Mbunge wa Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

Mbunge wa Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

Mwigulu kateuliwa ili tu kuwaziba mdomo waliozomea ushauri wake kuhusu takwimu za corona, mzee ni wa visasi lengo ni kuonesha jeuri tu za kitemi.

Mimi sipangiwi, ukinishauri nd’o umeharibu kabisa.
 
Matunda ya kwenda kwa mganga wa Lagos yameonekana, bado mzee wa uno Kangi mwenye moyo mgumu au hana nauli ya kwenda Lagos 😂
 
.
IMG-20200502-WA0011.jpg
 
Yaan hili la leo ndo linanifabya kila siku nikumbuke kauli ya raisi kenyata kuwa kazi yako siku ukifa hata Kabla ya kuzikwa boss atatafuta mtu mwingine Watoto wako ,mke wako watafukuzwa kwenye nyumba ya kampuni ,hivyo ni bora kumiliki biashara hata ukifa ghafla ndugu na wanao watarithi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera ndugu Mwigulu Nchemba

Ama kweli KUFA KUFAANA......!!!
Naanza kutilia mashaka sana ile speech ya huyu Madelu akiwaponda CHADEMA..... Likely it was pre-planned .....!!!
Angakizo kwa Wabunge Vijeba/Vibabu kutoka CCM wajitafakari upya maana Covid-19 haitawaacha salama maadamu kikao Cha Bunge kinaendelea....!!
 
  • Thanks
Reactions: bea
Amemuita na kumtosa mkumbo

Msisahau pia singida imetetereka kwani posho za uwaziri zilisaidia kuendesha club vilevile amejutia mapungufu hivyo anastahili
 
Madelu yuko juu japo ana ushetani wake.
Muntua anto sika akupendile vibaya mno ekolye neke
 
Mwigulu hana sifa wala hastahili kuwa Waziri wa Katiba na Sheria!
 
Huyu mramba viatu msimamo wake ukoje juu ya tume huru ya uchaguzi?
 
'Oooh, tumeondokewa na mwanadiplomasia nguli...pengo lake si rahisi kuzibika!' Shubaamit!...Why so quickly like this?! Heshima kwa marehemu iko wapi?

Yaani ni sawa mtu anafiwa na Mwenza leo, kesho anaoa au kuolewa. Wizara hiyo ingekuwa ya Afya kusingekuwa na Swali muda huu wa Corona. Condom yenyewe imetepeta hiyo, itasaidia nini?
 
Jamaa ana hasira za kitoto sana anafikiri anatukomoa kumbe anajiabisha mwenyewe yaan hapo kawajibu CHADEMA na hotuba ya mbowe walivyomtaka awe mstari wa mbele kwenye vita ya corona,

Ameonyesha kukubaliana na hoja za mwigulu alizosema kua rais sio nurse na Kama mnavyojua hua anamteua mtu asiyependwa na watu ili atukomoe tu kitendo cha mwigulu kusema vifo visitangazwe wengi walimponda mwigulu Sasa jiwe kamteua ili awaumize roho tu.

Mwigulu asifikiri kateuliwa kwa kua rais kapenda hapana ni sababu ya hasira tu, kitila mkumbo Sasa atafute Jimbo lingine
 
Nampa Hongera zake, huyu ni mwana jf mwenzetu, na alikuwa active member wa jf kwa kuchangia humu jf wakati akiwa ni Mbunge tuu, baada ya kuteuliwa uwaziri, wakati wote akiwa Waziri, hakuwahi kuchangia chochote jf, ila kulipoibuka timua timua ya wenye vyeti feki,
Likapandishwa bandiko humu jf kumtuhumu
Mwigulu Nchemba kuwa ana vyeti fake,
Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito - JamiiForums

Ndipo Mwigulu Nchemba akaibuka tena jf kujibu tuhuma ya vyeti fake
Majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu tuhuma za kughushi vyeti vya taaluma, kuiba jina - JamiiForums

Na sisi watetezi wa ukweli pia tukamtetea kuwa
Vyeti vyake Mhe Mwigulu Nchemba sio vyeti fake, ni vyeti bonafide genuine, vya ukweli na halisi
Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli - JamiiForums

Baada ya utetezi ule wa jina, Member mwenzetu huyu hakukanyaga tena jf hadi baada ya kutumbuliwa uwaziri na kuendelea na ubunge tuu, alirejea jf na bandiko la kampeni ya 2020 na kuturuhusu kumuuliza maswali yoyote, ni kweli wana jf tulijitokeza na aliulizwa maswali mengi na magumu na akajibu, japo kuna maswali kidogo tuu tena marahisi, Mwigulu Nchemba hajayajibu mpaka leo
Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020 - JamiiForums

Sasa ndio kateuliwa tena kuwa Waziri, sijui this time kama atachangia changia tena jf.

Mimi kwa upande wangu, huyu jamaa namkubali sana tuu!.
Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa! - JamiiForums

Hongera sana Mhe. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, uteuzi huu ni uthibitisho wa imani ya rais Magufuli kwako, na unatuma salaam, nzito kwa waliokuwa wanalimendea jimbo lako,

"NI HESABU MBAYA SANA KUPAMBANA NA MAMBA KWENYE KINA KIREFU CHA MAJI"
Nakubaliana kabisa na wewe.
Hongera sana.
P
 
Back
Top Bottom