Munambefu
JF-Expert Member
- Jun 24, 2012
- 2,811
- 7,200
Amin Amin nawaambia kwa uzoefu wangu kama mwalimu niliyejistaafisha,hawa waalimu wanaofundisha private zinazotoa division one darasa zima,ukiichukua staff yote mpaka mkuu wa shule ukawapeleka shule B ya serikali utaambulia zero na div 4 za kutosha.
Sijaona mantiki wala na wala hakuna tija yoyote itakayopatikana kwa kumfanyisha mtihani mwalimu.
Mazingira ya kazi yakoje?Mshahara ukoje?Motisha zikoje?
Hivyo ndio vitu vinafanya shule za serikali kufanya madudu wala sio kwamba waalim walioko huko ni viazi.
Nitawapa mfano hai,shule niliyofundisha katika kipindi changu cha ualimu take home ilikuwa 1.2m unapoanza kazi,nyumba,maji umeme,breakfast,lunch,dinner bure.Kila alama A ina bonus ya 20000, B 10000.
Sasa katika mazingira kama hayo mwalimu anaenda na wanafunzi kiulalo ulalo.Yani unakuta waalimu usiku,jmos wako kazini kuhakikisha cv yake haiharibiki kwa kufelisha.
Sasa mwalimu wa serikali anaweza kufanya hivyo?Mshahara chini ya laki 5 ana stress kibao.Hakuna motisha yoyote ya kumfanya atumie msuli za ziada.Hata tungechukua hao madokta na maprofesa wa hayo masomo huko vyuoni tukawapeleka secondary mwendo ni huo huo wa zero.