Mbunge wangu Mwigulu umeshindwa kabisa!

Mbunge wangu Mwigulu umeshindwa kabisa!

Wabunge hawa tunawaonea tu, wao hawakusanyi kodi sasa hayo mnayotaka wafanye watazifanya kwa hela ipi?

Ni jukumu la serikali inayokusanya kodi kuratibu na kuzitumia kuleta maendeleo kwa wote bila ubaguzi.

Kama tutaendelea kuendekeza dhana ya kuwa mbunge ndio ataleta maendeleo, basi tutasubiri sana kwani akiitarifu serikali kuhusu mahitaji ya jimbo lake kisha serikali isitekeleze chochote sasa hapo atafanya nini!!

Inatakiwa tu-adopt mfumo wa majimbo (Decentralization) ili kila mkoa itumie rasilimali zake ipasavyo kujiletea hayo maendeleo, huu utaratibu wa sasa ni wa hovyo kwani rais anatumia fedha za umma kama turufu ya kutafuta sujuda kwa wananchi. This is a very stupid set up.
 
Kwa hili la kwamba hakuna mbunge wa upinzani atarudi bungeni hasa wa cdm uko sahihi sana, bila kujali ni trend readings au utabiri. Na sio kwasababu ccm wanakubalika sana ama cdm hawachaguliki, bali sababu hasa ni kwakuwa rais aliye madarakani hawezi siasa za ushindani, na ana chuki ya wazi dhidi ya cdm. Kwakuwa katiba yetu ina madhaifu, basi rais aliye madarakani anatumia nguvu yake ya kimadaraka kuamua nani awe kiongozi katika chaguzi zetu, na kwakuwa taasisi zilizopo pia zinatii kila atakacho rais bila kujali uhalali wake, basi lazima kiongozi anayemtaka rais awe ndio anayekuwa, bila kujali sauti ya box la kura. Hili wala halihitaji mjadala, kwani hizo siasa chafu kila mtu anaziona na kuzifahamu.
No usiziite siasa chafu kwasababu hakuna standards formula ya siasa safi. Mimi hii nimeiita ni Tanzanian Democracy ambayo ni part of African Democracy model.

P
 
Mkuu Pascal Mayalla labda hujamuelewa hoja yake.... Anachosema yeye ww unabashiri kila kitu kwa pande zote alafu moja wapo likitick uonekane ww uliona mapema.

Mfano siku zitto anatimuliwa uliandika either zitto atapotea au Lissu atapotea..... Anyway ACT haikufurukuta 2015 so ukadai ni karma kwa zitto. Baada ya Lissu kupigwa risasi ukadai tena huenda ni karma kwa lissu kwa kumtesa zitto, bado hapo hapo uliuliza Je lissu anafaa kupambana na magufuli 2020??

Sasa ni hivi
ACT ikiwa KUB 2020 utasema ni karma kwa CHADEMA kwa issue ya zitto.

Lissu akishinda utafufua uzi uliodai anafaa kugombea u-Rais

CHADEMA ikishinda utafufua uzi wa 2011 uliodai chadema haijakua ila IMEPAA.

Yaani you predict both sides of the coins with vague,cryptic and open-ended predictions such that the probability of making a successful guess is imminent!!

tindo
Duh!. Jf kiboko!, watu mmenistukia!. Itabidi huu ushehe Yahya wa siasa za bongo niache!.
P
 
No usiziite siasa chafu kwasababu hakuna standards formula ya siasa safi. Mimi hii nimeiita ni Tanzanian Democracy ambayo ni part of African Democracy model.

P

Unatumia verified user, hivyo nitashangaa ukisema kuna siasa chafu. Hakuna cha Tanzania democracy au African model democracy, ni siasa chafu fullstop. Labda useme unafaidika nazo lakini sio kuzungusha zungusha maneno kaka.
 
Wabunge hawa tunawaonea tu, wao hawakusanyi kodi sasa hayo mnayotaka wafanye watazifanya kwa hela ipi?

Ni jukumu la serikali inayokusanya kodi kuratibu na kuzitumia kuleta maendeleo kwa wote bila ubaguzi.

Kama tutaendelea kuendekeza dhana ya kuwa mbunge ndio ataleta maendeleo, basi tutasubiri sana kwani akiitarifu serikali kuhusu mahitaji ya jimbo lake kisha serikali isitekeleze chochote sasa hapo atafanya nini!!

Inatakiwa tu-adopt mfumo wa majimbo (Decentralization) ili kila mkoa itumie rasilimali zake ipasavyo kujiletea hayo maendeleo, huu utaratibu wa sasa ni wa hovyo kwani rais anatumia fedha za umma kama turufu ya kutafuta sujuda kwa wananchi. This is a very stupid set up.

Mkuu huwezi kuamini, hilo tatizo la wabunge kusemeka hawajafanya kitu, hata wabunge wenyewe nawasikia wakitamka mpaka ndani ya bunge. Huwa nawasikia wabunge wa ccm wakiwaambia wabunge wa upinzani, mnaogopa kwakuwa hajamfanya maendeleo yoyote kwenye majimbo yenu. Baada ya kujua wajibu wa mbunge, na ni nani hasa anapaswa kupeleka maendeleo, nikisikia mtu anasema mbunge hajaleta maendeleo napata kinyaa. Ni sawa na kumlaumu golikipa kwanini timu haina magoli ya kufunga wakati wajibu wake sio kufunga magoli.
 
Umwambie tena afute ule uchafu alio andika kwenye miamba, madaraja, na ma culvert kuwa yeye ni rais wa tanzania
Wewe ni Mchumi na siku zote wachumi huelezea uhalisia wa mambo kwa namba. Wataalamu wanadai "namba haziongopi".

Mheshimiwa umekosa ujasiri wa kusema mambo ambayo umeifanyia Iramba kwa sababu hamna ulichofanya ambacho unaweza kujivunia.

Au unataka kuongelea kwa mfano shule yako ya Kata yaani Kyengege kutoka nafasi ya 15 kimkoa Mwaka juzi na kufikia nafasi ya 8 kwa Mwaka jana hayo ni mafanikio?

Viko wapi visima vya maji ulivyoahidi katika vijiji mbalimbali vya Iramba, umeshinikiza vipi Mradi wa umeme wa REA kukamilishwa pale ulipokomea?

Ukiacha Kituo cha Afya cha Kinampanda wapi kwingine unapojivunia uliacha?

Ukweli ulikazania siasa za Kitaifa za kutaka uwe Rais - wapi sasa maendeleo uyaonayo yameletwa na siasa zako za Kitaifa zaidi ya kuzidi kunyongonyezwa tu wewe na Nape na Januari?

Na inadaiwa umewekewa TISS wa kumwaga tu hadi chumbani kwako!

Kikubwa tumia akili achia ngazi mapema, tafuta kitu bora zaidi cha kufanya ili kuepukana na Rais Magufuli kwenye siasa kwa kuwa kwa vyovyote anavyokuchulia wewe ni threat kwake atahakikisha anakukata juu kwa juu na Ubunge hutopata!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hilo la tume ya uchaguzi naona ni sisi tu tunaongelea humu mitandaoni, lakini sioni vyama vya upinzani wakizungumzia hilo. Leo nimesikia wanaongelea kuhusu wito wa viongozi wa ccm huko ikulu.
Kuna wakati tutapanga jinsi ya kuwaadhibu hawa viongozi tena hao tunawamudu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,

Paskali hapa ni kama unamchora tu Mwigulu. Ufahamu hata Mwigulu mwenyewe anajua hakuna uchaguzi bali rais ndio anaamua uwe mbunge, na iwapo Rais hataki uwe mbunge, hata uchaguliwe na wananchi wote hutatangazwa mshindi.

Uzuri hata Mwigulu anaujua ukweli huu kwani naye ameshiriki muda mrefu siasa chafu hapa nchini, hivyo kinachomkuta hivi sasa ni karma.
Ogopa sana mpaka makamba Jr binafsi yake ajaamua kama ata ombea au LA
 
chizcom,

Mkuu tunashukuru kwa mchango wako, nakushauri achana na michango ya siasa rudi shule kwanza ukijifunze kuandika kwa usahihi, kama kuweka koma, nukta na matumizi ya herufi kubwa na ndogo. Pia una tatizo la matumizi ya herufi H kwenye uandishi wako. Usidhalilishe shule za kata tafadhali.

sipo shule na sio mfatiliaji sana wakiswahili katika mahandishi ndio maana kukosea kupo.asante

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
MWIGULU NCHEMBA ATAANGUKIA PUA KWENYE UCHAGUZI UJAO KWANI HATA JINA LAKE HALITAPITA 7BU KUBWA NI KWAMBA BWANA MKUBWA HAMTAKI, KUNA WATU HUMU WANASEMA WANAIRAMBA NDIYO WENYE SAUTI YA MWISHO NADHANI HAWAJUI UKUBWA WA MAMLAKA YA RAIS, HIVI KULE KWA TUNDU LISSU NI KWELI WANASINGIDA MASHARIKI NDIYO WALIOKUWA NA SAUTI YA MWISHO KWA YALIYOTOKEA?
JANUARY,FEBRUARY, NAPE,MWIGULU HAWATA TEULIWA 2020 KUGOMBEA UBUNGE MKULU HAWATAKI HAWA WATU KABISA KWANI WALIONYESHA TABIA ZA KUJIMWAMBAFAI KUMZIDI MALAIKA.
 
wakati anaaguza mrekodi kama ulikiwapo ama ukiwapo....kuhisi kitu kisha ukakiamini ni ugonjwa wa kisaikolojia..
Nitajie mpinzani yoyote aliyepata ubunge ama udiwani kwenye chaguzi yoyote iliyofanyika toka Magufuli amekuwa rais. Chini yake ndio tumeona kwa macho yetu mabox ya kura yakitolewa vituoni mbele ya polisi na wasimamizi wa uchaguzi kwenda kujazwa kura za ccm, kisha msimamizi wa uchaguzi kutangaza mshindi aliyepatikana katika mazingira hayo! Chini ya utawala wake ndio tumeshuhudia ofisi zikifungwa ili wapinzani wasirejeshe fomu ofisini ili ccm wapite bila kupingwa. Chini ya utawala wake, ndio tumeona uchaguzi wa nchi nzima viongozi wakipatikana bila kupigiwa kura, na yote ni maagizo yenye baraka zake. Kibaya zaidi ushindi huo wa mezani, umeshangiliwa kuliko hata chaguzi ambazo ccm walikuwa wakishinda kwa kura kabla yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni Mchumi na siku zote wachumi huelezea uhalisia wa mambo kwa namba. Wataalamu wanadai "namba haziongopi".

Mheshimiwa umekosa ujasiri wa kusema mambo ambayo umeifanyia Iramba kwa sababu hamna ulichofanya ambacho unaweza kujivunia.

Au unataka kuongelea kwa mfano shule yako ya Kata yaani Kyengege kutoka nafasi ya 15 kimkoa Mwaka juzi na kufikia nafasi ya 8 kwa Mwaka jana hayo ni mafanikio?

Viko wapi visima vya maji ulivyoahidi katika vijiji mbalimbali vya Iramba, umeshinikiza vipi Mradi wa umeme wa REA kukamilishwa pale ulipokomea?

Ukiacha Kituo cha Afya cha Kinampanda wapi kwingine unapojivunia uliacha?

Ukweli ulikazania siasa za Kitaifa za kutaka uwe Rais - wapi sasa maendeleo uyaonayo yameletwa na siasa zako za Kitaifa zaidi ya kuzidi kunyongonyezwa tu wewe na Nape na Januari?

Na inadaiwa umewekewa TISS wa kumwaga tu hadi chumbani kwako!

Kikubwa tumia akili achia ngazi mapema, tafuta kitu bora zaidi cha kufanya ili kuepukana na Rais Magufuli kwenye siasa kwa kuwa kwa vyovyote anavyokuchulia wewe ni threat kwake atahakikisha anakukata juu kwa juu na Ubunge hutopata!
Hivi Mwigulu ana hata kibanda Iramba??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeonaee
Watu wanampigia kelele Zitto Kabwe haonekani jimboni kwake, wanawasahau wabunge wa CCM 90% wanajazana Dodoma na Dar es Salaam na kwenye majimbo yao hawaonekani kabisa kusaidia changamoto na kero za wananchi wao.

Hasa waliopata "VYEO" kwenye serikali hii. Ila muda ndio ushafika wa "MAPAMBANO".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unataka kugombea Iramba, gombea tuu kwa kusema utafanya nini, hakuna jimbo lolote ni mali ya mtu, huna haja ya kutumia jina la Magufuli kumtishia Mwigulu, Mbunge aliyepo ni Mwigulu na ni Mbunge wa jimbo la Iramba na amechaguliwa na wana Iramba na sio Mbunge wa jimbo la Magufuli, hivyo hivyo vitisho vya kuwa Magufuli atamkata, usitishe watu, wanaochagua ni wana Iramba, wakijiona kama bado wanamuhitaji Mwigulu wao na Magufuli kweli akamkata, its up to Wanairamba kumkubali huyo atakayepitishwa au kumchukua Mwigulu wao na kumrudisha kupitia chama kingine, hivyo ndivyo wapinzani wengi waliingia bungeni toka Dr. Slaa hadi Mwambe.

P
Wewe ni nani kukataza watu kutumia haki yao kumtaja Mh.Magufuli.Yaani unataka kuwafanya watu wamuogope Mh.Magufuli kisa ni Rais ?? Tusijione kua sisi ni bora na miamba kwakua ni wasukuma na tupo Ikulu.@Pascal

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom