Nampa Hongera zake, huyu ni mwana jf mwenzetu, na alikuwa active member wa jf kwa kuchangia humu jf wakati akiwa ni Mbunge tuu, baada ya kuteuliwa uwaziri, wakati wote akiwa Waziri, hakuwahi kuchangia chochote jf, ila kulipoibuka timua timua ya wenye vyeti feki,
Likapandishwa bandiko humu jf kumtuhumu
Mwigulu Nchemba kuwa ana vyeti fake,
Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito - JamiiForums
Ndipo Mwigulu Nchemba akaibuka tena jf kujibu tuhuma ya vyeti fake
Majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu tuhuma za kughushi vyeti vya taaluma, kuiba jina - JamiiForums
Na sisi watetezi wa ukweli pia tukamtetea kuwa
Vyeti vyake Mhe Mwigulu Nchemba sio vyeti fake, ni vyeti bonafide genuine, vya ukweli na halisi
Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli - JamiiForums
Baada ya utetezi ule wa jina, Member mwenzetu huyu hakukanyaga tena jf hadi baada ya kutumbuliwa uwaziri na kuendelea na ubunge tuu, alirejea jf na bandiko la kampeni ya 2020 na kuturuhusu kumuuliza maswali yoyote, ni kweli wana jf tulijitokeza na aliulizwa maswali mengi na magumu na akajibu, japo kuna maswali kidogo tuu tena marahisi, Mwigulu Nchemba hajayajibu mpaka leo
Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020 - JamiiForums
Sasa ndio kateuliwa tena kuwa Waziri, sijui this time kama atachangia changia tena jf.
Mimi kwa upande wangu, huyu jamaa namkubali sana tuu!.
Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa! - JamiiForums
Hongera sana Mhe. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, uteuzi huu ni uthibitisho wa imani ya rais Magufuli kwako, na unatuma salaam, nzito kwa waliokuwa wanalimendea jimbo lako,
"NI HESABU MBAYA SANA KUPAMBANA NA MAMBA KWENYE KINA KIREFU CHA MAJI"
Nakubaliana kabisa na wewe.
Hongera sana.
P