Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya(CHADEMA) ajiuzulu Ubunge na kujivua uanachama, ahamia CCM

Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya(CHADEMA) ajiuzulu Ubunge na kujivua uanachama, ahamia CCM

Kila siku anakula bakora na muheshimiwa Olesendeka kwenye vikao vya legwanani kwann asihame. Kule simanjiro hakuna uhuni uhuni kama walendavyo CDM. ukileta mbwembwe za kihuni unaitwa mbele ya wazee unakula mboko. Jamaa akaamua kukimbia baada ya kuona aliko kunamsababishia maumivu kila akikutana na legwananis kule orkesment, Naberera, Landanai, Merenani nk.
 
....tarehe za uchaguzi kwa majimbo yaliyoko wazi kwani linii...tuambizanee
 
Nilibahatika kuwa Arusha siku Milya anatangazwa rasmi kuhamia cdm katika mkutano mkubwa sana pale NMC nakumbuka aliitwa mzee wa mila akamfanyia kiapo kwamba haitakuja kutokea arudi ccm. Sijui nini kimetokea.
 
Wacha waende sisi tupo hadi tamati
Naona umeanza kuwa humble.

Kwani kuna tatizo ndani ya Chadema kupelekea wanachama mahiri kama wabunge kuhama?

Naamini idadi ya wabunge in direct relationship na ruzuku. Mpaka sasa Chadema imepoteza wabunge wangapi na ruzuku ime/itaathirika vipi?

Je ni hatua gani au mkakati wowote Chadema imezichukua kuhakikidha wabunge waliobaki hawajiuzulu na kujivua uanachama?
 
Mmh!! huyu alishawahi kuwa na cheo cha juu cha ccm mkoani Arusha upande wa vijana? asee hata sasa kuna wazee wa3 siwaamini pale cdm siwaamini.
 
Hongera sana mwenyekiti wa zamani wa UVCCM mkoa wa Arusha, umechukua uamuzi sahihi kabisa. Nilijua huwezi kukaa na genge la wapiga deal, genge la wahuni. Karibu Sana nyumbani mshale ukienda porini haujapotea ndio nyumbani kwake. Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
 
Biashara inaendele!!

Wahame tu ila wananchi tuko na CHADEMA/upinzani maaana CCM na Magufuli hawana msaada kwetu.

Maisha ya mtanzania sio ndege, flyover, Chato Airport, banadari ya Chato, n.k, bali ni pamoja na bei nzuri ya mazao ya wakulima, ajira, mishahara na masilahi bora kwa watumishi, uhuru wa maoni, mikopo elimu ya juu bila ubaguzi, elimu bora ni si bora elimu, kodi rafiki kwa wafanyabiashara, n.k.

Maisha ya mtanzania ni watoto kutokusoma shule za nyasi na kukaa kwenye vumbi, watanzania kuto-share maji na mifugo,bei za bidhaa kutopanda, watanzania kutopoteza ajira kwasababu biashara zinakufa na makampuni kufungwa au kuyumba, n.k.

Watanzania hatutaki mtu asietaka kukosolewa, anaetuletea sheria za kutuziba midomo mfano sheria ya takwimu, kiongozi asiethamini demokrasia na asieheshimu maamuzi ya wapiga kura.kiongozi anaevunja katiba na sheria za nchi tena wazi wazi.

Watanzania hatuhitaji mtu asie na kauli za staha ambae anaweza kuongeoa lolote na mahali popote.

Waendelee kuwalipia madeni na mikopo kama inavyodaiwa ila wasitake kutuhadaa kisa matumbo yao.

Never ever hatutadanganyika na haya maigizo yenu na huyo mnaemsujudia.

Kibaya zaidi hakuna mnacho-achieve, sana sana mnazidi kuiogopa CHADEMA na kuona sanduku la kura kama mtihani uliowashinda katika maisha yenu!

CCM hii ni ndoto kubadili maisha ya watanzania kwani miundombinu pekee sio muarobaini wa unafuu wa maisha ya mtanzania.

Hakuna nchi ilioendelea kwa wabunge au madiwani kujiuzulu na kumuunga mkono Raisi alie madarakani na kusababisha nchi kuingia gharama kubwa za marudio ya uchaguzi kila kukicha.Hakuna.

Mnatutia aibu watanzania!

Poor you!

Nyinyi ndio wale mwalimu aliwaita mercenaries.
Ni kweli unacho kisema
 
Duh haya maisha ya kuamini wanasiasa yatawaua...Leo hii hata EDWARD LOWASA akirudi CCM wale wa huku watasema hivi hawa wahuku watasema hivi...acheni kufanywa watumwa wakifikra
Kiswahili kizuri ungeandika "hawa wa huku watasema hivi na wale wa kule watasema vile" Sasa wewe umeandika wote ni wa huku na wote watasema hivi. Yaani hawana tofauti ya location, wote ni huku na pia hakuna tofauti ya watakachosema, wote ni hivi. Lugha ikiandikwa au kusemwa vizuri, hufikisha ujumbe vizuri zaidi.
 
Muheshimiwa LOWASSA na SUMAYE hakikisheni mmemaliza kazi yenu vizuri kabla hamjarudi nyumbani,muda bado ,mpaka July 2019
Hakika kazi wameifanya vizuri tena kwa ustadi wa hali ya juu. Wanastahili pongezi bila kumsahau mratibu Mbowe. Sasa wanaweza kurudi nyumbani vifua mbele!
 
Hakika kazi wameifanya vizuri tena kwa ustadi wa hali ya juu. Wanastahili pongezi bila kumsahau mratibu Mbowe. Sasa wanaweza kurudi nyumbani vifua mbele!
Bado kidogo tu mkuu,tupiga finishing ya mwisho[emoji23]
 
Mlivokua mnamteua kugombea 2015 hamkujua kua hafai? Au kwakua amehamia upande wa pili? Kubalini tu kuwa ndani ya CDM kunatatizo mkijifanya vichwa ngumu watakwisha wote na mtakua kama NCCR mageuzi. Hapa namuona zito kabwe na ACT akiibuka huko mbereni.

Waliohamia upinzani kutafuta fursa lazima warudi tu walikotoka. Upinzani ni dhana ya mabadiliko na siyo fursa. Fursa zipo CCM. Chadema ni nguvu ya uma. Haiwezi kufa kamwe. Labda siku hii nchi ikose watu. Duniani tunaishi watu, siyo malaika.
 
Biashara inaendele!!

Wahame tu ila wananchi tuko na CHADEMA/upinzani maaana CCM na Magufuli hawana msaada kwetu.

Maisha ya mtanzania sio ndege, flyover, Chato Airport, banadari ya Chato, n.k, bali ni pamoja na bei nzuri ya mazao ya wakulima, ajira, mishahara na masilahi bora kwa watumishi, uhuru wa maoni, mikopo elimu ya juu bila ubaguzi, elimu bora ni si bora elimu, kodi rafiki kwa wafanyabiashara, n.k.

Maisha ya mtanzania ni watoto kutokusoma shule za nyasi na kukaa kwenye vumbi, watanzania kuto-share maji na mifugo,bei za bidhaa kutopanda, watanzania kutopoteza ajira kwasababu biashara zinakufa na makampuni kufungwa au kuyumba, n.k.

Watanzania hatutaki mtu asietaka kukosolewa, anaetuletea sheria za kutuziba midomo mfano sheria ya takwimu, kiongozi asiethamini demokrasia na asieheshimu maamuzi ya wapiga kura.kiongozi anaevunja katiba na sheria za nchi tena wazi wazi.

Watanzania hatuhitaji mtu asie na kauli za staha ambae anaweza kuongeoa lolote na mahali popote.

Waendelee kuwalipia madeni na mikopo kama inavyodaiwa ila wasitake kutuhadaa kisa matumbo yao.

Never ever hatutadanganyika na haya maigizo yenu na huyo mnaemsujudia.

Kibaya zaidi hakuna mnacho-achieve, sana sana mnazidi kuiogopa CHADEMA na kuona sanduku la kura kama mtihani uliowashinda katika maisha yenu!

CCM hii ni ndoto kubadili maisha ya watanzania kwani miundombinu pekee sio muarobaini wa unafuu wa maisha ya mtanzania.

Hakuna nchi ilioendelea kwa wabunge au madiwani kujiuzulu na kumuunga mkono Raisi alie madarakani na kusababisha nchi kuingia gharama kubwa za marudio ya uchaguzi kila kukicha.Hakuna.

Mnatutia aibu watanzania!

Poor you!

Nyinyi ndio wale mwalimu aliwaita mercenaries.
amehama na wanachama wangapi
 
Mlivokua mnamteua kugombea 2015 hamkujua kua hafai? Au kwakua amehamia upande wa pili? Kubalini tu kuwa ndani ya CDM kunatatizo mkijifanya vichwa ngumu watakwisha wote na mtakua kama NCCR mageuzi. Hapa namuona zito kabwe na ACT akiibuka huko mbereni.
Kwani hamjamuelewa mwalimu JKN?Hawa ni malaya malaya tu!
 
Hivi polepole amesharudi kutoka Ethiopia nasikia kakiwakilisha chama vizuri kwa kutoa hotuba nzuri ya kiingereza
IMG-20181007-WA0037.jpg
 
Kwa nini? Kwani wanaohama ni wabunge wao wewe baada ya kusema chadema wajitafakari unasema Ccm kweli duniani kuna watu na viatu
Sababu zangu 1;ccm wakiwakatalia hao wahamiaj hakutakua na chaguzi na matumiz mabov ya pesa kweny uchaguzi,wanapaswa kuzionea huruma pesa za watanzania,,,,,2;huwezi kuwa mtu wa kupokea kila mpinzan anaekuja kwako halafu unampa nafasi tena huyohuyo ,anapaswa kukaa bench kujifunza na kuwapisha wengine,,,,,ccm wajitafakari upya hapa
 
Back
Top Bottom