Ni vizuri kujutia makosa ulofanya kwenye maisha yako, lakini haya mambo ya mahusiano sioni sababu kwa mwanaume kuyaweka wazi mitandaoni tena ukimlaumu mwanamke wako eti ana tamaa...akikuzingua we malizana nae kimya kimya mwache aendelee na maisha yake na wewe endelea na maisha yako, piga kimya kiume. Sasa huyu pilipili anaanza mipasho ambayo mwanamke ndo alitakiwa kuongea, sasa hapo mwanamke ni nani kati yao?! Implication yake ni kwamba jamaa ndo loser kwenye hiyo battle ndo maana anaongea ongea mitandaoni ovyo mambo ya ndani na mke wake.