Mbunge wa Arusha Mjini, kikao kijacho cha Bunge usisahau kufuatilia kiwanda cha General Tyre

Mbunge wa Arusha Mjini, kikao kijacho cha Bunge usisahau kufuatilia kiwanda cha General Tyre

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
40,051
Reaction score
51,217
Kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre kiliwahi kuwa na mchango mkubwa sana katika uchumi wa mkoa wa Arusha na Taifa kwa ujumla.

Kili generate ajira nyingi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Shughuli za kiuchumi zilichangamka kiasi chake.

Baada ya kusimamishwa shughuli zake mkoa umepata pigo kwa kweli kwani shughuli za kitalii nazo ni za msimu.

Namkumbusha tu mbunge wa Arusha mjini , akifika bungeni kikao kijacho asiache kuulizia serikali kuhusiana na kukifufua kiwanda hiki.
 
Labda kaka kwa kuongezea. Wakifufue tena hiki kiwanda. Kikikuwa top kwenye suala la utengenezaj matair hapa nchini. Wawekezaji wamekichezea mpaka kikafungwa.
Sahihi kabisa mkuu ni vyema wakakifufua.
 
Kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre kiliwahi kuwa na mchango mkubwa Sana katika uchumi wa mkoa wa Arusha na Taifa kwa ujumla...
Huyo mbunge na serikali ya awamu ya 5 hawana uwezo wa kufufua hicho kiwanda.
 
Thubutu, hana ubavu ata chembe ya kurejesha hiko kiwanda, jiwe mwenyewe kashindwa sembuse huyo mchovu.
 
Haya mambo ya msingi ni zaidi ya kupiga domo kisiasa, jiulize kwanza issues kama management, raw materials, na capital, plus mashine vipo?

Sio huyo mbunge wa kura feki akatembelee hicho kiwanda halafu apige selfie mtuoneshe kwenye mitandao then biashara iishie hapo.
 
Mbunge mmoja alisema badget yote iliyotengwa kwa ajili ya biashara na viwanda haitoshi kufufua kiwanda cha general tire kwani Kutaitajika ufungaji wa mashine mpya za tubeless kuendana na technology ya sasa
Ipo haja ya kukipa kipaumbele hiki kiwanda kama bajeti ya wizara husika haitoshelezi.
 
Back
Top Bottom