Mbwana Samatta ilikuwaje ukashindwa kumhamishia baba yako ‘ushuani’ ukakubali afie Mbagala?

Ukisikiliza interview ya baba yake itafute YouTube,huko ushuani Wana maghorofa,baba yake ndie alikataaa kuhama mbagala Panapo mpa amani kwenda ushuani kwenye upweke hakuna hata vijiwe vya kahawa.
Pana watu wanapata vibe sana kuishi uswahilini
 
Thank you- wewe unawafahamu vizuri sana wazee wetu! Na kwa kariba ya wazee kama Mzee Samatta ambae anaonekana wazi ni mtu wa kujichanganya, katu huwezi kumwahamishia Ushuani uzeeni!!
Kuna watu wanaona kila mzee wanaweza kummudu kumuamulia mambo.

Kuboresha alipo inafaa zaidi lakini kwa mjini ni ngumu sana. Pia kuwahamisha watu hasa waswahili ni ngumu. Ukitaka kuwatoa wanaona umeanza kiburi na mzee ndio kagomea hapo hataki kuhama anasema pesa peleka msikitini
 
Upo sahihi kabisa! Unless mwenyewe yupo willing, vinginevyo best option ni kuyaboresha mazingira aliyoyazoea! Tena kama wazee wenyewe ni wale wa vijijini waliozoea kujishughulisha shughulisha hata kama hakuna anachopata, ukimleta mjini unaweza kumpunguzia hata siku za kuishi kwa sababu mtu ambae tangu utotoni hadi uzeeni kazoea mara kwenda shamba, mara kuokota kuni na kujitishwa maji halafu umpeleke sehemu anashinda ndani tu kwenye kochi kuangalia tv! Kama yupo reluctant na kuhama, bora hiyo nyumba mzuri, tv na makochi kamwekee mazingira yale yale ambayo ataamka asubuhi atachukua jembe kung'oa ng'oa majani kuzunguka nyumba, na hapo utamwongezea siku kadhaa za kuishi!
 
Yale yale tu, ni maeneo hayo hayo.....kuchezea kote maisha alikwenda kujificha uchochoroni, bangi hizi jamani.
Kijichi uchochoroni? Hivi hata Kijichi kwenyewe unakufahamu wewe au unasikia tu Kijichi?! Utaamua kuishi Kijichi uchochoroni ikiwa huna pesa lakini kuna neighborhood kubwa sana ya Kijichi ambayo ni ya Kishua!!
 
Kijichi ni ushuani
 
Upo sahihi kabisa! Unless mwenyewe yupo willing, vinginevyo best option ni kuyaboresha mazingira aliyoyazoea! Tena kama wazee wenyewe ni wale wa vijijini waliozoea kujishughulisha shughulisha hata kama hakuna anachopata, ukimleta mjini unaweza kumpunguzia hata siku za kuishi kwa sababu mtu ambae tangu utotoni hadi uzeeni kazoea mara kwenda shamba, mara kuokota kuni na kujitishwa maji halafu umpeleke sehemu anashinda ndani tu kwenye kochi kuangalia tv! Kama yupo reluctant na kuhama, bora hiyo nyumba mzuri, tv na makochi kamwekee mazingira yale yale ambayo ataamka asubuhi atachukua jembe kung'oa ng'oa majani kuzunguka nyumba, na hapo utamwongezea siku kadhaa za kuishi!
Mzee Samatta sio kundi hilo,
Haya basi kama aligoma angeboresha makazi yake
 
Mzee alikuwa na cheo cha ACP.Masaki,obey ndiyo nyumba za watu wa vyeo vyake walipokuwa wanaishi.Mzee alichagua life style ya kiswaziiiii kwa uswahili wake mwenyewe.
 
Inawezekan mzee aliona bond aliyotengeneza na majirani zake inampa faraja na anaishi kwa furaha, kwenye maisha kuna watu wala hawahitaji vitu vikubwa sana wanajali amani na furaha na wakiikosa hawawezi kuishi hiyo sehemu hata kama ina hadhi kubwa kiasi gani, jamaa kwa uwezo wake hajashindwa kumuondoa mzee wake hapo ila nafikiri Baba ndo hakutaka mwenyewe.

Je vipi kuhusu makazi ya Baba yake aliboresha au hajayaboresha?
 
Mkuu yani ACP Akakae Masaki hawana ubavu huo tokea Zamani mpaka kesho. Polisi wengi njaaa ukijumlisha na pesa zao za rahana, watu wanashangaa maisha ya Mzee Samatta wanatakiwa wajue hayo ndiyo Maisha yao Polisi wengi, huyo Baba Samatta angelikuaga Mwanajeshi wa JWTZ angekua tofauti kwanza angekua na eneo kubwa ata kama ni Uswahilini na Nyumba nzuri.
 
Kijichi ni mtoni,mtoni sio mbagala
Unajidanganya wewe
Embu nitajie post code ya kijichi ni ngapi na postcode ya Mwanamtoti ni ngapi?

Ni Kam wana Mbagala wanavyoikataa msikitini, walisema ni mtoni badala ya mbagala
 
Mbagala Zakheem sijui Rangi tatu ni sehemu za ovyo na za hali ya chini sana kwa jijini Dar es salaam.

Mahela yote ya wazungu ukashindwa hata kumjengea mzee wako mtoni kijichi

Diamond sio mjinga kuhama Tandale, Bakhresa zamani aliishi Kariakoo ila serikali ilimuhamisha kinguvu, najua hata Sumaye alikuwa na nyumba Mbagala ila alipopata akili na madaraka alihama.

Hakuna Staa mwenye akili atakubali kuishi mbagala hapa nyumba hapa jalala

Mimi sio staa na sina hela ila siwezi kuishi Mbagala.

Umemdhalilisha mzee wako. Wachezaji wenzako wa Ulaya wakija kukupa pole watakuona wa ajabu sana.

Sio kwamba wa Masaki hawafi, ila wastaafu hawapendi kelele wanapenda kuishi sehemu tulivu. Mbagala ni ‘ushenzini’

Watu wamekuja msibani hakuna parking, hakuna sehemu ya kufunga hema

Kama aligoma kuhama ungehamisha majirani ukaboresha makazi yake hapohapo
Mbagala kwa ovyo sana.
 
Mkuu yani ACP Akakae Masaki hawana ubavu huo tokea Zamani mpaka kesho. Polisi wengi njaaa ukijumlisha na pesa zao za rahana, watu wanashangaa maisha ya Mzee Samatta wanatakiwa wajue hayo ndiyo Maisha yao Polisi wengi, huyo Baba Samatta angelikuaga Mwanajeshi wa JWTZ angekua tofauti kwanza angekua na eneo kubwa ata kama ni Uswahilini na Nyumba nzuri.
Tibaigana akiwa na cheo cha ACP alikuwa anaishi masaki.Alfred Gewe alivyokuwa na cheo cha ACP alikuwa anaishi oysterbay.Mwidadi Ali akiwa ACP alishi obey, kastaafu yupo Temeke uswaziuswazi.
 
Mbagala Zakheem sijui Rangi tatu ni sehemu za ovyo na za hali ya chini sana kwa jijini Dar es salaam.

Mahela yote ya wazungu ukashindwa hata kumjengea mzee wako mtoni kijichi

Diamond sio mjinga kuhama Tandale, Bakhresa zamani aliishi Kariakoo ila serikali ilimuhamisha kinguvu, najua hata Sumaye alikuwa na nyumba Mbagala ila alipopata akili na madaraka alihama.

Hakuna Staa mwenye akili atakubali kuishi mbagala hapa nyumba hapa jalala

Mimi sio staa na sina hela ila siwezi kuishi Mbagala.

Umemdhalilisha mzee wako. Wachezaji wenzako wa Ulaya wakija kukupa pole watakuona wa ajabu sana.

Sio kwamba wa Masaki hawafi, ila wastaafu hawapendi kelele wanapenda kuishi sehemu tulivu. Mbagala ni ‘ushenzini’

Watu wamekuja msibani hakuna parking, hakuna sehemu ya kufunga hema

Kama aligoma kuhama ungehamisha majirani ukaboresha makazi yake hapohapo
Hii mitazamo ya masikini, wenye hela hawana haja ya kujikweza
 
Inawezekan mzee aliona bond aliyotengeneza na majirani zake inampa faraja na anaishi kwa furaha, kwenye maisha kuna watu wala hawahitaji vitu vikubwa sana wanajali amani na furaha na wakiikosa hawawezi kuishi hiyo sehemu hata kama ina hadhi kubwa kiasi gani, jamaa kwa uwezo wake hajashindwa kumuondoa mzee wake hapo ila nafikiri Baba ndo hakutaka mwenyewe.

Je vipi kuhusu makazi ya Baba yake aliboresha au hajayaboresha?
Basi angewanunua majirani na kuboresha makazi
 
Tibaigana akiwa na cheo cha ACP alikuwa anaishi masaki.Alfred Gewe alivyokuwa na cheo cha ACP alikuwa anaishi oysterbay.Mwidadi Ali akiwa ACP alishi obey, kastaafu yupo Temeke uswaziuswazi anauza mikate nyumba ina fremu kwa kuwa na yeye ni mswaziswazi.
Mkuu unasema Obey ya wapi ni ile ya Makamo wa Raisi na Waziri mkuu au ile ya kituo cha Polisi nyumba za polisi?, Mimi na sema wajenge Masaki na obey na siyo kuisho nyumba za Serikali.
 
Back
Top Bottom