Mbwana Samatta ilikuwaje ukashindwa kumhamishia baba yako ‘ushuani’ ukakubali afie Mbagala?

Mbwana Samatta ilikuwaje ukashindwa kumhamishia baba yako ‘ushuani’ ukakubali afie Mbagala?

Vijiji vingi ni vizuri kuliko Mbagala Kwa maana ya kuishi.
Mbwana ana nyumba na apartments sidhani kama swala la kumhamisha mzazi wake ilikuwa shida. Ila mzee akigoma huwezi mlazimisha.

Kuna life wazee wanalichukia kuliishi wanatamani wapate mitaa ambayo wazee wenzao wapo na wanapata fursa za kupiga soga, kucheza bao na draft na siku zikasonga vizuri.

Mzee Kukaa O-Bay ni sawa na kukaa nyumba za wazee Marekani. Changanyikeni kunampa vibe nzuri na kumuondoa msongo wa mawazo ya uzee.
 
Wako well off kiuchumi ila kichwani hawajielewi
Kuzungukwa na masikini ni kero sana
Hata angeishi masaki angekufa ila hapa tunajaribu kumoa mtu hadhi yake
Wazee wanahitaji maeneo tulivu wajifika umri wa utu uzima
Mbagala sio sehemu sahihi
Upo sahihi alichotakiwa Samatta ni kumjengea nyumba mshua wake maeneo yenye utulivu sio tu nyumba nzuri huko mbagala
 
Kuwahamisha wazee sometimes kuna changamoto sana, kama nyumba aliijenga kwa nguvu zake kumuhamisha hilo eneo ngumu sana.

Nakumbuka tulimjengea bibi yetu nyumba nzuri kubwa, tuliweka maji, umeme na nyumba ipo karibu na huduma za kijamii vizuri. Nia ilikuwa kumsurprise😂😂😂 na yeye akatusurprise.

Simply alisema hii ni nyumba yangu nilijenga na mume wangu na hapa kuna kaburi la mume wangu siwezi ondoka nikamuacha mume wangu.

Wakususa walisusa, wa kuongea waliongea ila mwisho wa siku ilibidi tu tukaboreshe nyumba yake ya mwanzo tu
 
Msuva Safi kabisa..kawajengea wazi wake Makamba mawili nyumba Safi Na Fenci yake..hakuna uswahili

Diamond alikula Tandale, but kawajengea nyumba nzuri wazi wake madale Na Sio Tandale

Ukiwa Na Hela lazima ubadirike...kijichi Kuna maeneo mazuri yenye utulivu alitakiwa anunue nyumba nzuri ambapo Mzee anakaa Kwa utulivu


Na kijichi Sio mbali Na mbagala kama mzazi anataka kwenda kuona uswekeni kwake anarudi tu...anakaa Na wadau wake Kisha jioni anarudi kijichi mjengoni

Tubadirike..ukiwa Na Hela jipende, Kwa Sasa hata Yamin Yamali..kawajengea nisema kununua mjumba Wa kifahari wazazi wake Kwa Sasa wanaishi mitaa YA Joshua Na Sio uswazi kama hapo Zamani

Unaposikia dream life...Ni pamoja Na kubadirisha muundo Wa familia..hakuna mzazi ambaye haupendi Kula Maisha YA mwanae akiwa kivulini
 
Ila acheni ukweli usemwe.
Hiyo sio nyumba jamani..yale ni makazi.
Kwa maana nyingine kile ni kiwanja.

Kwa reputation ya mchezaji mkubwa kama samatta ni aibuu.
Tena Captain wa Tanzania..

Alitakiwa afanye hivi,
Apige nyundo hayo makazi... ajenge nyumba mpya amrudishe baba yake palepale mtaani.

yaani hata sie watendaji tumemzidi sasa wakati sisi tunaishi kwa mihuri tu...Hapana bwana mbwana.

Siajabu hata huo msikiti aliojenga ni mauwongo tu...anyway Pole yake.
 
Ila acheni ukweli usemwe.
Hiyo sio nyumba jamani..yale ni makazi.
Kwa maana nyingine kile ni kiwanja.

Kwa reputation ya mchezaji mkubwa kama samatta ni aibuu.
Tena Captain wa Tanzania..

Alitakiwa afanye hivi,
Apige nyundo hayo makazi... ajenge nyumba mpya amrudishe baba yake palepale mtaani.

yaani hata sie watendaji tumemzidi sasa wakati sisi tunaishi kwa mihuri tu...Hapana bwana mbwana.

Siajabu hata huo msikiti aliojenga ni mauwongo tu...anyway Pole yake.
Naunga mkono hoja
 
1.Kama mwanaume, hapo unaonyesha haupo sawa upstairs.... as wamama (wanawake ndo wapo hivyo)
Sisi wanaume hasa watu wazima wale, akipata sehem Ina banda umiza na kijiwe cha kahawa bas karidhika... ndo mana kikwete myaka yote alipokuwa waziri ilimbidi ahamishie kijiwe nyumbani kwake pale ili kuepuka hatar za kiusalama endapo angeenda kijiwe cha mtaani alichokizoea na alichokuwa akie da akiwa mbunge, mkuu wa mkoa n.k.


2. Kama mwafrika hapo unaonyesha haujui utanzania ni nini na umelelewa vibay .... wazazi wetu kwa kawaida hawawez wakakubari kuendeshwa na hela walizopata watoto wao. Wewe nenda Pata hela oa ishi vizuri na wajukuu zetu basi, kwa sisi tukishindwa kula au hospital tutakwambia.

3. Kama mwanadam unaonyesha ukipata hela utakua mbinde sana... as utawatenga uloish nao kwa myaka mingi sana ila mze samata anahela kitambo na hajawah kuwatenga watu.

Mfano: kwa unachosema bas mo dewji angehamia marekani (ushuani kwa level yake) Azam angehamia hata DUBAI...
 
Mimi huko osterbay ,mbezi beach hata kule Mbweni siwezi kuishi iko wazi ,nitakuwa mpweke sana ...Nyumba yangu ina geti ila najiona kama Mbwa ...Nimehama uswqzi muda ila naishi kange ushuani ,liufupi nimekuwa mnyonge sana bora ya uswqzi.
 
Kama Mbwana kaenda na baba yake Ulaya mara kadhaa mnafikiri wazo la kumjengea halikuwepo?

Kuna wazazi wanaondoka kwa watoto wao kisa choo cha kufrash hakuna cha kulenga na kutumia majani na magunzi. Upweke ni kitu kibaya ambacho wazazi wanapambana nacho baada ya watoto wote kuondoka nyumbani. Halafu umtoe katikati ya watu umpeleke akashinde na ndege tu. Hakubali. Anaona atakufa kesho. Jambo la msingi akigoma boresha maisha hapo alipo ila so kumpeleka sehemu tulivu
 
Back
Top Bottom