika sehemu tatu kama alivosema mh.mbunge. Shida inakuja kwenye modal ya utekelezaji tukiingiza private sector tumepigwa hii nchi naijua utadhani mamangu [emoji23][emoji23][emoji1787]
 
Hoja ya Zitto ya miaka nenda rudi, maccm yanaibuka nayo leo bila hata ya kuacknowledge kuwa hii akili si ya kwao, pumbavu kabisa
 
Kama inashindwa kuperform leo ikiwa chini ya komandi moja hiyo ya sauti tatu unaona itakuwa na tija? Suala la vyeo ni tatizo kwani vyeo siyo majina zina gharama Kama hilo hulijari basi kuna tatizo mahali.
Rea vip sio tawi la Tanesco
 
Hata kama kungekuwa na taasisi ya kuzalisha umeme bado kusingekuwa na ongezeko la umeme kama uwekezaji hauongezeki.

Utafiti wa vyanzo vipya vya umeme haiwezi kuwa kazi ya kudumu bali itafanyika kulingana na mahitaji.

Tatizo tulilonalo ni uwekezaji mdogo (investment) katika vyanzo vya umeme tulivyonavyo.
 
Sio lazima ikiwa break up eti wapewe wawekezaji binafsi,hata ikiwa kama REA sawa..

Hata hivyo hoja ya sijui usalama utakuwa compromised ni upuuzi,huko kwingine inakofanyika wao hawaogopi usalama?

Silaha tuu zinatengenezwa na kampuni binafsi,akina Lugumi wanapewa tenda za kuleta silaha ndio ije kuwa mambo ya umeme?

Kwani saizi hackers wakiamua ku jam tumfumo twa bongo kuna nini tutafanya?
 
Duh!! Hawa jamaa wanamdharau Sana Mama.
Naamini angalau hili ataliepa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…