Mbwana Samatta ilikuwaje ukashindwa kumhamishia baba yako ‘ushuani’ ukakubali afie Mbagala?

Mbwana Samatta ilikuwaje ukashindwa kumhamishia baba yako ‘ushuani’ ukakubali afie Mbagala?

Wazee wengi hawapendi kuhama kwenda mahali ambapo hajapazoea, aanze kutafuta wazee wengine ugenini...Bora atulie uswahilini alikozoea....maisha yetu yanajulikana, hakuna mahali gari inapita kufika nyumbani na nyumbani eneo dogo hakuna Cha kufunga maturubai😄😄 matumizi mazuri ya eneo, hatuishi milele....wake kuomboleza wakae pazuri, wapaki magari vizuri ..haiwezekani
Wakati Samatta anacheza Mazembe (2011 to 2016) huyo mnaemwita mzee hakuwa mzee na mpunga alio vuna pale Mazembe ungetosha kumuhamishia dingi low density area. Hakujawahi kuwa na maisha mazuri uswahilini hata kama umezaliwa huko.
 
Tatizo kwetu mbagalaa hapa nyumba kwetu jalalaaa..hiiiiiiihiiii eeehhh..aaaaah..am baaaak ladies...am baaaak...
Kuishi mbagala hasa zakheim mmm inahitaji wazoefu wengi wametoka kusini ming'oko kwakwenda mbele, Bora nikapange kinyerezi milimani huko 😀😀😀
 
Wazee hukataa kabisa kuhama maeneo yao wamezoeaa company zao......naelewaaa
 
Wako well off kiuchumi ila kichwani hawajielewi
Kuzungukwa na masikini ni kero sana
Hata angeishi masaki angekufa ila hapa tunajaribu kumoa mtu hadhi yake
Wazee wanahitaji maeneo tulivu wajifika umri wa utu uzima
Mbagala sio sehemu sahihi
naunga mkono hoja kuna mwamba kajenga sehemu bonge ya mjengo, ila waliomzunguka kajamba nani, basi bifu za kipuuzi haziishi japo jamaa anajitahidi sana kuishi nao vzuri, ningekuwa na hela hata mbezi ya kimara siishi naapa.
 
Kuna wazee ukimpeleka kuishi osterbay, masaki and the like anafeel yuko keko au segerea
 
Mimi nina umri wa miaka 70 sasa. Ninaishi zangu Dondwe katika nyumba ya jasho langu.

Eti watoto sijui waje wanihamishie wapi - labda wanivute kwa crane!
 
Familia za watu tuziache zilivyo ,huwa moyo unakuwa mzito sana kuzungumzia maswala ya familia zingine ila si mbaya kushauri,
 
Yaani bibi angu hataki kusikia habari za maisha mazuri, alikatzwa aache kugema Ulanzi na kuuza,
Akajibu "mlisoma kupitia nini? Mniache na kazi yangu.
😂😂😂😂😂
Hao wazee ni ngumu kuwatoa kwenye reli wakishikilia jambo lao
 
Wakati Samatta anacheza Mazembe (2011 to 2016) huyo mnaemwita mzee hakuwa mzee na mpunga alio vuna pale Mazembe ungetosha kumuhamishia dingi low density area. Hakujawahi kuwa na maisha mazuri uswahilini hata kama umezaliwa huko.
😀swala sio maisha kuwa magumu au mepesi, ishu ni maziwa tu. Kuhama nyumba uliyoizoea ni kazi ngumu sana😛
 
Tuache kutetea umasikini kama ni sifa vile kwani hao watoto wake walishindwa hata kuiboredha hiyo nyumba ikawa ya kisasa kama mzee aligoma kuhama hapo?au wangewanunua baadhi ya majirani wakaongeza ukubwa wa eneo wakapatengeneza pakawa pa kisasa zaidi kwaiyo mzee angekataa!?hakuna binadamu asiyetaka kuishi vizuri ni uswahili tu unatusumbua hata wazee wa kichaga kuwaamisha kule mgombani sio kazi rahisi ila tunachofanya ni kujenga nyumba ya kisasa na kuwaamishia huko wanabaki hapo hapo mgombani.
 
Ac
Mbagala Zakheem sijui ranfi tatu ni sehemu za ovyo na za hali ya chini sana kwa jijini Dar es salaam
Mahela yote ya wazungu ukashindwa hata kumjengea mzee wako mtoni kijichi

Diamond sio mjinga kuhama Tandale,Bakhresa zamani aliishi Kariakoo ila serikali ilimuhamisha kinguvu,najua hata Sumaye alikuwa na nyumba Mbagala ila alipopata akili na madaraka alihama.
Hakuna Staa mwenye akili atakubali kuishi mbagala hapa nyumba hapa jalala

Mimi sio staa na sina hela ila siwezi kuishi mbagala.
Umemdhalilisha mzee wako
Wachezaji wenzako wa ulaya wakija kukupa pole watakuona wa ajabu sana

Sio kwamba wa masaki hswafi ila wastaafu hawapendi kelele wanapenda kuishi sehemu tulivu,mbagala ni ushenzini

Watu wamekuja msibani hakuna parking,hakuna sehemu ya kufunga hema
Acha fikra potofu kijana, unatumia akili gani hadi kushindwa kutambua maisha yalivyo!!! Ok, umeishi ushuani kama unavyosema, kifo hakikupato??? Sawa, kaburi nalo litakuwa la kishua au??? Acha dharau, mbona mbagala watu wako vizuri tu kimaisha na kiuchumi, mambo ya kitoto usiyatumie ktk maisha, utafeli milele. Kaburi haliangalii uliishi mbagala au ushuani, wote mtaenda mavumbini.
 
Mbagala Zakheem sijui ranfi tatu ni sehemu za ovyo na za hali ya chini sana kwa jijini Dar es salaam
Mahela yote ya wazungu ukashindwa hata kumjengea mzee wako mtoni kijichi

Diamond sio mjinga kuhama Tandale,Bakhresa zamani aliishi Kariakoo ila serikali ilimuhamisha kinguvu,najua hata Sumaye alikuwa na nyumba Mbagala ila alipopata akili na madaraka alihama.
Hakuna Staa mwenye akili atakubali kuishi mbagala hapa nyumba hapa jalala

Mimi sio staa na sina hela ila siwezi kuishi mbagala.
Umemdhalilisha mzee wako
Wachezaji wenzako wa ulaya wakija kukupa pole watakuona wa ajabu sana

Sio kwamba wa masaki hswafi ila wastaafu hawapendi kelele wanapenda kuishi sehemu tulivu,mbagala ni ushenzini

Watu wamekuja msibani hakuna parking,hakuna sehemu ya kufunga hema
Mkuu elewa kwamba mzee Samata amefariki kwa sababu ya sukari na presha. Kuhamia Ulaya au Masaki sio tiba ya sukari au presha.....bado itakuandama tu. Usipotoshe watu hapa mkuu.
 
Kwani lazina kuishi kama maisha fulani🤣🤣 Mbwana kamjengea mzee wake ila msiba umefanyika kwenye nyumba anayomiliki mzee wake ..Hapo ni kwa kina Mbwana alipokulia yeye ,nyumba ya mzee ni private na ishu zote zinafanyika hapo .

Maisha ya kuishi ndani ya fensi kama Mbwa hata mimi yemenishinda kabisa.
Mswahili utamjua tu 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mbwana ana nyumba na apartments sidhani kama swala la kumhamisha mzazi wake ilikuwa shida. Ila mzee akigoma huwezi mlazimisha.

Kuna life wazee wanalichukia kuliishi wanatamani wapate mitaa ambayo wazee wenzao wapo na wanapata fursa za kupiga soga, kucheza bao na draft na siku zikasonga vizuri.

Mzee Kukaa O-Bay ni sawa na kukaa nyumba za wazee Marekani. Changanyikeni kunampa vibe nzuri na kumuondoa msongo wa mawazo ya uzee.
Mkuu,

Hao wazee huwa wana networks zao wanazozipenda wenyewe ambazo wengine ukiwahamisha huwa wanahuzunika sana.

Bibi yangu tulimuhamisha kutoka Sinza kwenye nyumba yake kwenda kuishi Masaki, ikawa kila siku anarudi kukaa Sinza kwake.

Mimi nawaona wazee wangu wakija kutembea Marekani na kufanya checkups/ kuona wajukuu wanavyokuwa wapweke wanatamani warudi Bongo baada ya wiki chache tu. Kwa sababu kule ndiyo kuna networks zao.

Watanzania wengi ni mabingwa wa kutoa ushauri ambao hawajaombwa, kwa watu ambao hawawafahamu, kuhusu mambo wasiyoyajua.
 
Back
Top Bottom