Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM) mbaroni kwa kukutwa na Silaha 16 na risasi 536

Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM) mbaroni kwa kukutwa na Silaha 16 na risasi 536

Kwa wana-CCM kukutwa na vitu haramu katu haiwezi kuwa habari!

Hiyo ni taarifa tu kwamba "Ndugu Watanzania, Mhalifu mwingine kutoka CCM Gang Unit limebambwa likiwa na bunduki za kufanyia ujangili kama ilivyo ada ya wahalifu wengine wengi kutoka genge hilo. Ndugu Watanzania, tunajua kwamba mnajua ila tunawakumbusha tu kwamba CCM Gang Unit ni moja ya magenge hatari sana kwa uhalifu barani Afrika"

Hiyo haiwezi kuwa habari... ni taarifa tu, and thank you Mleta mada kwa kutupa taarifa!
 
Mimi nilidhani Wabunge wanaoonekana hawafai ni wa Upinzani pekee na CCM wote ni Malaika kumbe hata Kwao kuna Vitimbi?
Huyo wanajua siku nyingi kuwa ni jangili lakini analindwa na system kwani ndio wafadhili wa CCM.
Ukiona hivyo ujue CCM imepata mtu mwingine wa kumpa Ubunge hivyo lazima wamuondoe kwa maovu wayajuayo.
Style ya CCM ni kuwalinda wafadhili hata wawe wanakula nyama za watu, lakini siku wakikuchoka na kutaka kumpa kiti hicho mwingine basi lazima wakufanyizie tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ajabu sasa jambo kubwa kama hili litaishia kimya kimya kiushikajishikaji.
 
Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mh. Suleiman Masoud Nchambi kwa tuhuma za kumiliki silaha zisizo halali na kukutwa na nyara za serikali zilizopatikana kwa kufanya uwindaji haramu.

Yaani ukiona mtu ana sifu sana jua kuna kitu ana faidi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii sasa m
View attachment 1441653

Polisi mkoani Shinyanga wanamshikilia Mbunge wa Kishapu (CCM) Suleiman Nchambi kwa tuhuma za kukutwa na silaha 16, risasi 536 pamoja na nyara za Serikali
==

Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Suleiman Masoud Suleiman maarufu Suleiman Nchambi (CCM) kwa tuhuma za kupatikana na silaha 10, risasi 536 na nyama zinazodhaniwa kuwa ni za wanyawapori kinyume cha sheria.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Mei 6,2020, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Mei 3,2020 majira ya saa sita kasoro usiku katika mtaa wa Lubaga kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

“Mei 3,2020 majira ya sita kasoro usiku Kikosi kazi cha askari wa upelelezi kikiongozwa na Kaimu Mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi kwa kushirikiana na Afisa wa Wanyamapori mkoa wa Shinyanga Perfect Mbwambo walifanya upekuzi kwenye makazi ya Mbunge wa Jimbo la Kishapu baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kuwa Mheshimiwa huyo alikuwa akifanya uwindaji haramu kwenye eneo la Negezi wilayani Kishapu akiwa na gari yenye namba za ujasili T760 DSD Nissan Hard Body”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

“Katika upekuzi huo walifanikiwa kukamata nyama iliyodhaniwa kuwa ni wanyamapori yenye uzito wa kilogramu 35 zikiwa zimehifadhiwa kwenye jokofu lililokuwa jikoni,jingine sehemu ya mazoezi na nyama nyingine ilikutwa kwenye gari hilo likiwa limeegeshwa nyumbani kwake ndani ya uzio wa nyumba hiyo”,amesema Kamanda Magiligimba.

“Katika gari hilo kulikutwa silaha moja aina ya shortgunWakati askari hao wakiendelea na upekuzi ndani ya chumba chake cha kulala zilipatikana silaha zingine za aina mbalimbali na kufanya jumla ya silaha zilizokamatwa kuwa 16 ambazo ni Airgun 3, Shortgun 3,Rifle 8, Pistol 1 na Mark IV 1 pamoja na risasi 536 zikiwa kwenye kabati la nguo",anaeleza Kamanda.

“Baada ya uchunguzi wa awali iligundulika kuwa silaha 10 ambazo ni Airgun 2, Rifle 5, Shortgun 2 na Mark IV 1 kati ya 16 anazimiliki isivyo halali”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

Kamanda Magiligimba amesema nyama hizo zimepelekwa maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi na gari husika limekamatwa.

“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. Natoa onyo kali kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo vya kumiliki silaha isivyo kihalali hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”,amesema Kamanda Magiligimba.


Hii sasa ni aibu , wenzake wako bungeni , wengine wako karantini kimya kimya au wazi ,yeye yuko anawinda , lile tamko la Mwigulu na la Makonda leo kwa wabunge ambao hawako bungeni linawahusu wazembe na wahujumu uchumi kama hawa>??

Au huyu anataka kuunda jeshi la Interehamwe kama analolihubiri Gwajima ?
 
Kawafanya nn tena wakubwa was nchi tena
 
Baadhi ya Wabunge wapo CCM kwa ajili ya kuficha uhalifu wao

Hiyo ni ya miaka na miaka mingi mno basi tu
 
Plea bargain! Si kama ya nduguye King Maker tu? Atalipa na kisha kuachiwa. Habari imekwisha.
 
Back
Top Bottom