Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Kuna haja ya wanazuoni wa kimataifa si hawa wa bongo kuja kuitafiti aina mpya ya siasa tunayoiendesha hapa tz ni kwa faida ya vizazi vijavyo..lakini tanzania ni ya pili kwa vivutio vya utalii duniani si mbaya kuongeza utalii wa siasa pia
Dunia kama kawaida yake itaangalia tu kama ilivyokuwa kwa Rwanda mwaka 94
 
Chadema ifanye kama mbeya, taarifa zikivuja tu jamaa anataka kuhama unafukuza mapema ili asipate umaarufu wa kisiasa. Huku kumwacha mtu hadi anaita waandishi wa habari ni kumpa mtu kiki. Labda kama wanafanya kusudi
 
Kwa nini iwe usiku na haraka hivyo?

Mie nilisubilia kesho kumbe zege halilali

CHADEMA mjifunze kupokea mizigo isiyo bebeka

Mkuu kila siku tunasema Mbowe alipokiingiza cdm 2015 alipaswa kujiuzulu kwani wote tuliona jinsi Shibuda alivyoisumbua cdm. Lakini kwa sababu zilizo nyuma ya pazia 2015 akampokea Lowassa na kundi lake na kuwapa nafasi nyeti za kugombea ndani ya chama na kuwaacha waliokipigania chama. Matokeo ya hayo maamuzi ya kutokujali kanuni leo ndio haiba ya chama inachafuka.

Kwa mwenendo huu, hakuna haja ya kupiga kura kabisa, kwani tuliowachagua cdm hatuwezi kuwapa kura ccm, na hao wanacdm tunawachagua tena kwa kuuza usalama wetu wanaweka maslahi yao binafsi. Hizi ni aina chafu kabisa ya siasa ndani ya nchi hii.
 
Mtu mwenyeuwezo mzuri wa kufikiri,hawezi kuinga mkono chadema hii
Ccm imefanya nn la maana, zaidi ya maisha kuwa magumu mitaani. Wakulima taabu, wafanyabiashara taabu ,wafanyakazi taabu, kundi pekee linaloweza kujidai ni wanasiasa tu na wanasiasa wenyewe wabunge na si madiwani kwa sababu madiwani wa halmashauri nyingi hawalipwi mishahara wala posho hii ni kwa sababu ya kushuka kwa mapato kwa halmashauri nyingi kunakotokana na kuporomoka kwa mitaji na tija katika biashara na kilimo .wanasiasa madiwani wanakiri haijawahi kutokea katika utawala wa kikwete kutolipwa. Posho wala mishahara kwa sababu halmashauri zilikuwa zinakusanya to the maximum , .Naongea kama mchumi mtafiti ninayejishughurisha na masuala ya maisha ya watu. Hizi siasa za kununuana zinawapa faida chadema kwa chaguzi za 2020, kwani makundi mengi yameshakata tamaa na huwezi pima kukubalika kwa ccm kwa chaguzi hizi ndogondogo ambazo ccm inatisha wasimamizi.mwaka 2020 ni uchaguzi nationalwide kitu hawataweza kutisha wasimamizi wote, kitu ambacho msimamizi gani ahatarishe maisha yake na familia yake kwa kuitetea ccm huku akijua fika kubadilisha matokeo kutampelekea ulemavu.tumesikia kwamba mwenyekiti ameziagiza kamati za siasa za wilaya zote kuanza kufanya vetting ya watumishi ambao ni wanaccm ili watumishi hao ndio wawe wasimamizi wa uchaguzi wa 2020, endeleeni kufanya hivyo ila mjue kwa nini wanasayansi huwa wanatumia wanyama na si binadamu katika tafiti zao,kwa sababu binadamu ni kigeugeu hasa akishajua unamchunguza, na taarifa zimeshaenea kwamba mnawachunguza, endeleeni na uchunguzi wenu majibu mtayapata 2020 zile 52.9% zitapungua hadi 49.0 % kwa sababu hao mnao wategemea kuwasaidia hawatawasaidia ,watawauza
 
Last edited:
Naomba kuwauliza wanaCCM,

Hivi Unajisikiaje unapoona mpinzani anahamia CCM halafu "anakaribishwa" na kiti cha uongozi?

Wewe MWANACCM uliye "kipigania" chama ukitegemea "mkono wa pongezi " unajisikiaje rohoni unapoona hili?

Wewe MWANACCM unayeshinda mitandaoni ukipiga propaganda za "kutetea chama" unajionaje kuona hali hii?

Mkuu uko sahihi kabisa, sasa ngoja msumeno ukate na upande wa pili, hivi walijisikiaje viongozi wa cdm waliokipigania chama kwa madhila yote kisha dakika za mwisho Mbowe akawapokea kundi la Lowasa na kuwapa nafasi za kugombea, huku akiwaacha waliokitumikia chama kwa uaminifu? Ni kweli chini ya Magufuli tunashuhudia siasa chafu za ushindani hapa nchini? Lakini kosa hili la Mbowe hatulioni?
 
Ila anaweza iunga mkono CCM ambayo kwa miaka 50 imeshindwa kututoa kwenye umaskini ilihali tuna rasilimali zote.....

Embu nipe sababu moja kwanni mtu ajiunge CCM?? hvi hta sera ya ujamaa kuna hata mmoja anaitekeleza ndani ya CCM nitajie hata mjamaa mmoja tu humo CCM.

Mkuu Zitto Jr nashukuru kukuona. Sasa hivi tunashuhudia siasa chafu za ushindani hapa nchini. Lakini mbali ya siasa hizi chafu uongozi wa cdm unabeba sehemu ya tatizo hili. Wakati wa uchaguzi 2010 cdm walimpa Shibuda nafasi ya kugombea ubunge dakika ya mwisho hatimaye akawa mbunge. Shibuda alichowafanya cdm wote tukujiapiza kuchukua hizo oil chafu dakika ya mwisho ni kosa kubwa.

Kwanini nasema kila siku muda wa Mbowe kuachia uenyekiti cdm umefika ni sasa. Kama uongozi haukujifunza kosa la Shibuda, 2015 ndio ikachukua kundi la Lowassa na kuwapa nafasi ya kugombea ndani ya chama. Je waliokipigania chama walijisikije na wanajisijiaje kwa hiki kinachoendelea sasa? Jaribu kuangalia 90% ya wanaorejea ccm ni wale waliokuja na mafuriko. Hivi katika mazingira ya kuhatarisha usalama wa kulinda kura za wapinzani ni nani atapiga kura tena ns kuzilinda huku wanaochaguliwa wanajitoa kirahisi hivi?

Uongozi wa cdm unapaswa kujitokeza na kuomba msamaha kwa kosa hili na ikibidi kujiuzulu ili kurejesha imani ya wananchi waliovunjwa moyo na hali hii. Kinyume na hapo mimi ninaendelea na kampeni yangu ya kuwataka wasioridhishwa na ushindani wa kisiasa uliopo nchini kutokupiga kura. Nitajitahidi kuhakikisha wapiga kura wanakuw wachache kuonyesha kwamba box la kura haliheshimiwi.
 
Sidhani kama kuna usahihi maana yule mlezi wake ni Lowassa. Hawezi kuhama hivi hivi maana Lowassa ataonekana ameshindwa kisiasa.
Kwahyo hii taarifa ni uzushi?
 
Unajisikiaje kuona mpinzani anahamia ccm na kupewa uongozi huku wewe kada mtiifu ukiachwa? Huoni kama kuna tatizo mahali?
Hawa wanaohama walikuwa ccm wakahamia chadema na wakapewa nafasi ya kugombea ubunge na wengine udiwani. Labda na wewe utuambie mlijiskiaje?
 
Tutafute dawa ya hawa majizi ya fedha zetu na udhalilishaji wa utu wetu, hakuna jambo la aibu, hasara na la kutia simanzi kama hama hama hii.
 
Siasa bana..
Mbunge / anahama chama kwa madai kwamba wabunge wa upinzani wanalazimishwa kupinga bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti alafu unahamia chama ambacho wabunge wanalazimishwa kupitisha bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti vilevile
Ndugu yangu, wanasiasa sana nyuso mbili mbili.
Leo kasema hilo na kesho amekanusha.
 
Sijui ni wananchi wangapi wanaohamia ccm kuwafuata hao wabunge walihamia ccm.Wanananch wanachokiona ni kuona pesa yao inatumika hovyo
 
Back
Top Bottom