Elections 2010 Mbunge wa Arusha apigwa hadi kuzirai na jeshi la polisi

Elections 2010 Mbunge wa Arusha apigwa hadi kuzirai na jeshi la polisi

Jamani usanii mwingine ni mbaya sana. Mkurugenzi wa jiji aliwatangazia madiwani wote wakiwamo wa CCM kwamba kuna semina baada ya kutokubaliana kuhusu mamluki kutoka Tanga lakini baadae CCM wao wakaitana baadae Chadema wakshangaa kuwa wako peke yao ktk semina, wakakimbilia Manispaa wakakuta CCM wenzao na yule wa TLP wameshafanya uchaguzi na kujipa umeya na kumpa wa TLP Unaibu

Kama waliambiwa kuhusu semina hiyo kwa maandishi basi huyo Mkurugenzi atakuwa na kazi kujitetea. Mimi kila siku naamini kuwa tatizo letu si wanasiasa bali ni technocrats ambao hawataki kutimiza wajibu wao. Hawa watumishi wa umma wangekuwa na wito hakuna mwanasiasa ambae angefurukuta.

Amandla.......
 
Cha mwisho Ndugu Lema ni lazima afungue kesi za madai na fidia dhidi ya wale wote waliompiga kuanzia kwa huyo Mkurugenzi wa Manispaa. Askari ikiwa ni pamoja na huyo RPC wa hapo Arusha. Anatakiwa awashtaki katika unafsi wao kwani kufanya vitendo vya kuvunja sheria hakulindwi na mamlaka yao. Hakuna cha suluhu katika hilo na kama msaada wa kisheria najua Wanasheria wengi watatoa nami ni tayari kutoa.

Mkuu Rugemeleza,
nadhani ushauri wako kwa Chadema utazingatiwa, kuacha tabia hii ya ukiukwaji wa haki za raia hasa kwa ukatili wa polisi uendelee ni kujenga mazoea mabaya sana. Mbunge si tu raia bali ni kiongozi na mwakilishi wa wananchi katika jimbo lake. Hali au kitendo chochote cha kumdhalilisha ni dharau kwa wananchi anao wawakilisha. Chadema na wananchi lazima iwalinde wawakilishi wao. Nadhani msaada wa kisheria kutoka kwa Rugemeleza ni mwanzo mzuri wa wana JF kutetea haki kwa vitendo. Kudos Mkuu Rugemeleza!
 
kilichotokea Arusha kinatia kinyaa, nchi yetu inakwenda wapi, kuna haja ya kuwachukulia hatua hawa wakurugenzi wanaofanya mambo ya ajabu.
 
Kibs, huwezi kuleta suh a sweeping statement wakati haki na uhai wa mtu viko hatarini

Ujuaji mwingi kwamba CCM wamepiga kura bila CHADEMA?
ujuaji mwingi kwamba LEma amepigwa hadi kuzirai?
ujuaji mwingi kwamba wapinzani hawana haki?
au nini hasa?

this is too low of you and surely i didnt expect you woudl come in a MS kind of mentality

Maybe i am blind to think there a few good people remaining in CCM right now
Tatizo wengi mnajifanya kuwa ni vipofu kwa mtaji kuwa ni wapinzani, sheria ni msumeno. Iwapo alivunja sheria kwa kigezo kwamba yeye ni Mbunge kwa nini asichezee kibano? Vibaka wangapi wanasurubiwa na hao polisi? raia wangapi ambao wamepingwa na hao polisi ilhali hawana hatia yoyote?

Kama umeona kuwa mbunge huyo hajatendewa haki ya kula kibano cha mbwa mwizi, ni vema ukangalia tena ni namna gani jeshi hilo la polisi linavyofanya kazi hapo nyumbani! Sio siri kuwa ni wababe! Na wanajeuri ya kumpiga mtu yoyote! Huyo Mbunge kalewa madaraka na kujitia mjuaji, na anastahili yaliyomkuta. Pengine itakuwa fundisho kwake... Kama ana akili njema akirudi bungeni hana budi kuwa na hoja binafsi juu ya uharamia wa jeshi hilo!

Simwonei huruma yoyote kwa upumbafu wake alioufanya! Na sitajali kwa kiasi gani unaweza kunihukumu kwa hili, kwani hata mimi binafsi yamenishanikuta hayo nikiwa hapa hapa JF!

Ka'amua kujizarilisha, na hamezarilishwa!

Mkuu, unasherehekea mtu kupigwa na chombo ambacho kiko kwa ajili ya usalama wake? Tutafika kweli hivi?

Amandla.......
Naam, kama unaona ninashereheka sawa tu. Cha msingi iwapo alishindwa kuheshimu sheria, yaliyompata ni halali kwake!
 
Tatizo wengi mnajifanya kuwa ni vipofu kwa mtaji kuwa ni wapinzani, sheria ni msumeno. Iwapo alivunja sheria kwa kigezo kwamba yeye ni Mbunge kwa nini asichezee kibano? Vibaka wangapi wanasurubiwa na hao polisi? raia wangapi ambao wamepingwa na hao polisi ilhali hawana hatia yoyote?

Kama umeona kuwa mbunge huyo hajatendewa haki ya kula kibano cha mbwa mwizi, ni vema ukangalia tena ni namna gani jeshi hilo la polisi linavyofanya kazi hapo nyumbani! Sio siri kuwa ni wababe! Na wanajeuri ya kumpiga mtu yoyote! Huyo Mbunge kalewa madaraka na kujitia mjuaji, na anastahili yaliyomkuta. Pengine itakuwa fundisho kwake... Kama ana akili njema akirudi bungeni hana budi kuwa na hoja binafsi juu ya uharamia wa jeshi hilo!

Simwonei huruma yoyote kwa upumbafu wake alioufanya! Na sitajali kwa kiasi gani unaweza kunihukumu kwa hili, kwani hata mimi binafsi yamenishanikuta hayo nikiwa hapa hapa JF!

Ka'amua kujizarilisha, na hamezarilishwa!

Naam, kama unaona ninashereheka sawa tu. Cha msingi iwapo alishindwa kuheshimu sheria, yaliyompata ni halali kwake!

Inasikitisha kwani kushabikia mtu kupigwa na polisi ni jambo la ajabu sana. Hata kama Ndugu Lema angekuwa ni mbabe au mjuaji hastahili kupigwa hata kidogo. Hakuna hata sheria moja ya nchi yetu inayomruhusu polisi au mtu yeyote yule kumpiga mtu mwingine. Kilichopo ni kuwa Polisi wao ndio wanatakiwa kuhakikisha kuwa sheria za nchi yetu zinaheshimiwa. Sasa wewe unasema anastahili alichokipata hivi kweli wewe unaitakia mema nchi yetu au unataka nchi yetu itawaliwe na wababe na watu wasio heshimu sheria? Ninapenda kukuambia suala hili si tu ni aibu kubwa kwa serikali ya Kikwete na CCM bali ni aibu kubwa kwa nchi yetu na sisi sote kama Watanzania.

Tukiendekeza na kushabikia uhuni na ubabe huu muda si mrefu hakuna atakayekuwa na haki ya kusema chochote. Tunafahamu wababe wengi walivyoweza kutawala watu duniani na wakapata wanazi na wapenzi wengi. Unazi na ushabiki huo ndio ulisababisha mauaji ya maangamizi huko Ujerumani, Rwanda, Uganda na sehemu nyingi sana duniani. Gharama za kupambana na udhalimu huo zilikuwa kubwa kwani Urusi katika kupambana na udhalimu wa Hitler ilipoteza maisha ya watu milioni 27! Rwanda watu karibu milioni moja wamepotea. Sudani mamilioni wamepotea. Kama tulivyokuwa tunaimba kama Chipukizi wa Tanu kuwa "mtu asiyejua kufa mwambieni aone kaburi" nadhani ndugu yangu wewe hujui kufa na hivyo naomba uende ukaangalie makaburi ya watu waliouawa na wadhalimu ambao inaelekea wameamua kutwaa madaraka au kutumia madaraka ya nchi yetu ili kuendeleza uovu wao.
 
Tatizo wengi mnajifanya kuwa ni vipofu kwa mtaji kuwa ni wapinzani, sheria ni msumeno. Iwapo alivunja sheria kwa kigezo kwamba yeye ni Mbunge kwa nini asichezee kibano? Vibaka wangapi wanasurubiwa na hao polisi? raia wangapi ambao wamepingwa na hao polisi ilhali hawana hatia yoyote?

Kama umeona kuwa mbunge huyo hajatendewa haki ya kula kibano cha mbwa mwizi, ni vema ukangalia tena ni namna gani jeshi hilo la polisi linavyofanya kazi hapo nyumbani! Sio siri kuwa ni wababe! Na wanajeuri ya kumpiga mtu yoyote! Huyo Mbunge kalewa madaraka na kujitia mjuaji, na anastahili yaliyomkuta. Pengine itakuwa fundisho kwake... Kama ana akili njema akirudi bungeni hana budi kuwa na hoja binafsi juu ya uharamia wa jeshi hilo!

Simwonei huruma yoyote kwa upumbafu wake alioufanya! Na sitajali kwa kiasi gani unaweza kunihukumu kwa hili, kwani hata mimi binafsi yamenishanikuta hayo nikiwa hapa hapa JF!

Ka'amua kujizarilisha, na hamezarilishwa!

Naam, kama unaona ninashereheka sawa tu. Cha msingi iwapo alishindwa kuheshimu sheria, yaliyompata ni halali kwake!

Kibunango,

Yamkini unapashwa ukapimwe akili. Hakuna mahali popote ambako Polisi anaruhusiwa kumpiga mtu kwa sababu yoyote ile. Wanatakiwa kumkamata mtu na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria!!! Hivi nchi ikiwa na watu wanye kuchukulia mambo kama wewe si itakuwa balaa na hatari????

Tiba
 
Leta hapa taratibu za uchaguzi wa meya katika majiji tuone kama arusha zimevunjwa

leta hapa sheria inayosema mbunge akihatarisha amani kwa kuwa yeye ni mbunge aachwe atende atakalo hata kama amani ya nchi itapotea

tuacheni ushabiki wa kitoto kama kweli wao walikua hawakubaliani na utaratibu wangelikuwemo kwenye kikao na wakapingana kwa hoja, diwani wa tlp anawafata na kuwaambia twendeni tukapambane kule wao wanasusa, waliposikia jamaa weshakula wananawa wanakuja ooh na ss.

Chadema jipangeni watanzania watakuchokeni au weshaanza kukuchokeni.
 
Ngogo mbona sababu ya CDM kutoingia kwenye kikao iko wazi! Taratibu zinaruhusu kujiongezea wajumbe ili kushinda uchaguzi?
Ngongo anachuki binafsi na Godbless Lema naaliapa hatashinda akimpigia kampeni yule wa TLP ambae alikuwa hajulikani achilia mbali kukubalika sasa naona chuki za Ngongo dhidi ya Lema bado zinaendelea....
 
Leta hapa taratibu za uchaguzi wa meya katika majiji tuone kama arusha zimevunjwa

leta hapa sheria inayosema mbunge akihatarisha amani kwa kuwa yeye ni mbunge aachwe atende atakalo hata kama amani ya nchi itapotea

tuacheni ushabiki wa kitoto kama kweli wao walikua hawakubaliani na utaratibu wangelikuwemo kwenye kikao na wakapingana kwa hoja, diwani wa tlp anawafata na kuwaambia twendeni tukapambane kule wao wanasusa, waliposikia jamaa weshakula wananawa wanakuja ooh na ss.

Chadema jipangeni watanzania watakuchokeni au weshaanza kukuchokeni.

Nani alete?? weka hizo sheria na taratibu badala kuagiza.

Kwani wewe umewahi kuipenda CDM?
Nani kasema watanzania wameichoka CDM?? au Redet tayari wamefanya utafiti?
Mbona mie sijaichoka CDM na bado ni Mtanzania, au hao watanzania wanatoka sayari gani????
 
Wana JF naomba confirmation and update on the story. Kuna rafiki kanihabarisha kwamba mbunge Lema yupo hoi hospitalini baada ya kupata kichapo cha Polisi huko Arusha. Sijui ndo mambo ya chaguzi za Umeya?

Kama walikusudia kuua vile!
 
Don't just complain.Play your part.Tanzania must be a land for all Tanzanians and not for CCM only.
Don't abandon A-Town electorates for daring to dump CCM.Jamani tuwaunge mkoni kupambana na uhuni huu wa Gbago style.
 
Mbona mmezidi kulalamika sana na hakuna watu ambao wako tayari kuchukua hatua? Tumelala sana na kuona kwamba kama tukitoka kwenda kudai haki zetu TUTAONEKANA WAHAINI SIYO KWELI LAZIMA KUWE FREEDOM FIGHTER AMBAO TUTAWEKA HISTORIA tumezidi kujitetea na woga wetu na kuishia kulalamika na kuandika mambo marefu ya manung'uniko tu.

Hapa Arusha kuna watu wa marika mbalimbali watatuelewa tu na dunia nzima itakuwa nyuma yetu.

Kila mtu anaweza kupanga hata tukio moja kwa kusanya vijana kama 10 mpaka 20 ambao watakuwa wasiri na wakafanya matukio ya kuchoma moto na kuharibu mali za serikali pamoja na ofisi za chama tawala na atayeleta mdomo apewe hata kilema cha maisha.

Hii inatia uchungu na hasira za kutosha mtu yeyote mzalendo wa kweli unaibua mpaka magonjwa yaliyo lala kama vidonda vya vya tumbo na hata shinikizo la damu kwa nini tunanyanyasika nchini mwetu??????????

Hii ndo hatua pekee ya kuchukua hamna jingine! Sasa tunaona umuhimu wa kujitoa mhanga
 
Mkuu sina hakika kuhusu uhalali maana wanasema hata kama ingekua Chadema wamesusa kweli bado huyo Meya hajapata 2/3 ya kura za madiwani wote.

Kama kikao cha uchaguzi kinafanyika kama idadi ya madiwani inazidi nusu ya madiwani wote basi kikao hicho ni halali(unless kama madiwani wa Chadema hawakutaarifiwa kuwa kuna uchaguzi); na mshindi wa Umeya anapatikana kwa simple majority ya madiwani waliopiga kura.

Hivyo kama Chadema walijua kuwa kuna kikao cha uchaguzi na wao kufanya kosa la kutoshiriki kwenye kikao cha uchaguzi, basi huyo meya aliyechaguliwa ni halali.
 
Mgombea wa CCM kule Maswa alompiga mtama OCD hadi chini puuu!.Uliza kilichoendelea.Lema,Mbunge,akiwa kwenye shughuli rasmi kabisa za kazi yake, anadaiwa kutishia unajua kilichomtokea.Jamani tuamke sasa.
 
Heshima kwenu wanjamvi,

Ni kweli Mbunge wa Arusha Mheshimiwa Godbless Lema kapigwa sana na polisi [FFU].
Jana iliamuliwa kikao cha kumchagua Meya wa Jiji la Arusha kifanyike leo saa 3 asubuhi,kikao cha jana kilishindwa kumchagua Meya kwasababu CCM walitaka kumchomeeka mjumbe kutoka Tanga ili kuwasaidia kwenye mchakato wa kupiga kura pamoja na mizengwe ya kumchomeka mjumbe wa Tanga lakini bado CHADEMA walikuwa na nafasi ya kushinda kwakuwa diwani wa TLP Mheshimiwa Kivuyo alikuwa akiwaunga mkono CHADEMA.

Maajabu yalianza kujitokeza hiyo saa 3 asubuhi badala ya wajumbe wa CHADEMA kwenda kwenye kikao cha kumchagua Meya waliamua kufanya kikao Hotel Ikweta mkabala na ukumbi wa manispaa ya Arusha.Mheshimiwa Kivuyo baada ya kuona wajumbe wa CHADEMA hawaingii kwenye mkutano aliamua kuwafuata Ikweta Hotel kuwasihi wahudhurie kwenye kikao kwakuwa bado walikuwa na nafasi ya kushinda kiti cha umeya lakini juhudi zake hazikuzaa matunda wajumbe wa CHADEMA waliendelea kususia kikao cha uchaguzi wa Meya.

Mwenyekiti wa kikao cha uchaguzi wa Meya Bwana E Chang'ah aliamua kufanya mawasiliano na ofisi ya waziri mkuu.Waziri wa nchi Tawala za mikoa na serekali za mitaa alitoa maagizo sheria zifuatwe kwa kuwa idadi ya wajumbe ilifikia nusu mchakato wa uchaguzi ukaendela bila ya wajumbe wa CHADEMA kushiriki kwenye kikao.Wajumbe wa CHADEMA wakajulishwa Meya tayari kachaguliwa wakaamua kuingia kwenye kikao wakiongozwa na Mheshimiwa Mbunge G Lema.Zilitokea purukushani za hapa na pale Lema akachomoa bastola FFU wakmvamia na kumpokonya na kumpiga vibaya sana.

Wanajamvi CHADEMA hawakuwa na sababu za kutoingia ndani ya kikao cha uchaguzi wa Meya.Meya alipochaguliwa wajumbe wa CHADEMA wakaamua kuingia sijui waliingia kufanya nini ?.Lema hakutakiwa kutoa bastola yake wakati askari wa usalama walikuwepo eneo la tukio sijui alitaka kumpiga nani ?.Ikumbukwe Lema ana kesi ya kutishia kuuwa Mkurugenzi wa Jiji.

Unapokuwa na nusu ya wajumbe wana sera tofauti siyo suala la kulazimisha. Hapa ilitakiwa kuwe na makubaliano ya madaraka iwe kugawana vipindi nusu kwa nusu au meya CDM na naibu meya ccm. Kwa walivyofanya uongozi utakuwa mgumu haijapata tokea
 
I hope Anna Makinda atasema kitu in defence ya Lema juu ya hili! Naamini kabisa Sitta pamoja na UuCCM wake angefyatuka. Tukikubali wabunge wawe wanapigwa.....!

Wabunge nao ni raia wa Tanzania, suala hapa sio mbunge kupigwa bali ni jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa pasipo sababu.Lakini kitendo cha Lema kuitoa bastola yake kinawapa nafasi polisi kujifanya kuwa walikuwa wanajilinda/kulinda maisha ya waliokuwepo kwenye kikao hicho.
 
Kiongozi wa kambi ya upinzani Arusha ambaye ni Diwani wa Chadema, Kata ya Elerai, John Bayo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanatarajia kwenda mahakamani kesho (Desemba 20) kufunuga kesi kupinga uchaguzi huo kutokana na baadhi ya kanuni kutofuatwa.

Bayo alifafanua kwamba mojawapo ya kanuni iliyokiukwa ni kutozingatiwa kwa idadi ya theluthi mbili ambao ni madiwani 20 wenye mamlaka ya kumchagua meya na naibu wake.

My Take
Meya aliyechaguliwa hatokuwa halali kwa sababu kikao hakikuwa halali. Tutofautishe quorum kutimia na kanuni ya ushindi wa simple majority
 
Ati kisa katoa Bastola kwaajili ya kujilinda...walimpa bastola ya nini kama si ya kupambana na watu washenzi wanaompiga mtu hadi azimie!..Kwanza alitakiwa ampe mmoja ya ugoko!

Hapa namuomba Mwema apime na kutafakari umuhimu wa polisi kutumia that kind of excessive power dhidi ya raia wema. Atoe majibu hadharani kama bado tunamhitaji kwenye nchi ya amani kama Tanzania maana tulidhani baada ya Mahita tumepata mkombozi kumbe sivyo. Kuna tofauti kubwa kati ya kupambana na jambazi na raia mwema hiyo ni kazi yao!
 
Sasa na hii issue ya Bastola imetoka wapi?????

VOR ukiwa na siraha it is even too risk. Unaweza kuzushiwa lolote na mimi kwa Lema naona kosa lake ni kutembea na siraha. Watamzushia yote ikiwa na kumtishia mkurugenzi. Jamani, simfahamu Lema lakini machozi yananilenga kusikia kadondoka baada ya kuachiwa. Mungu ninaye mwamini atamponya. Sina itikadi ya siasa, inaniuma kama Mtz!
 
Back
Top Bottom