mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Mch. Eliona Kimaro ameonesha ukomavu wa kiroho na wa kiutumishi wa hali ya juu sana. Baada ya kupewa barua ya kutakiwa kuchukua likizo ya siku 60 (ambayo hakuiomba bila shaka maana alipanga kuendesha semina), inayomlazimu kusitisha semina aliyokuwa ameianza hapo kanisani kwake, na kutakiwa kuripoti makao makuu ya KKKT baada ya likizo ili apangiwe kituo kingine, itikio na kauli yake ni hii hapa:
Amesema:
"Mimi ni Mchungaji wa Lutheran ninayeheshimu kiapo changu cha kichungaji na kuishi katika kiapo changu cha kichungaji na maadili pia ya kichungaji kwa neema ya Mungu. Kwa sababu hiyo imenilazimu kutii amri na kwenda kwenye hiyo likizo ya siku 60 na baadae kuripoti kwenye ofisi ya Askofu kama nilivyoelekezwa" Asante.
Kwa kauli hiyo keshaishinda tayari vita inayomkabili hata kama haijaanza. Ushindi mkuu kwa mtu wa Mungu ni kukubali kujivika UNYENYEKEVU! Mch. Kimaro ana nguvu sana hapo kanisani kwake na kila mtu anajua hivyo.
Angeweza kabisa kudai apewe maelezo kwa nini afanyiwe hivyo kwa ghafla na bila shaka angeweza kuliomba baraza lake la wazee lisimame kidete pamoja naye kupinga maamuzi hayo, na nina uhakika sehemu kubwa ya washirika wangemuunga mkono na pangetokea vurugu!! Yeye hakufanya yote hayo!!
Sijasema kuwa Mch Kimaro hana makosa maana sijui undani wa jambo lenyewe, lakini kuna dalili kuwa anaweza kuwa amechezewa mchezo "usio mzuri". Siyo siri kuwa Kanisa la kkkt kijitonyama ni kanisa tajiri na kuna fedha hapo!! KIla mmoja anaitazama hiyo bila kujua kazi kubwa iliyofanyika kuandaa mazingira ya kiroho na kiuwezeshaji hadi kuona matunda hayo yaliyo dhahiri kwa kila mmoja. Kanisa linaloweza kuchanga sh milioni 300 kwa nusu saa siyo mchezo. Usiniambie kuwa ni kwa sababu kuna matajiri hapo la hapana, bali wale watu wameandaliwa vizuri kwa Neno la Mungu, wamelelewa vizuri na mchungaji wao kisha kuweza kutoa maziwa mengi. Kuna mtu anaona maziwa tu lakini kumbe hayo maziwa ni matokeo ya uchungaji bora!
Watu wana asili ya WIVU!! sitashangaa kama sakata zima limejengwa juu ya wivu!! Ilikuwa ni haki ya mch Kimaro kufaidi matunda ya huduma yake hapo kama mchungaji. Hakuna namna ambayo mchungaji hawezi kufaidi maziwa ya kundi analochunga. Sasa wengine hiyo inawauma!! Biblia inasema hivi:
"Ni askari gani aendaye vitani wakati wowote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Je ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi. 1Wakorintho 9:7?"
Ninafahamu katika mazingira haya kuna uwezekano mkubwa wa Mch. Kimaro kutuhumiwa "kula pesa za kanisa" ili kuhalalisha hatua zilizochukuliwa, lakini Mungu wa mbinguni anajua yote!! Kwa wengine kwa mchungaji kunywa katika maziwa ya kundi analochunga kama Biblia inavyoagiza huko wanadai ni "kula pesa za kanisa".
Lakini ukweli ni kwamba kazi ya mchungaji ni pamoja na kula pesa au sadaka za kanisa. Mchungaji akila maana yake Mungu amekula!! Huo ni ukweli tukubali tusikubali!
Yawezekana kuna mtu ana mpango wa kula matunda ya jasho la mwingine, Mungu anajua!
Namtia moyo mch Kimaro kuwa tayari keshaishinda vita kabla hata haijaanza na Mungu atakuwa pamoja naye popote atakapoenda!! Baraka za Kweli za Mungu huwa hazifuatwi bali huwa ZINAMFUATA MTU WA MUNGU!! Ni suala la muda tu watu watalishuhudia hili.
Mch. Kimaro nenda kapige kazi popote Na baraka za Mungu zitakufuata!!! Kama kuna tatizo la msingi napo usikose kulitengeneza kwanza na Mungu atakuwa pamoja nawe!!