Serikali haiwezi kufidia Watu wasio na umiliki. Mali zao ni ngombe na hakuna MTU aliyezichukua. Hakuna Watu WENYE ardhi isiyo na mipaka...
Honestly, hata sijaelewa hoja yako specific ni nini..
Lakini, haijalishi. Labda nikuulize swali hili moja..
Kwani, wewe kwenu ambako ni asili yako na wazazi wako ni wapi kwani ndugu
1000 digits?
Hebu tuashumu, ni kule Peramiho kata ya Mtogo ambako wazazi wako na vizazi vyao vimekuwapo...
Sasa, hebu jaribu kujibu swali hili ukitumia dhamira safi ya nafsi na moyo wako pasipo kujidhulumu mwenyewe..
Kwamba, itokee sasa serikali inaamua kuja kunyang'anya ardhi wananchi wote wa kijiji chako na vya jirani eneo lenye ukubwa wa zaidi ya 16,000km² bila kuwashirikisha, bila kukubaliana nao eti tu kwa sababu iliyoamua ni serikali...
How would you feel..? Wananchi hao ndugu zako wangefanyeje unadhani?
Hiki ndicho kinachotokea huko Loliondo na Ngorongoro...!!
Nakushangaa tu unavyowalauumu hao Wamasai na kuwapa kila aina ya majina mabaya eti tu kwa sababu hawakaribishwi watu wengine kwenye ardhi yao..
Sasa, utawezaje kumpangia mtu namna ya kuishi ktk eneo lake binafsi? Hiyo ni ardhi yao, wamezaliwa hapo tangu vizazi na vizazi. Wanalinda mila, desturi na utamaduni wao ikiwemo kutouza ardhi kwa wageni...
Leo serikali eti inataka iwatoe wamasai ktk ardhi yao ya asili ili imuuzie mtu toka taifa jingine kwa jina la "mwekezaji". Hiyo ni ngumu, haikubaliki. Kama ni hilo dude uliitalo "serikali" kushikwa sharubu, sasa hakika litshikwa na lazima litulie kwa sababu nguvu ya umma ni kuu kuliko kikundi kidogo cha watu kinachoitwa "serikali"...!