Mh.Peter Msigwa mbunge wa Iringa mjini(CHADEMA) amesema kuna watu wanampigiapigia simu na kutaka kumshawishi ahamie chama cha mapinduzi (CCM).
Amesema watu hao wanampigia simu na kumtishia kuwa ni bora achukue hela aweze kujianga na CCM maana 2020 yeye, halima, sugu, mnyika, na Lema hata wafanyeje wataondoka tu.
Amesema kuwa kwanza wanaompigia simu wakome kabisa hana bei na hawezi kuuza heshima aliyopewa na wananchi wa Iringa na wakirudia tena atawarecord ili aweze kusamabaza mitandaoni.
CCM ni kama mti wa mchrismas wanajaribu kupamba matunda yanaonekana yanang'aa kumbe ni artificial yanayopambwa na watu wachache waliokosa dira.
Uhalisia kama kweli CCM inafanya kazi au rais Magufuli anafanya kazi Aruhusu democracy ichukue mkondo wake, Aruhusu kukosolewa, Aruhusu haki za binadamu,Aruhusu utawala bora siyo hizi debe anazopigiwa na watu waliokosa dira na kutotambua nini maana ya democracy na utawala bora.