Tanganian
JF-Expert Member
- Jan 27, 2025
- 7,464
- 12,564
Yeap ,siwezi hata siku moja kuishi ndani kama Mbwa wa kizunguMswahili utamjua tu 🤣🤣🤣🤣🤣
Yeap ,siwezi hata siku moja kuishi ndani kama Mbwa wa kizunguMswahili utamjua tu 🤣🤣🤣🤣🤣
Nakuelewa ndio maana nikachekaYeap ,siwezi hata siku moja kuishi ndani kama Mbwa wa kizungu
Naishi ndani ya geti ,nyumba yangu ila natamani sana kwenda kupanga karibu na kibanda umiza ,au niende mitaa kama makorora huko kwneye vurugu...Mimi siwezi kuishi hizo sehemu hata siku moja ,kama osterbay ,Mbweni .Nakuelewa ndio maana nikacheka
Wenyewe wanasema uache uwanja
Ila kila life style Lina watu wake
😂😂😂😂😅😅😅🤣🤣🤣😀😀😀😃😃😃Acha dharau
Kuishi kwa shemeji yako kusikutoe ufahamu.
hujui raha ya kuishi uswahiliniElewa mada,ishi kulinganana hadhi yako,sasa watu wamekuja msibani hakuna hata pa kufunga hema
Haswaaa.Hao wazee ni ngumu kuwatoa kwenye reli wakishikilia jambo lao
Bibi yangu upande wa Baba alivyokuwa mzee sana alikuja Oysterbay Dar kwa baba yangu kutoka Mwanza kwa ajili ya kuwa karibu na huduma za matibabu.Tulimleta mama mdogo mjini kutoka kijijini, alipokaa mwezi mmoja akasema anataka kurudi kijijini maisha ya town hayataki.
Mkuu uswahilini wanaofariki ni wengi tena kwakusoa laki moja ya matibabu, Kuna jamaa alifariki kwa kukosa laki moja na nusu ya upasuaji wa mgongo huyo jamaa alikua anafanya kazi ya kubeba mizigo bandarini. Nilivyosikia hivyo niliuzunika sana. Kusikia kijana amefariki kwa kukosa laki moja ya matibabu, Uswahili familia zina maisha magumu na wanarogana sana, sehemu za Waswahili siyo sehemu za kuishi kama wewe siyo mswahili maana Kurogana kwingi sana.Hao wa Mbagala ndio wanao fariki tu na wa Upanga hawafariki?
Acha dhihaka mkuu kwa hiyo wanaoishi mbagala hawana akili?"Mtu mwenye akili hawezi kuishi mbagala"Kazi kwelikweli
🤞Familia uzi ndo utanielewa. Mimi nimekopi na kupaste kutoka kweny muandish wa uzi na kuongezea kazi kwelikweli
Huko Masaki atacheza bao na nani? Kijiwe cha kahawa atakipata wapi? Kuna maisha ya uswahilini huwezi kuyapata huko Masaki, hasa kwa mtu aliyezaliwa na kukulia uswahilini.Unaliacha tu kama makumbushi unamuhamusha tu kwa kumshawishi
Kumbuka pia Mshua alikuwa Afande,,sasa nadhani unajua kauli za "Ndiyo Afande" zinavyokuwaga zinasimamiwa kikamilifu.Ni kama unampigia mbuzi gitaa kwenye misimamoMsuva Safi kabisa..kawajengea wazi wake Makamba mawili nyumba Safi Na Fenci yake..hakuna uswahili
Diamond alikula Tandale, but kawajengea nyumba nzuri wazi wake madale Na Sio Tandale
Ukiwa Na Hela lazima ubadirike...kijichi Kuna maeneo mazuri yenye utulivu alitakiwa anunue nyumba nzuri ambapo Mzee anakaa Kwa utulivu
Na kijichi Sio mbali Na mbagala kama mzazi anataka kwenda kuona uswekeni kwake anarudi tu...anakaa Na wadau wake Kisha jioni anarudi kijichi mjengoni
Tubadirike..ukiwa Na Hela jipende, Kwa Sasa hata Yamin Yamali..kawajengea nisema kununua mjumba Wa kifahari wazazi wake Kwa Sasa wanaishi mitaa YA Joshua Na Sio uswazi kama hapo Zamani
Unaposikia dream life...Ni pamoja Na kubadirisha muundo Wa familia..hakuna mzazi ambaye haupendi Kula Maisha YA mwanae akiwa kivulini
Mtu mwenye cheo cha CP wa polisi alikuwa na uwezo wa kufanya makubwa bila msaada wa mwanaeMbagala Zakheem sijui ranfi tatu ni sehemu za ovyo na za hali ya chini sana kwa jijini Dar es salaam
Mahela yote ya wazungu ukashindwa hata kumjengea mzee wako mtoni kijichi
Diamond sio mjinga kuhama Tandale,Bakhresa zamani aliishi Kariakoo ila serikali ilimuhamisha kinguvu,najua hata Sumaye alikuwa na nyumba Mbagala ila alipopata akili na madaraka alihama.
Hakuna Staa mwenye akili atakubali kuishi mbagala hapa nyumba hapa jalala
Mimi sio staa na sina hela ila siwezi kuishi mbagala.
Umemdhalilisha mzee wako
Wachezaji wenzako wa ulaya wakija kukupa pole watakuona wa ajabu sana
Sio kwamba wa masaki hswafi ila wastaafu hawapendi kelele wanapenda kuishi sehemu tulivu,mbagala ni ushenzini
Watu wamekuja msibani hakuna parking,hakuna sehemu ya kufunga hema
Alikuwa Assistant Commissioner of Police na sio Commissioner of police.Mtu mwenye cheo cha CP wa polisi alikuwa na uwezo wa kufanya makubwa bila msaada wa mwanae
Nakumbuka uliwahi kuweka kisa humu cha mbibi alietoka Mwanza vijijini kwenda kutibiwa Dar, aliboreka kukaa sehemu ya kishua kila siku anataka kurudi kwao huko kijijini 😂Mkuu,
Kuna watu wameshazoea mazingira yao ukiwahamisha uwapeleke wewe unapoona pazuri wao wanaona tabu.
In any case hayo ni maamuzi ya familia wewe nani uipangie pa kuishi?
Pole kwa wafiwa.
Unajua mtu ukishaishi sehemu kwa miaka mingi hiyo sehemu kuhama ni ngumu utakuka uliza watoto mpaka wamekua watu wazima ukiambiwa uhame moyo unakataa, yani ata kwawatumishi wa umma utakuta mtumushi kaishi kwenye nyumba ya serikali tokea kija mpaka uzee wa kustaafu umefika siku akiambiwa aondoke kwenye nyumba hanakosa furaha.Mazingira mazuri iko kwenye tafsiri ya mtu binafsi. Kuna mtu mazingira mazuri ni kuona purukushani za wanakitaa, mwingine kuona mbuzi na ng'ombe. Hawa ukiwatoa kwenye asili yao unawavuruga kabisa kama wakina Dudukwe na Chaba. Ukiwaleta huku ambako kila kitu unanua wakati wao wanajua vyote ni bure mtapiga mtaua.
Maisha yale ndio yenyewe. Nimeshashuhudia mzee Sammatta akiwa kwenye moja ya apartments za mwanae. Mnafikiri angemuambia mwanaye nijengee sehemu fulani ingechukua hata mwezi?
Kuna bibi alijengewa na wanaye sehemu nzuri huko kwa washua alihama baada miezi sita. Akiwa peke yake vibaka walimvamia mara 4 na kuiba, na hata wakipiga kelele sauti zinaishia kwenye uzio wao. Akaamua kurudi uswahilini ambako alikuwa anaishi na wapangaji.
Sometimes good life is not good and safe at all
Kweli Uswahili ni fujo tupu umekaa umelala chimbani watu wanakujq kukaa nje ya dirisha lako wanapiga stori na wamama wanachota maji na wengine wanapika vitumbua. Ukijaribu kwenda kukaa sebuleni napo nje fujo watoto wana piga kelele mara unasika kigodoro kinapita, mara jirani kakodi mziki maspeaker makubwa mziki unapigwa.Watu wanasema eti kukaa ndani ya Fensi ni upweke kumbe ni ugumu wa maisha ndio unawafanya hivyo hivi mtu uwe na uhakika wa Kila kitu upweke unatoka wapi kama stori si unatoka kwenye Fensi unaenda kupiga hizo stori
Nakumbuka uliwahi kuweka kisa humu cha mbibi alietoka Mwanza vijijini kwenda kutibiwa Dar, aliboreka kukaa sehemu ya kishua kila siku anataka kurudi kwao huko kijijini 😂
Mtu akizoea mazingira ni ngumu sana kumuhamisha, kuna watu washazoea uswahilini, yale maisha kwao ndio yanawapa utulivu,
Bado ni cheo kikubwa.Alikuwa Assistant Commissioner of Police na sio Commissioner of police.