Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya(CHADEMA) ajiuzulu Ubunge na kujivua uanachama, ahamia CCM

Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya(CHADEMA) ajiuzulu Ubunge na kujivua uanachama, ahamia CCM

Kiongizi wa kuchaguliwa akikubali kununuliwa kwa pesa na siyo kwa kura, ni wazi akipewa madaraka makubwa atanunuliwa tena. Moja kwa moja kiongozi wa aina hiyo ni
Fisadi Papa , na chama chake cha siasa akifai kuaminiwa
chama kinahusika vipi sasa hapo?
kwani chama kizima kimenunuliwa? mbona kuna watu wana madaraka makubwa kwenye vyama na waliiba nyumba za serikali!!!!
 
Nani awakabidhi nchi ikiwa hata ofisi ya makao makuu inawashinda ,chama kikuu cha upinzani kimepangishwa kwenye pagala la mwenyekiti wenu toka kimeanzishwa,mikoani kimepangishwa kwenye nyumba za wachaga,hii ni tope
Hivi wakati Nyerere anakabidhiwa nchi na mwingireza, ofisi za Tanu zilikuwa wapi mkuu?
 
Mimi naona waende wote tu, nchi ibaki chini ya chama kimoja. Nadhani tutashika adabu
 
Ni haki yake kuhamia anapotaka. Anasema aliacha siasa za majukwaani kwa miaka hii mitatu (alikimbia majukumu ya kuwawakilisha wananchi). Ni vyema amejiuzulu kwa kuwa ni wazi kuwa tangu awali alikimbilia Chadema kutafuta fursa na siyo kuwatumikia wananchi.

Amechelewa sana kuelewa kuwa huku Chadema ni kugumu mno na waliopo ni wale waliojitoa kuifanya kazi ngumu (ya kuweka misingi mipya) ambayo yeye hana huo utayari.

Badala ya kumlaumu nadhani ni vyema kumpongeza kwa kujitambua kuwa aliwapotezea wananchi fursa za kupata maendeleo waliyoyatamani tangu mwanzo. Aombe tu msamaha kwa kuwapotezea wananchi waliompa dhamana muda wa miaka mitatu.
Mlivokua mnamteua kugombea 2015 hamkujua kua hafai? Au kwakua amehamia upande wa pili? Kubalini tu kuwa ndani ya CDM kunatatizo mkijifanya vichwa ngumu watakwisha wote na mtakua kama NCCR mageuzi. Hapa namuona zito kabwe na ACT akiibuka huko mbereni.
 
Nimegundua.ukiwawaza sana wanasiasa wana weza kukuumiza akili.kikubwa tafuta ugali wa watoto wako.
kumbuka zaidi ya 80‰ ya watanzania ni maskini au wanyonge Kwa lugha ya awamu ya tano
 
Ngoja tuone kama tambiko la kimasai litafanya kazi..alipojiunga na Chadema alifanyiwa tambiko.
 
Duh haya maisha ya kuamini wanasiasa yatawaua...Leo hii hata EDWARD LOWASA akirudi CCM wale wa huku watasema hivi hawa wa kule watasema hivi...acheni kufanywa watumwa wakifikra
 
uhakika wa ubunge anao ata asipochaguliwa na wanainchi upo rushwa kapewa. anashida gani??

kwa akili hizi Tanzania kuendelea itachukua muda mrefu sana.

Hawa ndio wale 'marayamaraya' wa siasa. Baada ya kuona muziki wa Ole Sendeka hauwezi akawatumia Chadema kuukwaa ubunge. Sasa karudi tena CCM. Huu ni umalaya!!!!! Mamluki, ndumilakuwili, unpredictable and above all, unpatriotic.
 
Unajipa matumaini ambayo hayapo.

Tunajua kuna mtu ameapa kuangamiza upinzani ila ajue atashindwa tu katika hizi hujuma zake.

Naona umeanza kuwa humble.

Kwani kuna tatizo ndani ya Chadema kupelekea wanachama mahiri kama wabunge kuhama?

Naamini idadi ya wabunge in direct relationship na ruzuku. Mpaka sasa Chadema imepoteza wabunge wangapi na ruzuku ime/itaathirika vipi?

Je ni hatua gani au mkakati wowote Chadema imezichukua kuhakikidha wabunge waliobaki hawajiuzulu na kujivua uanachama?
 
Back
Top Bottom