Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Aisee[emoji22]
Hatari sana.

Haya mambo ya kufuga mbwa,na una watoto wadogo,na haushindi nyumbani ni hatari sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
subiri sasa mwenyeji ajisahau aingine ndani labda kuchukua simu yake inaita wee akirudi anakuta unavuja damu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Mali asili walifuata nini?
 
Hauhofii familia nyumbani?Hasa watoto[emoji15]

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah hao mbwa hawana shida wana mapenzi sana na binadamu yale ya kweli ukitoka anatamani akusindikize mpaka getini kama usiku wanaonyesha ishara ya upendo kwa kutikisa mikia yao hao Pitbull hawatikisi mkia muda wote wapo kishari shari tu mbwa akilala ukimstua ghafra kwa bahati mbaya anakubwekea mwenyewe huyo ndio Pitbull na pia hawa German wanafundishika sana...
 
Kwa kweli nyie watu wenye mbwa mtatembeleana wenyewe

Nikijua tu una mbwa ndani kwako sifiki.. maisha ya mashaka siyawezi.
 
Kwa kweli nyie watu wenye mbwa mtatembeleana wenyewe

Nikijua tu una mbwa ndani kwako sifiki.. maisha ya mashaka siyawezi.
Mbwa wangu anakaa banda kubwa hata hauwezi kujua kama pana mbwa na wala apigi kelele hovyo na pia ni wale mbwa wanaofundishwa sio yupo nje tuu lazima aume mtu ni mbwa mkubwa sana naweza kufanya nae mazoezi nje huko bila hata kumfunga na hana shida ila ukimpa ishara kamata kile ndio hapo anatii amri,nilikua na mbwa wa kawaida Mbeya ila alikua mkali kweli pana mama alitupa mtoto maeneo ya mbali kidogo wale mbwa madume walimzingira yule mtoto mpaka alfajiri walipokuja watu ndio wakaondoka na yule mtoto alikua mzima hawakumdhuru na alichelewa kuingia ndani maana dume ana kawaida hata ukuta uwe mkubwa vip anaruka na kurudi ndani kwa wale wasiokua na mafunzo mimi mbwa siwaogopi kabisaa ila sio hao Pitbull jamii ya Simba...
 
Mbona huyo mbwa sio bulldog?. Huyu ni boerboel na bado nadhani sio pure breed.

Bulldog kuna mtu lazima wangebaki naye maana aking'ata kang'ata tena wawili ndio kabisaa angekufa mtu hapo kama sio watu.

Mbwa hataki mambo yakushtukizwa hata ukiwa mhudumu wake. Pia kuna uwezekano rangi za nguo walizokuwa wamevaa zikawa ni rangi alizofundishiwa huyo mbwa, ukichukua ni usiku ni rahisi kushambuliwa.

Ukiona mbwa wako amekubadilikia muite jina bila kusita (ni ngumu) ila kamwe usikimbie au kumtishia maana atakurarua hautaamini.

Mwisho mbwa wa hivi hawashauriwi kwa ulinzi majumbani, fuga German shepherd au Belgian Malinois hawa ni mbwa asili sio wa maabara.
 
Yaani kile kitendo cha kwenda kwa mtu
Eti natembea kwa manati nakufuata kwa nyuma,sina uhuru kisa mbwa!
Aisee..tabu hizo.

Huku Mbeya mtaani naona tu mambwa yamezagaa zagaa ya kawaida...watu aanayaachia mambwa yanazurula jamani wanatupa shida bure,watoto wetu wanaogopa.


Hongera Mkuu kwa kupenda mbwa.

Mimi tangu mbwa wangu wa utotoni afariki sijawahi kufuga tena mbwa na wala sitaki...labda nikija kuwa millionea mdogo,kwa sasa sina cha kuibiwa.

Na wala sitaki kabisa kuja kuishi na mtu anafuga mijibwa.
Heri niendelee kufuga kitimoto na ng'ombe nikijua kabisa ntakula nyama na kunywa maziwa..kuliko nafuga jitu ambalo baadaye dishi likiyumba linanirarua.
 
Yaani mbwa alisharuka na Mtoto unasema mwite jina😳
 
Yaani mbwa alisharuka na Mtoto unasema mwite jina😳
Hao watoto kuna namna alikosea, mbwa ukute kanguruma wao wakaanza mbio au madihara nae.

Hao watoto ndio walitakiwa kumuita jina, huyo mama na kaka hawakupaswa maana mbwa anaweza tafsiri kama amri ya kushambulia sababu kwanza anayemwita anamjua na probably atamwita kwa uoga au vilio so kwa mbwa ni kuwa mmiliki wake yupo hatarini. Aisee hatakuacha salama.

Mbwa ni wakorofi ils hakuna mbwa mkorofi kwa mtu anayeweza kummudu. Kumpa mbwa chakula sio kigezo eti hatakushambulia. Kigezo pekee ni kuweza kummudu tu.

Point nyingine muhimu, mbwa wanafundishwa kwa rangi, sasa kuwa makini na mavazi yaliyopo nyumbani kwako na muda yanapotumiwa.

Katika hali zote kuna uzembe hao watoto waliufanya ukawaponza wote.
 
Nilipokua.kijana mdogo kwetu nimefuga sana mbwa hawa wa kawaida.Sasa hivi nimekua baba wa familia nimefuga Germany Shephard...jike..ana miaka 2 sasa.Nimekuja kugundua kuna utofauti mkubwa sana nikilinganisha na hawa wengine....yuko composed, hapanick, habweki ovyo ovyo, royal.muda wote anakuangalia straight machoni kama vile anasubiri umwambie kitu.Akibweka mishindo miwili tu mtu wa kawaida lazima a-feel.
Nawaza nitafute Rotweiler dume, nimix
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…