Mbunge wa Geita Mjini anatia mashaka. Anataka kusema Musukuma ni muongo?

Mpaka likamilike bro,sasa tunajadili kilichopo mezani,ndio maana amemlipua mkurugenzi.
Likamilike gani mkuu tayari kule Nzera sasa kuna watumishi? Na DED yupo kabisa! Juzi tu Msukuma mwenyewe kafanya ziara ya kushtukiza maana kama watumishi walikuwa wameweka kamgomo fulani hivi ka kuhamia huko! Msukuma anafanyakazi kwa mihemko na hapo ataanzisha ugomvi na Mh. Kanyasu usiokuwa na mwisho!
 
Kanyasu anatetea ufisadi!
Waziri mkuu alitowa kibali, msipende kuonea watu.

Mkurugenzi wa Temeke amenunua V8 kwa Million 400 pia, hiyo kamati ikitoka Geita iende Temeke.

Mimi nafurahi tu hawa wakurugenzi kutiwa adabu kwa sababu ndio mitambo ya wizi wa kura, wao ndio wanajuwa jinsi walivyoiba uchaguzi muwaache kabla hawajaanza kuwavuwa nguo.
 
Lakini wakati gari linanunuliwa baraza lilikuwa moja?
Hapo uko sawa kabisa mkuu! Ingawa labda tuseme mchakato wakati unapitishwa baraza lilikuwa moja! Lakini Msukuma anajitoa ufahamu tu wakati wanapitisha na yeye alikuwamo!
 
Kwa hiyo baraza la madiwani limezinduliwa? Au wapo kwenye hatua za kuanzisha halmashauri?
 
Yaani wanavyowafukuza muda si mrefu wakaanza kuwaumbua! Hata huyu Msukuma wanaenda kusema sasa hivi kwamba bila sisi Msukuma usingekuwa mbunge maana ulikuwa umeangushwa!
 
Huyo mkurugenzi akapumzike, hamna namna.. sijaona mtu anayeweza kupimana nguvu na joseph kasheku Msukuma.
Mkurugenzi ndiye anayejuwa siri yote ya uratibu wa kuiba kura.

Huyo msukuma amewekwa hapo na mkurugenzi.
 
Mkurugenzi hakujua nguvu ya mbunge..kifupi walikuwa wanamchukulia poa msukuma..msukuma alipomfuata alitakiwa amueleweshe na kama hahusiki na ununuzi alitakiwa aweke documents..kinyume na hapo anamuambia kwanza tunanunua manne tena.
Kimsingi Mkurugenzi ndio mwenye nguvu kama akijitambuwa na kuzitumia nguvu zake.

Wakurugenzi nchi nzima ndio waliosimamia na kuratibu wizi wa kura.

Tatizo la Watanzania wengi ni wanafki na waoga, Membe angekuwa ndio mkurugenzi asingeguswa na mtu, angewaambia tu niguse unuke.
 
Bwashee naona mnaparurana tu
Ni fisadi tu anayeweza kuongea bila uoga kuwa zile sh 400m zilitoka kwenye fedha za ndani hivyo ilikuwa halali kununua gari hilo.

Kanyasu angekuwa China kwa utetezi aliotoa kitanzi kingemuhusu!
 
Cha ajabu hela zilipokuwa zinatumika kununua wapinzani na chaguzi kurudiwa kwa mabilioni ya hela hatukuskia izi kelele zenu

Huu uzalendo wa kinafiki mi ndio ninaoukataa.
 
Yaani wanavyowafukuza muda si mrefu wakaanza kuwaumbua! Hata huyu Msukuma wanaenda kusema sasa hivi kwamba bila sisi Msukuma usingekuwa mbunge maana ulikuwa umeangushwa!
Mkurugenzi wa Temeke amenunuwa V8 kwa Million 400 Meya akaleta mdomo akampa lile gari akaagiza V8 nyingine ya million 400 ndani ya miaka hii mitano ya hiki kishindo cha awamu ya tano, ni unafki mtupu.
 
Mbona chaguzi za maigizo za waunga juhudi zilitumia mabilioni ya shiling, lakini hatukuskia izi kelele za matumizi mabaya ya pesa?

Ifikie kipindi watanzania tuache unafiki, haya yote ni kwa sababu rais kaongelea hili suala. na tunachokiona hapa ni unafikk wa baadhi ya watu kujifanya wana uchungu wa fedha za kodi za watanzania .....cha ajabu wanachagua fedha gani wawe na uchungu nazo!.
 
Huwezi kuwa msafi,mwadilifu,mchapakazi na mcha Mungu halafu ukawa CCM.
Fisi kala fisi.
Mbwa kala mbwa.
 
Kama huu ndiyo utaratibu basi tunatawaliwa na mashetani na siyo binadamu. Mbona kuna magari ya bei rahisi mengi na yenye kufaa kwa hiyo kazi.
Tatizo we huelewi sababu zinazofanya wanunue magari ya mil 400.

Ni hivi!, sababu inayofanya wanunue magari ya bei kubwa ni kwa sababu yanadumu muda mrefu na hayaharibiki ovyo ovyo.

Ni bora kununua gari ya mil 400 itakayodumu kwa miaka 15 kuliko kununua gari ya milioni 70 itakayokuwa inahitaji matengenezo ya mara kwa mara na haiwezi kudumu kwa muda mrefu

Ni sababu za kiuchumi zaidi na sio kwamba walikaa wakakurupuka kwa matakwa yao binafsi, na hizi standard zimewekwa na serikali yenyewe na sio kwamba mkurugenzi kajiamulia tu!.
 
Kwahiyo mkurugenzi ni mzalendo?!
 
We jamaa una simu Kama yangu Tecno F1
 
Mkuu kosa si kutokufata utaratibu ama ufisadi katika gharama za kununua gari.

Shida na mtafaruku uliopo ni je gari hilo ni kipaumbele cha kwanza kabla ya mathalani ununuzi wa madawati kwa wanafunzi wanaokaa chini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…