Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(CHADEMA) ajiuzulu na kuhamia CCM

Awe amenunuliwa au vyovyote tutakavyomuita lakini kitu kimoja ambacho ni hakika ni Chadema inaenda kubaya. Tuache kuimbiana mapambio tuseme ukweli otherwise naiona NCCR mpya za zama hizi! Mkapa aliivyonza NCCR na sasa naona mzee baba anafanya the same to Chadema. Vyovyote vile haya yanayotokea CCM si ya kulaumiwa bali Chadema yenyewe, acheni kutafuta mchawi.

Mlichomfanya Dr Slaa 2015 wengine tuliandika hadi vidole vikauma lakini tuliona shimo ambalo wengine kwa mihemuko hawakuona. Msijipe moyo, tubuni makossa ili muanze upya na kujenga upya uaminifu ambao unapaswa kuanzia kwa viongozi wenyewe.
Tusimung'unye maneno mpango ni kuua upinzani na sasa wapinzani wanaohama vyama vyao ndo hawa wanateuliwa kuingia serikalini. Waliobaki ndio hawa wenye kesi za uchochezi. Kwa sasa ni kuchagua kubaki upinzani upate tabu au hamia ccm upate cheo.
 
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Mwikwabe Waitara, atangaza kuniuzulu CHADEMA na kuhamia CCM. Kajiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

> Asema sababu ni kutofautiana na viongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA baada ya kuhoji kuhusu matumzi ya luzuku pamoja na demokrasia ndani ya chama

> Ameeleza kuwa alihoji matumizi ya Milioni 237 za ruzuku kwani mpaka sasa CHADEMA haina Ofisi Kuu, ya Kanda wala Mkoa

> Mwenge wa Uhuru umekuja kuzindua miradi ya maendeleo niliyoipigania lakini naambiwa usiende pale na mimi shida yangu haikuwa CCM pale ilikuwa ni mradi niliopigania

"Leo nimejiondoa rasmi CHADEMA kwahiyo mimi sio Mbunge tena, nimetupa jongoo na mti wake" amesema Mwita Waitara

“Mimi nataka niende mahali ambako kuna kazi za kufanya,” Waitara amewaambia waandishi na kuongeza kwamba anatamani kuwa Waziri Kamili.

Habari zaidi....

Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara amejiuzulu uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM leo Jumamosi Julai 28, 2018.

Waitara ametangaza uamuzi wake huo leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi ndogo za CCM Lumumba mjini hapa, akiwa sambamba na katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.

Kwa uamuzi huo wa Waitara ambaye alikuwa CCM kabla ya kujiunga Chadema, jimbo la Ukonga linabaki wazi.

Waitara amekuwa mbunge wa pili wa Chadema na wa tatu wa upinzani kuhama chama na kujiunga na CCM.

Wengine wa Dk Godwin Mollel (Siha) na Maulid Mtulia (Kinondoni).

ALICHOANDIKA Zitto:

View attachment 821107
wacha aende wapinzani tutafika japo kwa machozi mengi,atavuna alichokipanda
 
Hii mbinu ya mkuru wa kaya (saliti upate cheo) sidhani kama itamwaacha mtu salaama. Ngoja tuone....
 
umewahi fikiria;kabla hujazaliwa uliishije,vivyo baada ya mauti utarejea na ndo utakua mwisho wa mwanzo wa maisha yako/yangu
 
Tusimung'unye maneno mpango ni kuua upinzani na sasa wapinzani wanaohama vyama vyao ndo hawa wanateuliwa kuingia serikalini. Waliobaki ndio hawa wenye kesi za uchochezi. Kwa sasa ni kuchagua kubaki upinzani upate tabu au hamia ccm upate cheo.
Mkuu hufahamu kwamba Waitara alikuwa kada wa CCM kule Tanga? Wanaohama wote wanalalamikia demokrasia ndani ya chama, wanalalamika kwamba mwenyekiti anapiga pesa ndefu na hataki kupingwa? Zitto, Kitilla, Mzee Arfi, Mwigamba, Tuntemeke, Shonza, nk wote walilalamukia vitu hivyo hivyo. Ni wakati muafaka sasa CHADEMA ijiangalie upya kuhusu hizo tuhuma vinginevyo kibra ipo pembeni yao.
 
Chadema hakuna zimwi wala shetani , dola ina nguvu kama hamkumpata wa kuiheshimu mmekwisha. Nawapa pole chadema watapata tabu sana ( kwa sauti ya mwenyekiti)..
Nawapa pole sana na nyie kwa kusugua benchi maana wapinzani wanakuja na kubeba nafasi!naona roho inawauma lol..mtapata tabu sana endeleeni kusugua gaga[emoji16]
 
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Mwikwabe Waitara, atangaza kuniuzulu CHADEMA na kuhamia CCM. Kajiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

> Asema sababu ni kutofautiana na viongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA baada ya kuhoji kuhusu matumzi ya luzuku pamoja na demokrasia ndani ya chama

> Ameeleza kuwa alihoji matumizi ya Milioni 237 za ruzuku kwani mpaka sasa CHADEMA haina Ofisi Kuu, ya Kanda wala Mkoa

> Mwenge wa Uhuru umekuja kuzindua miradi ya maendeleo niliyoipigania lakini naambiwa usiende pale na mimi shida yangu haikuwa CCM pale ilikuwa ni mradi niliopigania

"Leo nimejiondoa rasmi CHADEMA kwahiyo mimi sio Mbunge tena, nimetupa jongoo na mti wake" amesema Mwita Waitara

“Mimi nataka niende mahali ambako kuna kazi za kufanya,” Waitara amewaambia waandishi na kuongeza kwamba anatamani kuwa Waziri Kamili.

Habari zaidi....

Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara amejiuzulu uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM leo Jumamosi Julai 28, 2018.

Waitara ametangaza uamuzi wake huo leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi ndogo za CCM Lumumba mjini hapa, akiwa sambamba na katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.

Kwa uamuzi huo wa Waitara ambaye alikuwa CCM kabla ya kujiunga Chadema, jimbo la Ukonga linabaki wazi.

Waitara amekuwa mbunge wa pili wa Chadema na wa tatu wa upinzani kuhama chama na kujiunga na CCM.

Wengine wa Dk Godwin Mollel (Siha) na Maulid Mtulia (Kinondoni).

ALICHOANDIKA Zitto:

View attachment 821107
Na bado. CHADEMA mtaendelea kuisoma namba.
 
Chadema mmeumbuka. Waitara kaeleza mkutano uliofanyika wa kumtaka Lissu agombee uenyekiti. Siku mbili mbele mbowe akamlissu, kwa ujinga na chuki zenu mkajiegesha kwa serikali eti ndio imefanya hayo. Aibu yenu wenyeweeeee
 
Aliwahi kusema yeye pia ni muhimu wa chemistry na maths. Akaenda mbele na kusema kwa bashasha kama ilivyo kwa mheshimiwa mkuu. So no wonder.
 
Heri hata alikotoka aliweza hata kuhoji matumizi ya ruzuku au kutaka kugomea uenyekiti.Je, huko aendako ataweza kuhoji ununuzi wa dreamliner au ujenzi wa chato airport? Au anaweza kuhoji kwanini mwenyekiti anachaguliwa bila kupingwa 100% na watu zaidi 1000? Binafsi sijawahi mwamini mwalimu hata Siku moja!!!! Labda JK pekee.
 
Last edited:
CHADEMA haitakufa kwa watu kuondoka. Chadema itakufa iwapo itaacha misingi yake. Hawa wanaoondoka wasiwatishe na msikate tamaa!!
 
Nawapa pole sana na nyie kwa kusugua benchi maana wapinzani wanakuja na kubeba nafasi!naona roho inawauma lol..mtapata tabu sana endeleeni kusugua gaga[emoji16]
Ahsante charty kweli tunaumia sana roho.ngoja tusubiri labda kuna siku nasiye tutakumbukwa.
 
Naamini hivia sasa ataenda kuhoji matumizi ya ruzuku vizuri pamoja na demokrasia. Wenzake wanateswa wanauawa na bado anaenda kuungana na hao wanatuhumiwa??
 
Chadema mmeumbuka. Waitara kaeleza mkutano uliofanyika wa kumtaka Lissu agombee uenyekiti. Siku mbili mbele mbowe akamlissu, kwa ujinga na chuki zenu mkajiegesha kwa serikali eti ndio imefanya hayo. Aibu yenu wenyeweeeee
Huu ni ujinga mtupuuuu! Aibu kwa serikali ambayo kama kweli imeshindwa kumpata/kuthibitisha kama huyo unayemtaja ndiye aliyehusika. Kama serikali imeshindwa kuwapata/kumpata aliyemlisu Lisu vipi nchi jirani inayotamkwa kuwa ziwa lots Nyasa ni lao tutawaweza?
 
Back
Top Bottom