Mch. Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama ameishinda vita hata kabla haijaanza. Muda utazungumza

Vijana wengi wanaokidai ni wakristo ni wezi kweli. Sio uongo ni ukweli. Kwa nini tumumumye maneno? Kristo anao wake wasiopiga goti kwa baali ila ni wachache. Tena mno. Uaminifu kwa Wakristo wengi ni ziro japo na mimi ni mkristu. Waache kusingizia hapo
 
Hi jamani kuna nini hapa? kwani nilazima ahubirie humo KKKT?!!!
 
Clip kukubalika ni mpaka ichunguzwe na wataalam waliobobea ili kujua kama ni halisi/authentic! Na gharama ya kufuata mchakato huo siyo ya kitoto maana huchunguza hadi geoposition na actual date and time ambapo picha hizo zilichukuliwa. Siamini kama hgiyo clip inayotembea imepitia mchakato huo. Ndiyo maana kama mahakama haikubali ushahidi wa clip hadi ipitie mchakato huo niliousema!
 
Kwa hiyo hii clip inayotembea imepitia huo mchakato wa kuiwasilisha? Unapozungumzia mchakato lazima ichunguzwe na wataalam waliothibitishwa kuchunguza kama clip hiyo ni halisi kwa maana watataja location/geoposition ya ilipochukuliwea, tarehe na saa ya tukio!! Huo uchunguzi siyo wa kitoto na gharama yake imekwenda shule!!!
 
Kama Kijitonyama ina sadaka kubwa, aliyehamasisha watu watoe ni Kimaro. Na siamini huyo mchungaji kiongozi atakayeletwa atakubalika kama Kimaro.

Tena, Kimaro anaweza kukubali kupata uhamisho aende atakapopelekwa, halafu baada ya miezi michache ajiuzulu uchungaji kama baadhi wa wachungaji wengine wamewahi kufanya
 
Hiyo clip haipo mahakamani, ni mitandaoni tu, mwenye nayo (yaani anayeonekana videoni) ndiye anayeweza kusema kuwa ni ya uongo au la, mpaka sasa hajakana kuhusu clip hizo kuwa anayeonekana sio yeye au ni yeye ila maneno sio yake, hivyo inafanya ziaminike mpaka pale atakapozitolea neno.

Kuhusu mahakamani, hizo vitu hazikataliwi sababu kwa dunia ya leo, teknolojia imekuwa rahisi. Kazi ya kuthibitisha kuwa clip ni bandia nk ni ya anayeipinga, sio ya anayetaka kuitumia kama ushahidi. Na hana haja ya kuleta mageo position na metadata, bali anahoji tu maswali juu ya uhalali wa clip, hapo anaweza kuonesha ubandia wake. Gharama ni kumlipa wakili aulize maswali ya maana kama ya nguli Lissu au Kibatala, hivyo tu.
 
Mkuu kama hufahamu Usharika wa Kijitonyama ulikuwa ndo unaongoza kwa matoleo ya sadaka na mapato kwa ujumla Kwenye Dayosis nzima kwa muda mrefu tu kabla ya ujio wa Mch. Kimaro.. umekuja kupitwa miaka ya karibuni tu hapa na Usharika wa Kimara pamoja na Mbezi Beach... Kwa hiyo kusema kuwa ujio wa mch kimaro ndo uliongeza sadaka si sahihi sana sema tu kuwa kimaro amejitahidi sana kuwaimarisha waumini kiimani na mafundisho yake mengine ya kuichumi kuwajengea waumini uwezo wa uzalizaji.
 
Mahakama inataka kiapo tu kinachoeleza uhalali wa clip, kuwa ilirekodiwa lini, nani aliirekodi, alitumia vifaa gani, vilikuwa ni vizima au la, ilihifadhiwaje, nani aliyehifadhi, imehamishwaje kutoka kifaa kilichorekodi nk.. ukithibitisha hayo, clip inakubalika. Sasa wewe unayepinga kuwa sio halali ndio unaweza fanya hiyo michakato ya geoposition nk hiyo ndiyo position ya sheria kwenye mahakama zetu na si vinginevyo.
 
Niseme tu, hakuna marefu yasiyo na ncha.
Kilichokuwa kinatakiwa kufanyika ni kum demolish Kimaro tangu akiwa Usharika wa Kariakoo.

Kwa miaka mingi tumefanya mbinu na njama mbalimbali kumuondoa lakini hazikuwq na matokeo tuliyo yatarajia. Hivyo tukajaribu mbinu nyingine na nyingine tena, hatimaye leo mbuyu haujaanguka ila umemwagika.

Mara ya kwanza tulipofanya yetu akiwa pale Kariakoo alikimbia usharika na kwenda kujificha kwa Mapadre, na mapadre ndio waliofanya jitihada hadi akarudi tena usharikani, ila hii ya sasa harudi, na akirudi basi itakuwa zamu yetu kusalimu amri.

Kimaro alipokuwa Kariakoo, sio kwamba aliharibu taratibu za ibada hapana, hii ni cover tu, tunayoitumia.

Kimaro alipokuwa Kariakoo aliharibu biashara za wengi kwenye ulimwengu wa roho.

Watu walikuwa na madhabahu zao kubwa ambazo ziliprovide ulinzi wa pesa na mali, pia zikikuwa zikivuta mali kutoka kwa maboya wengine.

Alipofika Kimaro, wale ambao tulikuwa tukizivuta mali zao, wakaanza kumiminika kule kila alfajiri, ulinzi wa mali zao ukaanza kuongezeka, na zile biashara zao ambazo tulizifanya zisionekane na wateja zikaanza kuonekana, na taratibu taratibu wakaanza kukua na kutupora wateja wetu.

Kwa msio na ufahamu wa biashara, hamna biashara isiyo na madhabahu (iwe ya asili au hizo kama za Kimaro), hamna biashara isiye na kuhani, na wala hamna biashara isiyotolewa sadaka/kafara.

Watu wakaanza kufundishwa kutoa sadaka za maneneo na manuizi kwa ajili ya biashara zao, tukapata upinzani sana.

Kwa kushirikiana na wenzetu ndani ya kanisa, tukaanza figisu. Ibada hizo mpya zifutwe na ikiwezekana Kimaro ahamishwe Kariakoo.

Tukafanya Kimaro apitie magumu, tukakausha kabisa hali ya utoaji wa sadaka hadi kanisa likashindwa kulipia umeme na maji, tukahakikisha wanapitia kwenye hali ya ugumu kweli kweli.

Baadae Kimaro anajua alichokifanya, akapindua meza, hali ya uchumi wa kanisa ikaimarika sana, likawa pigo lingine kwetu.

Kipindi kile mkuu wa kanisa alikuwa yule jamaa wa Mbeya, tukafanya kila liwezekanalo ahamishwe. Ndipo akapelekwa Kijitonyama.

Zama zile Kijitonyama alikuwepo dogo mmoja anaitwa Kinyaha, hayo mambo ya ibada za asubuhi yalikuwa hayapo au yamekufa kabisa.

Ibada ilikuwa ikihudhuriwa na vizee vienne, wakizidi sana sita. Sasa alipokuja Kimaro sijajua alikuja na mguu upi, akaleta ibada za asubuhi na usiku.

Watu wakaanza kufurika, akaanza kununua nyumba za watu wetu na kuzifanya kuwa za kanisa. Kijitonyama yote ilikuwa ni ngome yetu.

Kata ya Kijitonyama ndio kata ina vijiji viwili mjini kati Dar es Salaam. Kijiji cha Mwenge na Kijiji cha Makumbusho. Jina na asili Kijitonyama sitaki kulielezea leo, lakini kaa ukijua kuwa ile ni ngome yetu na sehemu yetu ya kulia nyama na vitu vyetu vya kutuongezea nguvu. Kijitonyama ndiko kwenye madhabahu ya kuteketeza, ndio maana hata Wahindi miili yao huchomewa Kijitonyama.

Pale tulijaribu mbinu za kishushu, kuna kipindi tulitaka kumfitinisha na serikali kwa kupitia kijana aliyejinyonga kwa madeni aliyokuwa nayo, lakini alikwepa vihunzi kwa namna ya ajabu kabisa.

Kwetu sisi ni furaha, watu waharibifu aina ya KIMARO hawafai, wakakae huko vyuoni wafundishe. Na tutammaliza kwa njia hiyo.
 
Huko Ofisi ya Askofu aangalie wasije wakamuwekea sumu, Malasusa na Dk. Shoo hawataki mtu awazidi umaarufu achukue uaskofu wao. Wana chuki sana kuliko hata yule mwovu.

Aangalie hizo chai na soda
 
Umeandika vitu gani mkuu?
 

Samaleko Mkuu
 

Umemsikia akikanusha Kua Sio Clip Zake??
 
Umeshaiona clip inayomhusu, au umeamua kuja na porojo tu..
Jee wewe umesoma na kuelewa mleta uzi alichomaanisha? Ndiyo maana mnashindwa mitihani kizembe,soma na uelewe kilichoandikwa kabla hujajibu
 
Samaleko Mkuu
Braza mimi Mkristo. Nimeona vingi mno. Wakristo tumeharubu mfumo wa nchii hii na kumuaibisha Kristo. Mfumo huu kila mtu ni mwizi. Waislamu wa Zanzibar wanaweza kuwa na changamoto nyingi ila uwizi sio mojawapo. Siwasemei wa bara maana wamekua ndani ya mfumo huu wa kikristo. Tunamuabisha Yesu mno. Nahisi akitazama kutoka mbinguni maumivu ni makali mno. Namuomba anioe neema ya kutokumuaibisha.
 
Huko Ofisi ya Askofu aangalie wasije wakamuwekea sumu, Malasusa na Dk. Shoo hawataki mtu awazidi umaarufu achukue uaskofu wao. Wana chuki sana kuliko hata yule mwovu.

Aangalie hizo chai na soda
Tatizo la karibu kabisa pale ni Mch. Anna!!!
Sijui why haoni ila yule bi mkubwa yuko pale kwa mkakati maalum kabisa.ndio aliemchomakwa mashtaka ya siri Jimboni kipindi kile.Bahati nzuri aliekua kaimu katibu ni yule mzee wa Kimara ambae ni jamaa yake sana Kimaro.Yyule mama kakubali kutumiwa na shetani kuharibu kazi ya Mungu
 
Katika kipindi tulichonacho ni muhimu kusimama ktk kujua Mungu kibinafsi, maana ukimtegemea mchungaji akaondoka Imani inaweza yumba Sana, maana kipindi hiki wachungaji, maskofu wengi wapo kivyeo na si kumtumikia Mungu, ndio maana unaweza kuta mashtaka ya kupiga hela za kanisa at kutapeli waumini.. Na mbaya zaidi baadhi ya watumishi hao hao wapo ktk vyama vya waabudu mashetani. .. Hivyo ni rahisi kuharibu yeyote anaetishia himaya ya shetani makanisani
 
Hv ni kweli!! Wale wezi vibaka,panyaroad, mijambazi asilimia kubwa ni wa imani gani?
La msingi tukubaliane kuwa hakuna dini inayofundisha wizi na utapeli. Ni malezi na kiwango cha Roho wa Mungu alichonacho mtu. Hivyo inawezekana kwa kila dini bado vibaka na matapeli wapo ikiwa tu kibinafsi hawakukuzwa kwa malezi mazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…