Uchaguzi 2020 Mbunge wako amefanya nini kwa miaka hii mitano mpaka sasa?

 

Mkuu, naona unalitazama jimbo LA nyamagana kwa angle ya sahwa. Kwani kila unachokieleza kimelenga huko kana kwanba ndio eneo pekee katika jimbo..
Kueleza kuwa maji yanapatikana buhongwa na hasa bulale wakati wakazi wake tukilalamika ukosefu wa huduma hivyo kwa muda wa hadi wiki moja ni kutukosea.
Kwa kuwa umeiongea buhongwa, jitahidi kuuliza au kufika bulale kama hiyo njia inahitaji kuitwa barabara. Kuna watu watakushabgaa kuwa barabara zinapitika ilhali kwa sasa bajajj za kutoka buhongwa kupitia nyanembe hadi bulale, zimesitisha safari kutokana na ubovu wa barabara.
Vivyo hivyo kwa barabara nyingi za mwanza ni majanga. Muulize kwanini barabara ya California alikokuwa akiishi miaka miwili iliyopita haipitiki ilhali alikihamia upande wa pili ikikarabatiwa kila siku!
Umefika stand ya nyabulogoya, inafaa kwa matumizi ya binadamu,? Kuna mbunge hapo? Anafanya nini?
Kuzungumzia changamoto ya mji katika mji wa mwanza, ashakum si matusi,, ni ujuha ! Ni mpumbavu pekee atalia kiu akiwa katikati ya kisiwa. Vipi ukose maji ilhali umezingirwa na ziwa?
Hicho unachosema chanzo kipya cha butimba, kwanza ungetuambia kitaanza lini
 
Huyu jamaa ni shida kubwa, kuelekea Majohe, barabara haipitiki kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbunge wangu Jitu Patel hajafanya lolote hata hajui jimbo lina kata ngapi,huyu kabachori ikifika uchaguzi anaanza kumwaga hela

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la maji Mwanza ni sugu kwa majimbo yote, usitudanganye hapa. Mie napiga simu za malalamiko ya maji almost daily na hakuna jipya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hela za hawa watu zinakuwaga ngumu sana,unaweza kusema utazipokea ila huwapigii kura lakini ukifika ktk sanduku la kura nafsi inakataa [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3][emoji3][emoji3]wanazipitoshaka kuziloweka pahala kabla ya kuzigawa. Chief huo ni uzembe wako binafsi kupiga kura kwa ajili ya pesa kwa mtu ambaye ni bora kuongozi badala ya kuongozi bora

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji3][emoji3][emoji3]wanazipitoshaka kuziloweka pahala kabla ya kuzigawa. Chief huo ni uzembe wako binafsi kupiga kura kwa ajili ya pesa kwa mtu ambaye ni bora kuongozi badala ya kuongozi bora

Sent using Jamii Forums mobile app
Nazungumzia maeneo ya vijijini mkuu huko ndio mitaji ya wanasiasa ilipo na wanajua wapi kwa kuwashika,huku mijini wengi wana uelewa kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mantiki hiyo unasema; Tuwaondoe hawa mambumbumbu wa ccm tuweke vichwa wa kutoka upinzani. Serekali itanyooka na maendeleo yatakuja??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…