Kwanza ninashangaa mtu mwenye akili zako kamili unashabikia kuingia garama za kurudia uchaguzi majimbo ambayo yana wabunge na ni wabunge hao hao watakao kwenda kugombea tena, hivi ni nani aliwaloga watanzania mbona wenzetu hapa Kenya tu jirani na sisi wako tofauti kabisa kimawazo tunatatizo gani sisi? Sasa kwanini tusiwe masikini milele kama ndo vitu tunavyoona vya kushabikia hivyo. Mtanzania tena mlipa kodi unanufaika vipi mbunge akiacha jimbo lake na kuchaguliwa tena katika jimbo hilohilo. Mbona mi siyo mwanasiasa lakini naumia sana kodi ninayolipa halafu inatumika kwenye hayo mambo. Sijui tunapata wapi ujasiri wa kushabikia mambo yanayotutia umaskini mi binafisi hivyo vitendo sioni tofauti na uhujumu uchumi kwakweli. Kama Mbunge anajihuzulu aache huo ubunge asigombee tena lakini leo anaacha kesho anaomba kuchaguliwa awe Mbunge wa jimbo hilohilo, hapana kwakweli huko ni kutuletea umaskini kwa makusudi. Hata kujitegemea nchi haijaweza inategemea misaada halafu kidogo tunachopata kinachezewa kwenye hizo chaguzi za marudio. Mungu iokoe nchi yangu isiangamie.