Mbunge wa Jimbo lilipo daraja la Wami, msaidie huyu mama

Mbunge wa Jimbo lilipo daraja la Wami, msaidie huyu mama

Halina bima?

Hii ndio point ya msingi, na ndio tunapokosea baada ya watu kujifunza kufanya vitu systematically au kua na mifumo responsive mfano disaster mgt unit , wangapi wana matatizo zaidi yake au wanahitaji msaada hata wa matibabu tu waokoe uhai?

Alafu mbunge ana special funds za ku accomodate vitu kama hivyo?? Au atoe wapi hizo hela ??
 
Ni uzembe, na hatutakiwi kulelea uzembe. Kwanza nilidhani magari makubww ni lazima ya na comprehensive insurance kabla hayajaingizwa bara barani, hiyo ingecover mwenye gari, mwenye mzigo na dereva.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama kwel mpambanaji,..kumiliki scania sio Kaz ndogo...Mimi tu hapa nimeshindwa kumiliki hata IST..mungu azid kumsaidia huyu Mama..
 
Kuna wakati wabunge sijui wanawaza nini hawajui kujichanganya na matatizo japo madogo tu ya wananchi , tarehe 5 mwezi huu , katika daraja la mto wami lori lilitumbukia mtoni na dereva wake , dereva alifanikiwa kutolewa na wataalam wa kuogelea , lakini lori bado mpaka leo lipo ndani ya maji , kwa mujibu wa mmililiki wa lori Mama mmoja ambaye ni mzee kwa kweli gari hili alilinunua baada ya kudunduliza hela zake na kupata kiasi cha milioni 18 akaamua kununua hilo gari ikiwa ndio safari yake ya kwanza likapata ajali , toka ajali itokee yule mama kapiga kambi pale wami akiomba msaada , mpaka jana kiasi cha milioni mbili kilichangwa na wamama ili kumsaidia , na zinaitajika kiasi cha milioni tano ili kutoa lori hilo katika mto.

NIMSHAURI MBUNGE WA ENEO HILO FANYA JAMBO KUMSAIDIA HUYO MAMA HATA KAMA SIO MPIGA KURA WAKO , ILA AJALI IMETOKEA KATIKA ENEO LAKO.
Milioni 83,000,000/= Tshs.ndio hela alionunulia gari hilo.
 
Third party, analipwa uliyemsababishia ajali mwenye gari tengeneza mwenyewe.
... ni uzembe wake mwenyewe. Kwa chombo muhimu kama kile na alichokitoklea jasho jingi (TZS 83 m/-) hakupaswa kukiweka barabarani kizembe namna ile bila kuwa na bima ya kueleweka. Anyway, yaliyotokea yametokea hakuna namna ya kurudisha muda nyuma; kuna wawili watatu wataelimika kutokana na tukio hili.
 
Bei ya hiyo comprehensive inazidi faida atakayoipata kwenye biashara Yake mwaka mzima labda.
Hapana mkuu, usiwakatishe tamaa wamiliki. Bahati mbaya sijaona hapa likitajwa aina ya gari na lilikuwa na umri gani pengine wataalamu wangesema ni wastani was kiasi gani ingelipiwa.
Bado bima sio za juu sana kulingana na maumivu ya ajali au kwenye nyumba moto
 
Ndio nasikia leo kwamba comp ni kwa baadhi ya magari.
Upo sahihi. Siyo kila gari inakatiwa Comp.
Ile gari niliona No. Zake ni A...

Na kukatia Comp. Gari mwisho miaka kumi baada ya kuingia Nchini hii Ni kwa mujibu wa Sheria za TIRA.. Ukipewa Comp. Na Kampuni yoyote ya Bima baada ya huo muda hiyo wameamua kuvunja tu sheria..

Sasa ukijiuliza ile gari inazaidi ya miaka 10.. hiyo Namba A ni ya kitambo sana.. Namba C sidhani kama anapewa Comprehensive..
 
MCHANGIE MAMA HUYU KULIOPOA GARI MTO WAMI
(SCANIA 113 - 360hp) Semi Teller.

Hii ni Moja wapo ya ajali mbaya miongoni Mwa ajali zilizo wai kutokea kwenye mto wami.

CHANZO CHA AJARI NIKUPOTEZA BREKI.
Mashuhuda waajali wanasema waliona loli linakuja kwa mwendo wa kasi sana, na dereva huyu Frank (Marehemu) alikua ameshafanikiwa kulenga katikati ya daraja.

Mbele ya loli lililotumbukia kulikuwa kuna gari imetangulia, ikasimama ghafla sasa kwa kua daraja hili nijembamba huyu dereva waloli alipojaribu kumkwepa ndipo loli likaingia mtoni.

GARI HILI NDIO LILIKUA LIMEANZA KAZI, NA HII NDIO ILIKUA SAFARI YAKE YA KWANZA.
Bahati mbaya Gari ndio likatumbukia mtoni.

MMILIKI WA LOLI HILI.
Mmiliki wa loli hili ni Mwana Mama mjasiliamali, anaitwa MWAJUMA SHAIBU mkazi mbezi mwisho.
Mama huyu anakitu cha kutufundisha.

Miaka 9 iliopita Mama huyu alisikia kuna loli lina uzwa milioni 15, akaenda kulinunua, akaanza kulitengeneza kidogo kidogo;

Alikua anatoa spea ya zamani na kufunga mpya, alipo kamilisha kulitengeneza,
Akaanza kubandika dukani tairi Moja Moja,hadi yalipo kamilika mataili 16 na spea Moja la 17.
Amesha tumia milioni 83 kulitengeneza na kuliingiza barabarani.

HUYU NDIE MWANAMKE SHUPAVU,
Sio kazi raisi kwa mwanamke kumiliki SCANIA 113-360hp kwa mtindo alioutumia huyu Mama.

KWANINI BIMA ISIMSAIDIE?
Baati mbaya alikata bima ndogo, akasema ikipiga ruti mwezi Mmoja atakata bima kubwa, matokeo yake ruti ya kwanza tu Gari imetumbukia mtoni.

KULIOPOA GARI MTONI NI MIL 5.
Nimpongeze Mkuu wa kituo wami, Jeshi lawananchi, ambao wamekua jirani na huyu Mama tokea ajali imetokea niwiki sasa.

SHUKURANI KWA WAFUATAO:
Justina Mutafungwa (Mke wa RPC morogoro anaesimamia mtandao wa wanawake kusaidina; na HILDA KISOKA mkurugenzi wa PAPO Planet, ambao wamemchangia huyu Mwanamke mwenzao Milioni 2.

Mh Rais wetu J.P.Magufuli, Mh J.Ndungai na wabunge wako,Mawaziri, naomba mumchangi eni huyu mama aopoe Gari:

Namba: 0788 62 42 30.
Jina: MWAJUMA SHAIBU.

Mgideoni:
Richard Yohanan Sanga.Richard Yohanan Sanga
 
Kuna kahela kangu kameingia kwenye hiyo namba ila sipati feedback toka juzi[emoji848]
 
Back
Top Bottom