Japkas
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 4,074
- 6,617
Mazingira mazuri iko kwenye tafsiri ya mtu binafsi. Kuna mtu mazingira mazuri ni kuona purukushani za wanakitaa, mwingine kuona mbuzi na ng'ombe. Hawa ukiwatoa kwenye asili yao unawavuruga kabisa kama wakina Dudukwe na Chaba. Ukiwaleta huku ambako kila kitu unanua wakati wao wanajua vyote ni bure mtapiga mtaua.Sema nn kuishi mazingira maziri ni unyama sana.
Maisha yale ndio yenyewe. Nimeshashuhudia mzee Sammatta akiwa kwenye moja ya apartments za mwanae. Mnafikiri angemuambia mwanaye nijengee sehemu fulani ingechukua hata mwezi?
Kuna bibi alijengewa na wanaye sehemu nzuri huko kwa washua alihama baada miezi sita. Akiwa peke yake vibaka walimvamia mara 4 na kuiba, na hata wakipiga kelele sauti zinaishia kwenye uzio wao. Akaamua kurudi uswahilini ambako alikuwa anaishi na wapangaji.
Sometimes good life is not good and safe at all