Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AKILI YAKO NDO INAKUTUMA UFIKIRI HIVYO.Sababu wanazotoa wengine mpaka wanatia aibu leo Mbunge wa Jimbo la Singida mashariki Tundu Lissu yupo hospital kwa muda wa mwaka baada ya jaribio la kutaka kumuua kufeli leo Mbunge anaenda kujiunga na hao maharamia
Lazima imuume maana ni kodi yake hiyo, wewe usiyelipa kodi kwako ni sawa tu.Imekuuma etiiiii
Wanavuna kwa bidii maembe ili kuudhofisha mti wa muembe, what a silly strategy!!Sasa wana shambulia ngome ya lowasa huku wana endelea na mashambulizi kwenye ngome ya mbowe pale Hai
Ambatanisha risiti za manunuzi kama ushahidi. La sivyo acha udaku.Ni upuuzi ccm kuiba hela za serikali na kununua upinzani...
Kazi tunayo! Yaani hayo ndiyo yakufurahishayo?Daaaah yani Tanzania naona kabisa upinzani unakufa, wabunge wengi wanaondoka, yajayo yanafurahisha.
Ushauri wa bure, ukitaka kuuangamiza mwembe usichume maembe, kata mizizi kabisa. Kukata mizizi ya upinzani Tanzania ni kufanya yafuatayo na mengine mengi;2020 chadema kitarudia status quo yao ya kuwa na wabunge wanne tu. Wameitumia vibaya fursa waliyokuwa wameipata. Yaani ruzuku kazi yake ni kulipia tu deni hewa la m/kiti wao. Yaani wabunge wao lazima 50% ya mishahara yao ipelekwe kwenye chama kulipia hilo deni hewa la m/kiti lisiloisha!! It is now over! Wamasai na wakurya wamekataa. Wambeya (wahehe) wamekataa. Kila mtu amekataa.
Kwenye ripoti ya CAG hiyo taarifa ipo kwenye ukurasa gani.Hapa duniani hakuna binadamu ambaye si mchumia tumbo. Hata mimi na wewe sote ni wachumia tumbo. Ila binadamu wengine wamezidi mno!. Yaani ruzuku yote ya chama kila mwezi inaenda kwenye tumbo moja kulipia madeni hewa yasiyoisha. It is just too much 'uchumia tumbo'!
Kimsingi hapa uelewa wa umma wa watanzania upo kwenye majaribio makali. Macho yangu yote kwao wakati nikisubiri kifuatacho.Siasa hii ya viongozi wengi wa chama cha upinzani kujiudhuru nyadhifa zao na kuhamia chama tawala zinafanyika katika nchi ya Tanzania pekee.
Siasa za namna hii kwanza zinaondoa imani ya wananchi kwa vyama vya upinzani.
Pia zinachangia sana wapigakura wengi kususia kupiga kura wakati wa uchaguzi.
Tena zinapunguza kura nyingi kwa wagombea wa upinzani.
Mwisho zinadhihirisha udhaifu wa vyama vya upinzani.
Kwa mwendo huu wa kujiudhuru udhuru na kuhamia hamia lengo la vyama vya upinzani la kuchukua dola halitafanikiwa katika muda unaotarajiwa.
Baadhi ya viongozi wa upinzani wanakosa heshima kwa jamii kwa tabia hii wanayoinesha.
Hapa si pa kuisingizia CCM bali pa kujutia.
Kama unanunulika wewe ni dhaifu, kama hujiamini wewe ni dhaifu, kama unakimbia matatizo ya chama badala ya kuyatatua ndani ya chama wewe ni dhaifu, kama una siasa za kuchumia tumbo wewe ni dhaifu tu. nk
Kwa ujumla upinzani wa Tanzania bado ni dhaifu sana.
Tunaupima udhaifu huo wa kusumbua wapiga kura wa upinzani toka enzi za TLP, NCCR, CUF na sasa CHADEMA.
Wananchi wanakosa chama cha kukiamini matokeo yake wengi hawapigi kura.
Siku Tanzania kikatokea chama cha upinzani imara na chenye viongozi makini, hakika kitachukua dola kiulaini kabisa.
Naomba usifanye haraka kuwalaumu wabunge, hawakuwa wanafanya hivyo kwenye tawala zilizopita, kuna jambo linafanyika nyuma ya pazia, either wanahongwa au wanatishiwa kwa namna moja ama nyingine.Ifike mahali hawa wabunge wawaheshimu wananchi waliowapa dhamana! Huku ni kutudharauna kuona hatuna la kuwafanya na hawaoni uchungu wa kodi zetu kurudia uchaguzi. Ushauri wangu, ni vema wananchi tuliowapa dhamana hawa wasaliti tukaamua kuwashughulikia na hata kuwafanya vilema! Tukiwafanya wawili au watatu na wakajua ni kwa nini wamefanyiwa huu upumbavu utakwisha, otherwise watatuchezea sana. Wapumbavu wakubwa.
Naomba usifanye haraka kuwalaumu wabunge, hawakuwa wanafanya hivyo kwenye tawala zilizopita, kuna jambo linafanyika nyuma ya pazia, either wanahongwa au wanatishiwa kwa namna moja ama nyingine.
Ni vyema kwa sasa kuwaacha tu waende, ila kamwe huwezi kuumaliza upinzani kwa kuchukua viongozi wa upinzani, unamaliza upinzani kwa kutatua shida za wananchi wa kawaida kitu ambacho CCM wameshindwa na hawatakuja kuweza. Tutabakia the least developed country in the world mpaka tushike adabu yetu.
Baada ya kuwachukua wabunge wote hao naomba CCM wafanye tathmini ya kiwango chao cha kupendwa na wananchi kwa kuruhusu mikutano ya kisiasa kwa siku moja hapa Dar, CCM wafanyie Jangwani na CHADEMA wafanyie kwenye viwanja vya mpira vya pale Chang'ombe, tuone huo mziki wake.Kwa lipi?. Tangu aondoke chama ndo kimeitisha dola mpaka jiwe anafanya unayoyaona na kuyasikia, Ujue CDM inaogopwa kuliko kipindi chochote. Mnasema CDM imekufa huku hamlali kwa mahangaiko ya kuidhoofisha kwa mbinu DHALIMU.
Wanafanya kila siku kupitia mwenyekiti wao na viongozi wengine, lakini pamoja na hayo hata tukifanya sample ya haraka humu JF, wapinzani ni wengi sana kuliko wafia chama.Kwani huyo kahama kwasababu ccm wanafanya mikutano ya kisiasa?
Talking loads of rubbish.Hakuna wanachama wakugombea huko lazima msubiri watakaotemwa CCM ndiyo muwachukue kugombea Chadema. Chadema ni SACCOS ya Mbowe na Mtei