Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ajiuzulu nafasi ya Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni

JokaKuu,
Hayo ndo maoni ya Mbowe? Kama ndiyo basi, kichwa kiko tupu. Kwani kukaimu hakuhitaji utambulisho rasmi? Unaweza kukaimisha mtu bnafasi bila maelezo yoyote rasmi?

CHADEMA ni biashara! Hii ndo inatuharibuia vyama vya upinzani. Wengi wanaviongoza ili kujinufaisha na ndiyo maana sioni kama Mbowe ni mtu aliyestahili kuendelea na siasa. Kwa kuwa anawinda ruzuku, na anapewa ushabiki, aendelee lakini wanaoing'ang'ania CHADEMA mwisho unaonekana.
 
ukiwa upinzani unatafuta perfection ili utengeneze uhalali wa kuisema ubovu wa ccm.

Hoja kuu hoja ndogo ama dhambi ndogo ama dhambi kuu sio tatizo.

Hilo la uchaga limezoeleka sio hoja tena bali ndio uhalisia
Una hoja za hapa na pale, lakini hoja kuu hapa mnaikosa maana angekuwa mtu mwingine mngesema kwakuwa sio mchaga. Kwa bahati mbaya hayo yamemkuta mchanga, hivyo hoja yenu kuu inakosa nguvu so inabidi muokoteze sababu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukiwa upinzani unatafuta perfection ili utengeneze uhalali wa kuisema ubovu wa ccm.

Hoja kuu hoja ndogo ama dhambi ndogo ama dhambi kuu sio tatizo.

Hilo la uchaga limezoeleka sio hoja tena bali ndio uhalisia

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa hiyo perfection inakosekana kwa kutomdhibitisha hiyo Selasini kama mnadhimu? Kwa maneno mengine cdm itakuwa perfect kwa 30 kudhibitishwa na Mbowe kuwa ni mnadhimu, na hapo ndio itapata uhalali wa kuisema ccm? Kwani madhambi ya ccm yanasemwa iwapo tu cdm itakuwa perfect? Kimsingi hilo la uchaga ndio hiyo yenu kuu, ila hapa imekosekana ndio maana mmeishia kuukoteza maneno.
 
Ahsante kwa ku declare mwenyewe kuwa wabunge wenu ni unfit huko majimboni kwenu

Nitajie majimbo matatu tu ya wabunge wa ccm ambao ni fit na kwasasa kila kitu wameshatatua huko majimboni mwao, na hapo walipo wanasubiri tu uchaguzi. Tena usiende mbali taja ubora wa maisha ya jimbo la Magufuli na Kalemani, kisha tufananishe na maisha ya wananchi huko anakotokea Selasini.
 
..amemkaimisha.

..maana yake ni kwamba Mbowe bado anamtambua TL kama mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni.

..Mbowe akimthibitisha Selasini atakuwa anahalalisha kuwa ni sahihi TL kuvuliwa ubunge, na pia ni halali alivyopigwa risasi.
Kwani TL ni mbunge tena? Unasemaje bado anamtambua TL? Tumia akili zako kidogo tu utajitambua!
 
Chaguzi zote hapa nchini zinafanywa kwa uhuru na haki, mnashindwa kutekeleza ahadi zenu majimboni mnakosa wabunge mnasingizia hakuna haki kwenye uchaguzi CHADEMA mna safari ndefu sana sana tuu

Hatusingizii chochote ni vitu vilivyo wazi. Kwa macho yangu nimewaona polisi wakiwapiga mawakala wa upinzani ili kusaini matokeo fake ya uchaguzi ili ccm watangazwe washindi.

Kwa macho yetu tuliona kupitia kituo cha ITV maboxi ya kura yakitolewa vituoni kwenda kujazwa kura za CCM, haya yalifanyika mbele ya polisi na tume ya uchaguzi, na bado ndani ya huo ushenzi na uhayawani wa wazi, tume ya uchaguzi ilimtangaza mshindi wa CCM.

Ushenzi huo ndio ulichangia wananchi wengi kususia kujiandikisha kupiga kura uchaguzi SM. Huo ushenzi ndani ya chaguzi zetu unafanyika mbele ya macho ya watanzania na wanayaona.
 
Hakupewa barua ya kukaimu yeye anawezaje kuandika barua ya kujiuzulu, barua moja hujibiwa na barua nyingine ki ofisi kwa Reference. Mbunge alitakiwa amuone Mbowe ana kwa ana ajiuzulu kwa maneno ya mdomoni ili Mbowe sasa atengue uteuzi wa Joseph kwa maneno na amteue mwingine kwa barua au ateue kwa mdomo kama ndio utaratibu.
 
..upinzani na CDM ni zaidi ya Mbowe unayemchukia.

..uchaguzi mkuu wa cdm umefanyika mwezi uliopita wewe tayari unatabiri na kuwaombea viongozi waliochaguliwa wafeli.
Simchukii Mbowe hata kidogo nina tatizo na jinsi Chadema inavyoendeshwa. Tatizo kubwa ni watu kama nyie ambao mnafaidika na utawala wake. Nafikiri baada ya kibano 2020 then tutajua kama mnaipenda Chadema au mnapenda Mbowe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye kufaidi viti maalumu nimecheka sana aisee
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…