Mbunge wa CCM badala ya kujadili kero za ugumu wa maisha, anashauri Mawaziri wajengewe sehemu za starehe. Hii ni aibu

Habari za uzima wanajamii!

Naomba nielekee kwenye mada husika kama inavyosomeka, Hili suala limesikika leo kwenye kikao cha bunge baada mbunge mmoja kulifikisha bungeni kama hoja(Pendekezo) kwa spika wa bunge Mh. Tulia Aksoni akiiomba serikali iwape msaada wa ujenzi wa Hotel & Nightclub(Faragha) katikati ya mji wa Dodoma(Capital City) kwa kuhofia kuchangamana na wananchi ili kuepuka kuvuja kwa nakala za serikali pamoja na kulinda mazungumzo yao binafsi wanapokutana baada ya vikao vya siku kukamilika, Nakuendelea zaidi kuwa itakua ndio sehemu yao pekee kwa mapumziko kwa vipindi vyote wakiwa huko na kuongezea zaidi kwakua ofisi nyingi za serikali zimehamishia makazi yake kwenye mji huo wa Dodoma kwa hivyo itakua ni njia rahisi ya kukutana na watumishi wa ngazi za chini kutoka wizara na idara tofauti za kiserikali pasipo mashaka yoyote yale ambapo hali ni tofauti na ilivyo kwa hivi sasa..

Swali: Hii hela itakayoenda kutumika kukamilisha ujenzi huo, Endapo ombi litakubaliwa zitatoka kwenye fungu lipi la Mapato serikalini?
 
Zile pesa Makampuni ya simu wanaturudishia sh 50 mara 100...wakajenge hiko huko Dodoma
 
Wajengewe night club wakati huko mbeya wanafunzi wanasoma kwa shida hata madawati ya kukalia hawana
 
Ameshashiba anaropoka tu nazani akishatoka kwenye hicho kiti akaja uraiani nazani atapata akili

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mambo yao binafsi wasiyaingize kwenye mambo ya Taifa! Tabia ya ubinafsi ikizidi sana ndio akili na aibu hujiweka kando!
Hii ni aibu sana kiukweli. Usijadili maisha ya unaemuwakilisha, unazungumzia starehe zao! Hii inaonesha kabisa kwamba hawakustahili kuwepo hapo walipo
 
Hili ndilo bunge marehemu alitaka liwe hivyo!!ili awe Raisi wa maisha
 
WABUNGE wa BUNGE hili ukiwapeleka Kenya ni MADIWANI
 
Ni mjinga kama wajinga wengine!
 
Matatizo yao ndio muhimu, wataanza kuomba waongezwe posho. Hajui kazi ya mbunge ni nini, kwake starehe yao ndio ilimpeleka bungeni
 
hapo ndio kakaa kafikilia weee kafika mwisho.... Kasafiri mamia ya Km eti kaenda kuwakilisha wananchi wake.
 
kabisa yani anaacha kujadili mambo ya msingi anaongelea club mambo yaliyopitwa na wakati,siku hizi tekinolojia imekua sio kama zamani mambo ya kukutana sehemu for what?
Hizo akili zakujadili mambo ya msingi atazitoa wapi?.Hapo ndipo uwezo wake ulipoishia.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…