Uchaguzi 2020 Mbunge wako amefanya nini kwa miaka hii mitano mpaka sasa?

Uchaguzi 2020 Mbunge wako amefanya nini kwa miaka hii mitano mpaka sasa?

Jimbola Kibambq Mungu ndio anajua, huyu jamaa asirudi tena, atafute Jimbo lingine huko.
 
Kwanza unazifahamu kazi za mbunge?
Kazi za mbunge ni zipi?
Weka kwanza kazi za mbunge ndio maswali yako yatajibika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unazifahamu kazi na wajibu wa mbunge?
"Kupigania sana" ndio kufanyaje?
Stanslaus Mabula mbunge wa Nyamagana jiji la Mwanza kapigania sana tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama maeneo sugu kama buhongwa,mahina,kishili bulale,sawa ya chini na ya juu.

Bwana stanslaus mabula imefanikiwa kuionganisha barabara muhimu ya buhongwa kishiri kwa kiwango cha changarawe.
Ameboresha zahanati nyingi kwa kuongeza vifaa tiba na majengo.

Bwana Mabula kajitahidi sana ukilinganisha na wabunge waliopita kwa kuhakikisha vijana wanapata mikopo kupita mfuko wa vijana wa mkoa.kwa kweli Stanslaus Mabula ana mengi mazuri na ana stahili pongezi za dhati,ametufanyia mengi wana nyamagana na anastahili pongezi.

Yapo mengi sana lkn naomba niwasilishe haya machahce

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafahamu wajibu wa mbunge?
Igunga tumetelekezwa na Dalali Kafumu Mzee wa MAKINIKIA. Hata barabara YA kwenda Kijijini kwao Itumba ni mbaya haipitiki,Barabara za Wilayani Igunga ndio OVYO ovyoo wala hana habari. Wapambe wake wameanza kuzungua kugawa rushwa kwa Viongozi wa KATA elfu hamsini kila Mjumbe ili kumsafisha, Japo kwa CCM ya Dkt Magufuli sidhani kama rushwa zake zitamsaidi. Watanzania sio Wajinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie wenyewe mnachagua mbunge kwa kuangalia vyama tu,hamchagui mtu kwa sababu mmeona anafaa kuwa mbunge wenu bali mnamchagua kwa sababu ya chama alichopo.
Sasa unaambiwa mbunge tangu alivyochaguliwa hajakanyaga kwenye jimbo lake lakini uchaguzi ukija anachaguliwa tena hapo ndiyo utashangaa,tunakuwa na wabunge ambao hawaoni kama wanatakiwa kuwajibika kwetu kwa sababu sisi ndio tuliyowachagua.

Tuache kuendekeza sana siasa za vyama.
 
Unafahamu kazi za mbunge?

Back
Top Bottom