Tungetanguliza utu, uzalendo, upendo, na uadilifu, maamzi ya kufanya hicho mlichofanya Geita na maeneo mengine kisingefanyika.
Gari moja 400M, tena sio ambulance wala grader kwa ajili ya kutengeneza miundombinu, ni gari la kumbeba kiongozi! Hizo fedha za ndani ni fedha mlizokusanya kwenye shughuli za mikono ya walalahoi, bila huruma, mkurugenzi na menejiment yako mkakusudia kununua gari hilo.
Kuweni na utu jamani. Mnataka hadi maamuzi ya kizalendo aje Mh awasimamie? Sasa Mh Rais atafanya kazi ngapi?
Wakati Mh Rais anahangaika kutafuta pesa kwa ajili ya kujenga miundombinu wakati mwingine hadi kukopa, wengine huku mnatumia hela kwa utaratibu huo, kuna haja gani ya kukopa na kuongeza deni la Taifa wakati hela matumizi yetu yanakuwa kama hayo?
Tumtangulize Mungu katika maamuzi yetu, na utu kwanza.